Haya yakifanyika uhalifu utaisha, panya road watakwisha na raia watakuwa wanalala milango wazi hadi asubuhi

Hii serikali yetu ya sasa kwa kweli inasikitisha mno
 
Muwaue saangapi wakati wanafunga mtaa wanawageuza geuza kama nguo za mtumba mnadani na hakamatwi hata mmoja, saa1:30- saa 3 wanaume wamejificha duu!
Sawa ila mimi nawasubiri kwa hamu huku mtaani kwetu
 
Sasa magufuli ameingiaje hapa. Wasukuma mna tabu sana tangu mjue kingereza
 
Siku ile tulifanya rioting na Mtikila. Asubuhi yake Mrema akatangazwa kuwa Naibu Waziri Mkuu.

 
Aisee kama hawa ndio panya road wenyewe, basi ni aibu kubwa kwa nchi yangu. Haiwezekani vijana wa chini ya miaka 17, na ambao wanaonekana mlo wao ni wa shida kwa siku, eti wawe gumzo kwa nchi nzima. Watoto wanashindia bagia mbili na jagi zima la maji wanapata wapi nguvu za kufunga mtaa na kuiba nyumba kwa nyumba? Enzi za kina Kuveta (Komando Yosso) mtu alikuwa anajifungia ndani na sifuria la ugali, huku ana fungu zima la samaki na pili pili. Akitoka hapo jioni anaenda bondeni au maskani kufanya mazoezi ya ngumi na karate. Yani unakuta komando yosso mmoja ana uwezo wa kunyanyua piki piki kubwa akaiweka begani kama baiskeli na kuondoka nayo. Sasa hawa mbavu za mbwa ndo wanataka kujifananisha na wazee wa kazi komando yosso. Ata bado sana, kwanza hata ujasiri hawana.

 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£ bro umenichekesha sn, ety hawa ndio panya lodi
 
Dah mzee wa "Oparation Mrema" ameondoka na oparation yake. RIP mzee Mrema.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£ bro umenichekesha sn, ety hawa ndio panya lodi
Panya rod wanashindia vipande viwili vya mihogo na kombe 1 la maji, afu wanalaza watu wazima na familia zao saa 2 usiku 🀣🀣🀣
 
Aisee mzee Mrema kaondoka bila kuusoma huu uzi uliomzungumzia yeye kwa kiasi kikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…