Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
- Thread starter
- #121
Hahahaha.. mkuu umenichekesha sana.Basi mkae kwa kutulia hivi vipanya road vinapobaka dada zenu na wake zenu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaha.. mkuu umenichekesha sana.Basi mkae kwa kutulia hivi vipanya road vinapobaka dada zenu na wake zenu.
Hii serikali yetu ya sasa kwa kweli inasikitisha mnoInashangaza kuona serikali mpaka leo imeshindwa kuirudisha OPARATION MREMA. Afu wa halifu wa leo sio kama wa miaka ile. Enzi zile wahuni wengi walikuwa wanacheza ngumi, karate nk. Pia walikuwa na miili iliyoshiba, mtu anakula kilo ya unga na fungu la samaki, afu hawakuwa na masihara hata kidogo, lkn serikali ilipoamua iliwamaliza. Leo hii panya road umri ni 14, 15 hadi 18. Hawana nguvu za mwili wala za mapambano ya kiakili, unakuta panya road anashindia mihogo miwili kwa siku, afu eti wanatingisha mji mzima huku serikali ikiwaangalia tu.
Sawa ila mimi nawasubiri kwa hamu huku mtaani kwetuMuwaue saangapi wakati wanafunga mtaa wanawageuza geuza kama nguo za mtumba mnadani na hakamatwi hata mmoja, saa1:30- saa 3 wanaume wamejificha duu!
Ya kweli mkuu, serikali maneno yamekuwa mengi kuliko vitendo.Hii serikali yetu ya sasa kwa kweli inasikitisha mno
Sasa magufuli ameingiaje hapa. Wasukuma mna tabu sana tangu mjue kingereza"Utadanganya baadhi ya Watu kwa muda mfupi, lakini si wakati wote wa maisha yao yote, popote duniani"
The Late JPM's legacy existence in TZ is still upgrading itself there, due to these roads mouses motions. Hence it was never ever heared, even present at everywhere in his overall presidency [emoji6].
Kwa kweli wanatuchosha mno, yaani mimi nikisikia tu serikali ya CCM inataka kufanya jambo fulani nashikwa na hasira kwa sababu najuwa ni uwongo tuYa kweli mkuu, serikali maneno yamekuwa mengi kuliko vitendo.
acha kabisa walimfanya boka killer hivyoSungusungu ya ngarenaro Arusha ni wamoto enzi hizo
Oparation ile ilikuwa ya aina yake toka nchi yetu ipate uhuru. Na serikali ilifanikiwa kwa kiwango cha 95% kurudisha amani na usalama nchini.Hakika... ilikua operation nzuri sana...
Ucjal mkuu soon tutaanza tena dadekiii zao. We niletee taarifa nianze nao 😂Enzi hizo ilikuwa unapeleka taarifa kimya kimya, usiku wazee wa kazi wanakuja nyumban kwa mtuhumiwa kufanya yao.
Haya mkuu 😂😂🤣🤣Ucjal mkuu soon tutaanza tena dadekiii zao. We niletee taarifa nianze nao 😂
Zamani watu walikuwa na umoja, ndomaana kila walichopanga kilifanikiwa.acha kabisa walimfanya boka killer hivyo
😂😂😂🤣🤣🤣 bro umenichekesha sn, ety hawa ndio panya lodiAisee kama hawa ndio panya road wenyewe, basi ni aibu kubwa kwa nchi yangu. Haiwezekani vijana wa chini ya miaka 17, na ambao wanaonekana mlo wao ni wa shida kwa siku, eti wawe gumzo kwa nchi nzima. Watoto wanashindia bagia mbili na jagi zima la maji wanapata wapi nguvu za kufunga mtaa na kuiba nyumba kwa nyumba? Enzi za kina Kuveta (Komando Yosso) mtu alikuwa anajifungia ndani na sifuria la ugali, huku ana fungu zima la samaki na pili pili. Akitoka hapo jioni anaenda bondeni au maskani kufanya mazoezi ya ngumi na karate. Yani unakuta komando yosso mmoja ana uwezo wa kunyanyua piki piki kubwa akaiweka begani kama baiskeli na kuondoka nayo. Sasa hawa mbavu za mbwa ndo wanataka kujifananisha na wazee wa kazi komando yosso. Ata bado sana, kwanza hata ujasiri hawana.
View attachment 2217729
Dah mzee wa "Oparation Mrema" ameondoka na oparation yake. RIP mzee Mrema.Habari zenu ndugu zangu. Baada ya salam, ningependa niende kwenye mada husika kwa kutumia mifano hai iliyopita.
Katika historia ya nchi yetu toka tapate uhuru mpaka leo, hakuna kipindi kilichokuwa na changamoto za kiusalama kama kipindi cha miaka ya 1989 hadi 1993. Hiki ndio kipindi ambacho nchi ilishuhudia vikundi mbali mbali vya kihalifu kama vile COMANDO YOSSO, RED SOLDIER (red sonja) SIAFU FAMILY, WATOTO WA SHETANI nk.
Kati ya hayo makundi mimi nililijua zaidi kundi la "COMMANDO YOSSO" hili kundi lilikuwa ni kundi hatari kati ya makundi yote yaliokuwepo wakati huo. Kundi hili lilianzishwa na lilikuwa na masikani yake huko Mburahati, ambapo vijana wa kundi hilo walikuwa ni wenyeji wa maeneo hayo ya Mburahati, Kigogo, Mabibo, Manzese, na baadhi ya vijana kutoka maeneo ya Tandale na Kagera mikoroshini pia walikuwemo. Kiongozi mkuu wa kundi hilo alikuwa ni baba yangu mdogo kwa jina alikuwa anaitwa Kuveta R.I.P. Bila shaka wazee, vijana, na watu mbali mbali wa maeneo hayo miaka hiyo walikuwa wanamfahamu aidha kwa kumuona au kumsikia.
Baba yangu mdogo huyo hakuwa katili kivile, ila ukiingia kwenye 18 zake hauwezi kubaki salama. Kwenye 18 zake yeye hakujali wewe ni askari, muhuni mwenzake au nani. Mara nyingi alikuwa na machale kiasi kwamba akikaa maskani akiwaambia tuondokeni basi watakaopuuza baada ya dakika mbili jela itawahusu, japo sometimes na yeye polisi walikuwa wanamuotea, pia alijaaliwa uwezo wa kupambana na adui yeyote.
Alikuwa kaenda hewani, mwili jumba hasa kwa upande wa kifua na mikono, miguu iliyo imarika. Utotoni alijifunza michezo hatari ya ngumi na karate maeneo mbali mbali, swala la kuvunja tofali kwa ngumi au kichwa lilikuwa la kawaida kwake. Kwahiyo alikuwa fit na aliogopeka kweli kweli, maana hata kukamatwa kwake, alikuwa anamatwa na lundo la askari tena wenye silaha za moto.
Hakuna jela ya Tanzania ambayo hakuwahi kufungwa, na kote alipokwenda wababe mkwara walimpa heshima yake, na alikuwa mpaka na tandiko lake. Majambazi, wezi na vibaka wa mchana na usiku waliogopa kuvamia nyumba yoyote ambayo walihisi, au walijua kuwa mwenye nyumba wa nyumba husika ana undugu na Kuveta. Nasikia kuna bongo movie washawahi kucheza sinema yake (japo sijaiona kutokana na kuishi nje ya Tz muda mrefu).
Tukiachana na yeye pia kulikuwa na baadhi ya watemi wengine wa chini yake kina Domokeka, Kaboka mchizi, Chura dume, na wengine wengi wa makundi hayo ambao nimewasahau majina yao. Pia kulikuwa na vikundi vya michiriku ambavyo navyo vilikuwa vikifuga wahuni mbali mbali jijini. Yani hicho ndio kilikuwa kipindi hatari kwa utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi usiokuwa na kipimo, wizi wa usiku na mchana kweupe.
Ilifikia kipindi kukiwa na mnanda karibu yenu basi msicheze mbali na milango au madirisha yenu, au kundi la wahuni linaweza kumteka mwanamk mbele ya mumewe likaenda kufanya mambo yao na wakimaliza wanamuacha arudi kwao nk.
Watu walikatwa mapanga hovyo bila sababu, makundi haya yalimiliki silaha za moto, na za jadi kama vile bunduki, mapanga, shoka nk. Yani hicho ndio kilikuwa kipindi kibaya cha umwagaji damu jijini Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla. Raisi Mwinyi alipoona hali ya usalama nchini inazidi kuwa mbaya ikabidi amteuwe mh Augustino .L. Mrema kuwa waziri wa mambo ya ndani.
Mrema alipoteuliwa akaapa kuyatokomeza makundi hayo kwa kuandaa oparation maalumu ya polisi, wakishirikiana na sungu sungu ambao yeye (Mrema) ndo muasisi. Basi bwana shughuli ikaanza huku Mrema mwenyew akiwa mstari wa mbele katika oparation ile.
Kwa vile serikali ilishirikisha sungu sungu ambao ni wananchi wa maeneo mbali mbali ya jiji, basi ilikuwa rahisi kuwatambua kimya kimya wahusika wa makundi yale pamoja na wahalifu wengine. Ikawa wakijua nyumba fulani kuna kijana muhalifu wazee wa kazi askari wakishirikiana na sungu sungu wanakuja usiku wanagonga mlango askari wanaingia, wanamchomoa waliemfuata wanaondoka nae. Kama wewe ni mzazi au ndugu, basi asubuhi utaletea taarifa na mjumbe kuwa uende sehemu fulani ukachukue mzoga wako uuzike.
Oparation hii haikushia kwenye nyumba tu bali mpaka kwenye maskani zao walifuatwa na kuangamizwa huko huko. Nakumbuka bamdogo Kuveta aliuwawa siku ya tatu tu akiwa ametoka jela. Akiwa ameenda kulala kwa demu wake, siku hiyo ghafla usiku walivamiwa na kundi la watu zaidi ya 50 wakiwemo askari wenye silaha na sungu sungu wenye mapanga na kuanza kumshambulia.
Maiti yake tulikuta ikiwa na majeraha makubwa kwenye maungio ya mikono yake, kifuani na kichwani. Tulipomuuliza demu wake akasema alipata yale majeraha ya mikononi baada ya kupambana na askari mwenye silaha, ambapo sungu sungu waliona angefanikiwa kumpokonya askari ile bunduki basi ingekuwa hatari kwa uhai wao, so suluhisho likawa ni kuikata mikono yake kwa mapanga japo hiyo haikumfanya aache kupambana, ndipo wakaamia kichwani na kifuani so kutokana na kuvuja sana kwa damu akaishiwa nguvu akaanguka na kufariki.
Pia yule demu wake walimjeruhi baadhi ya sehemu za mwili wake, ila hawakumuua. Baada ya mauaji hayo ya wahalifu mbali mbali, wizi ukapungua kama sio ukaisha kbs jijini Dar es salaam. Vikundi vya michiriko (minanda) navyo vikaanza kusambaratika, amani ikarejea.
Watu wakaanza kuishi kama Saudia Arabia ambapo mida ya sala inafika, watu wanaenda kusali huku wakiwa wameacha biashara zao wazi kabisa. Sasa inashangaza sasa hivi vipanya road vyenye umri wa miaka 14, 15 hadi 18 vinafunga mtaa wa wanaume wenye umri mkubwa na kuchukua kila kitu ndani ya majumba yao.
Kwanini ile oparation maalumu ya Mrema isirudie kuwamaliza mbwa hao. Au polisi kwanini wasishirikane na wananchi (sungu sungu) kwa style ile ile waliyotumia wenzao kumaliza ushenzi huo unaoendelea kwa kasi jijini na nchini kwa ujumla? Watanzania tuiombe serikali irudishe OPARATION MREMA, huu uhalifu utaisha mara moja.
Panya rod wanashindia vipande viwili vya mihogo na kombe 1 la maji, afu wanalaza watu wazima na familia zao saa 2 usiku 🤣🤣🤣😂😂😂🤣🤣🤣 bro umenichekesha sn, ety hawa ndio panya lodi
Aisee mzee Mrema kaondoka bila kuusoma huu uzi uliomzungumzia yeye kwa kiasi kikubwa.Habari zenu ndugu zangu. Baada ya salam, ningependa niende kwenye mada husika kwa kutumia mifano hai iliyopita.

Samahan mkuu kwa kuuliza. Kwani kazi ya bodi ya parole ilikuwa ni nini?Wamrudishe Mrema kuwa mshauri
😂😂😂😂Panya rod wanashindia vipande viwili vya mihogo na kombe 1 la maji, afu wanalaza watu wazima na familia zao saa 2 usiku 🤣🤣🤣