Haya yakifanyika uhalifu utaisha, panya road watakwisha na raia watakuwa wanalala milango wazi hadi asubuhi

Haya yakifanyika uhalifu utaisha, panya road watakwisha na raia watakuwa wanalala milango wazi hadi asubuhi

Mkuu huyu mbona ukifuatilia maelezo yake mengi, anaonekana ni msaka fursa tu wa sadaka kupitia kanisa. Kwa wakongwe tuliozaliwa na kuishi Dar miaka hiyo hasa maeneo ya mburahati, mabibo, kigogo manzese hatukuwahi kuumfahamu huyu mwamba, labda kutokana na umri pengine muonekano wake umebadilika sawa. Lakini Commando Yosso asili yake ni maeneo hayo niliyoyataja na huyo Kuveta ninaekwambia hakuna mtu wa miaka hayo na maeneo hayo ambae alikuwa hamjui. Nakwambia mpaka jamaa wa bongo movie nasikia walicheza cinema kuhusu maisha ya mtemi huyo, japo wachezaji wa bongo movie hao inasemekana waliweka chumvi nyingi kama kawaida yao. Laiti nikibahatika kuipata hivyo movie nitaiweka hapa, japo na yenyew haizungumzii maisha yake halisi kutokana na kujaza machumvi mengine movini.
Kuveta anamjua huyo mwamba.
Ni mmoja ya members wa Yosso kundi la fire.
Umri umeenda hio ni flashback yake
 
Habari zenu ndugu zangu. Baada ya salam, ningependa niende kwenye mada husika kwa kutumia mifano hai iliyopita.

Katika historia ya nchi yetu toka tapate uhuru mpaka leo, hakuna kipindi kilichokuwa na changamoto za kiusalama kama kipindi cha miaka ya 1989 hadi 1993. Hiki ndio kipindi ambacho nchi ilishuhudia vikundi mbali mbali vya kihalifu kama vile COMANDO YOSSO, RED SOLDIER (red sonja) SIAFU FAMILY, WATOTO WA SHETANI nk.

Kati ya hayo makundi mimi nililijua zaidi kundi la "COMMANDO YOSSO" hili kundi lilikuwa ni kundi hatari kati ya makundi yote yaliokuwepo wakati huo. Kundi hili lilianzishwa na lilikuwa na masikani yake huko Mburahati, ambapo vijana wa kundi hilo walikuwa ni wenyeji wa maeneo hayo ya Mburahati, Kigogo, Mabibo, Manzese, na baadhi ya vijana kutoka maeneo ya Tandale na Kagera mikoroshini pia walikuwemo. Kiongozi mkuu wa kundi hilo alikuwa ni baba yangu mdogo kwa jina alikuwa anaitwa Kuveta R.I.P. Bila shaka wazee, vijana, na watu mbali mbali wa maeneo hayo miaka hiyo walikuwa wanamfahamu aidha kwa kumuona au kumsikia.

Baba yangu mdogo huyo hakuwa katili kivile, ila ukiingia kwenye 18 zake hauwezi kubaki salama. Kwenye 18 zake yeye hakujali wewe ni askari, muhuni mwenzake au nani. Mara nyingi alikuwa na machale kiasi kwamba akikaa maskani akiwaambia tuondokeni basi watakaopuuza baada ya dakika mbili jela itawahusu, japo sometimes na yeye polisi walikuwa wanamuotea, pia alijaaliwa uwezo wa kupambana na adui yeyote.

Alikuwa kaenda hewani, mwili jumba hasa kwa upande wa kifua na mikono, miguu iliyo imarika. Utotoni alijifunza michezo hatari ya ngumi na karate maeneo mbali mbali, swala la kuvunja tofali kwa ngumi au kichwa lilikuwa la kawaida kwake. Kwahiyo alikuwa fit na aliogopeka kweli kweli, maana hata kukamatwa kwake, alikuwa anamatwa na lundo la askari tena wenye silaha za moto.

Hakuna jela ya Tanzania ambayo hakuwahi kufungwa, na kote alipokwenda wababe mkwara walimpa heshima yake, na alikuwa mpaka na tandiko lake. Nasikia kuna bongo movie washawahi kucheza sinema yake (japo sijaiona kutokana na kuishi nje ya Tz muda mrefu).

Tukiachana na yeye pia kulikuwa na baadhi ya watemi wengine wa chini yake kina Domokeka, Kaboka mchizi, Chura dume, na wengine wengi wa makundi hayo ambao nimewasahau majina yao. Pia kulikuwa na vikundi vya michiriku ambavyo navyo vilikuwa vikifuga wahuni mbali mbali jijini. Yani hicho ndio kilikuwa kipindi hatari kwa utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi usiokuwa na kipimo, wizi wa usiku na mchana kweupe.

Ilifikia kipindi kukiwa na mnanda karibu yenu basi msicheze mbali na milango au madirisha yenu, au kundi la wahuni linaweza kumteka mwanamk mbele ya mumewe likaenda kufanya mambo yao na wakimaliza wanamuacha arudi kwao nk.

Watu walikatwa mapanga hovyo bila sababu, makundi haya yalimiliki silaha za moto, na za jadi kama vile bunduki, mapanga, shoka nk. Yani hicho ndio kilikuwa kipindi kibaya cha umwagaji damu jijini Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla. Raisi Mwinyi alipoona hali ya usalama nchini inazidi kuwa mbaya ikabidi amteuwe mh Augustino .L. Mrema kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Mrema alipoteuliwa akaapa kuyatokomeza makundi hayo kwa kuandaa oparation maalumu ya polisi, wakishirikiana na sungu sungu ambao yeye (Mrema) ndo muasisi. Basi bwana shughuli ikaanza huku Mrema mwenyew akiwa mstari wa mbele katika oparation ile.

Kwa vile serikali ilishirikisha sungu sungu ambao ni wananchi wa maeneo mbali mbali ya jiji, basi ilikuwa rahisi kuwatambua kimya kimya wahusika wa makundi yale pamoja na wahalifu wengine. Ikawa wakijua nyumba fulani kuna kijana muhalifu wazee wa kazi askari wakishirikiana na sungu sungu wanakuja usiku wanagonga mlango askari wanaingia, wanamchomoa waliemfuata wanaondoka nae. Kama wewe ni mzazi au ndugu, basi asubuhi utaletea taarifa na mjumbe kuwa uende sehemu fulani ukachukue mzoga wako uuzike.

Oparation hii haikushia kwenye nyumba tu bali mpaka kwenye maskani zao walifuatwa na kuangamizwa huko huko. Nakumbuka bamdogo Kuveta aliuwawa siku ya tatu tu akiwa ametoka jela. Akiwa ameenda kulala kwa demu wake, siku hiyo ghafla usiku walivamiwa na kundi la watu zaidi ya 50 wakiwemo askari wenye silaha na sungu sungu wenye mapanga na kuanza kumshambulia.

Maiti yake tulikuta ikiwa na majeraha makubwa kwenye maungio ya mikono yake, kifuani na kichwani. Tulipomuuliza demu wake akasema alipata yale majeraha ya mikononi baada ya kupambana na askari mwenye silaha, ambapo sungu sungu waliona angefanikiwa kumpokonya askari ile bunduki basi ingekuwa hatari kwa uhai wao, so suluhisho likawa ni kuikata mikono yake kwa mapanga japo hiyo haikumfanya aache kupambana, ndipo wakaamia kichwani na kifuani so kutokana na kuvuja sana kwa damu akaishiwa nguvu akaanguka na kufariki.

Pia yule demu wake walimjeruhi baadhi ya sehemu za mwili wake, ila hawakumuua. Baada ya mauaji hayo ya wahalifu mbali mbali, wizi ukapungua kama sio ukaisha kbs jijini Dar es salaam. Vikundi vya michiriko (minanda) navyo vikaanza kusambaratika, amani ikarejea.

Watu wakaanza kuishi kama Saudia Arabia ambapo mida ya sala inafika, watu wanaenda kusali huku wakiwa wameacha biashara zao wazi kabisa. Sasa inashangaza sasa hivi vipanya road vyenye umri wa miaka 14, 15 hadi 18 vinafunga mtaa wa wanaume wenye umri mkubwa na kuchukua kila kitu ndani ya majumba yao.

Kwanini ile oparation maalumu ya Mrema isirudie kuwamaliza mbwa hao. Au polisi kwanini wasishirikane na wananchi (sungu sungu) kwa style ile ile waliyotumia wenzao kumaliza ushenzi huo unaoendelea kwa kasi jijini na nchini kwa ujumla? Watanzania tuiombe serikali irudishe OPARATION MREMA, huu uhalifu utaisha mara moja.
JPM alijaribu kwa wale wahuni wa Amboni na Rufiji, wapuuzi akina Zitto na Lissu hadi leo ni kumlaumu
 
Nimeguswa!. Very touching story.
Sijapenda jinsi starring alivyo uwawa bila kosa lolote!.
Wale wote walio husika kumuua kamanda huyu bila kosa lolote, karma inawahusu.

RIP Kuveta, Kamanda wa Commando Yosso.
 P
Damu ya mchawi, mwizi, jambazi hizi hazina karma wala laana yeyeto,wala hazina password kama damu za watu wasio hatia.
Bullets ndio njia sahihi ya kusafisha takataka kwenye Jamii.Rwanda, South Africa,USA wametumia matokeo ni 100% archive.
 
Mkuu huyu mbona ukifuatilia maelezo yake mengi, anaonekana ni msaka fursa tu wa sadaka kupitia kanisa. Kwa wakongwe tuliozaliwa na kuishi Dar miaka hiyo hasa maeneo ya mburahati, mabibo, kigogo manzese hatukuwahi kuumfahamu huyu mwamba, labda kutokana na umri pengine muonekano wake umebadilika sawa. Lakini Commando Yosso asili yake ni maeneo hayo niliyoyataja na huyo Kuveta ninaekwambia hakuna mtu wa miaka hayo na maeneo hayo ambae alikuwa hamjui. Nakwambia mpaka jamaa wa bongo movie nasikia walicheza cinema kuhusu maisha ya mtemi huyo, japo wachezaji wa bongo movie hao inasemekana waliweka chumvi nyingi kama kawaida yao. Laiti nikibahatika kuipata hivyo movie nitaiweka hapa, japo na yenyew haizungumzii maisha yake halisi kutokana na kujaza machumvi mengine movini.

Kaigiza yule bonge wa mchezo wa Kombolela[emoji1787]
 
Ukitaka kumaliza vibaka, panyaroad ni kuuwa Mkubwa wao watasambaratika. Hakuna njia sahihi ya kudeal na watu primitives nje ya primitives way.
Njia ni watu kupata kazi ajira zinaondoa wahalifu na wauza miili
 
Operation Kama hii ishawahi kufanyika miaka kadhaa huku kwetu mkoani (nafikiri ni miaka karibu kumi hv). Wakati huo kulikuwa na Kijiji jirani ambacho kilijaa wahuni, wezi na wababe ilikuwa mkicheza nao mpira mkiwafunga kichapo kinawahusu hata wakishinda bado wataanzisha vurugu ilimradi tu kuonesha ubabe, mtu ukienda na usafiri wako huko(baiskeli wkt huo) jamaa wanapita nayo. Sasa ilifikia hatua raia walichoka na vurugu zao wakaandaa mkakati wa kumsaka mmojammoja popote walipo dah walipukutishwa wote nakumbuka mmoja tulisoma nae jamaa aliuliwa kikatili Sana na wanakijiji na ndo alikuwa mwizi konki alikimbizwa na kundi la raia akakimbilia mtoni alifuatwa hukohuko akapigwa ndani ya maji mpaka akafa.
Nowdays full amani
Safi
 
Operation Kama hii ishawahi kufanyika miaka kadhaa huku kwetu mkoani (nafikiri ni miaka karibu kumi hv). Wakati huo kulikuwa na Kijiji jirani ambacho kilijaa wahuni, wezi na wababe ilikuwa mkicheza nao mpira mkiwafunga kichapo kinawahusu hata wakishinda bado wataanzisha vurugu ilimradi tu kuonesha ubabe, mtu ukienda na usafiri wako huko(baiskeli wkt huo) jamaa wanapita nayo. Sasa ilifikia hatua raia walichoka na vurugu zao wakaandaa mkakati wa kumsaka mmojammoja popote walipo dah walipukutishwa wote nakumbuka mmoja tulisoma nae jamaa aliuliwa kikatili Sana na wanakijiji na ndo alikuwa mwizi konki alikimbizwa na kundi la raia akakimbilia mtoni alifuatwa hukohuko akapigwa ndani ya maji mpaka akafa.
Nowdays full amani
Hili tukio kama nalikumbuka vile jamaa alikua anaitwa Willington
 
Kabisa mkuu Hawa jamaa wa mapindi hayo unakuta linabeba vyuma, walikuwa wanaogopeka mtaani mtu anaibiwa unaona kabisa ila unakausha husemi.
Hivi vya sasa hivi vitoto kabisa tunavilealea yaani ukifanikiwa kukakaba kamoja kwenye angle unakaua kabisa
Hahaha.. unamkuta panya road hana hata kilo 25 za uzito, mlo wake kwa siku ni bagia mbili na jagi zima la maji, mfukoni ana bisibisi au kisu cha mkunjo afu usiku anafunga mtaa mzima 🤣🤣🤣😂😂.
 
RPC Saba sita baba yake tunda aliyasambaratisha makundi ya wahuni Arusha, huku RPC Sanya aliwasambaratisha wahuni wa Mbeya. Tibaigana akayasambaratisha ya Dar. Sasa hawa Ma RPC wa sasa wanafeli wapi.
Hata mimi nashangaa mkuu. RPC ana askari wa kutosha, silaha za kutosha na pia anaweza kupata msaada wa kuwafaham wahalifu kupitia raia wema, afu akaanza kufanya yake kimya kimya, mpaka watu watapokuja kushtuka tayari kaisha wamaliza. Sijui RPC anashindwaje kuanzisha OPARATION MREMA.
 
Yes, ni kama ulivyosema ni alikuwa!. Mtu ametoka jela juzi, hajafanya uhalifu wowote, yuko kwa demu wake, watu unamwingilia usiku kumvamia, kumkatakata mapanga, kumuua na kumjeruhi demu wake!. Wahusika wote karma itawahusu.
P
Yeye aliua wangapi mpaka kufikia hapo? Na vipi kama kilichomkuta ndio ilikua malipo ya Karma kwake.
 
Back
Top Bottom