Haya yalikuwa makosa ya kimkakati-Yametupokonya fursa

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Anaandika
Askofu Bagonza Kalikawe Lwakalinda

Taifa linahitaji Maridhiano. Yawe ya kweli au ya hila, ni muhimu kutambua makosa matatu ya kimkakati yaliyotupokonya fursa na sifa nzuri ya taifa letu. Kwa uwazi au kwa siri tujutie haya:

1. Kumfunga Freeman Mbowe kwa miezi 8.
Ndani ya CDM na CCM wamo wanasiasa wenye misimamo mikali (radicals). Mbowe alipokuwa kifungoni, radicals walikiteka chama. Watu kama Lisu, Lema, Sugu, Heche, Msigwa, Wenje na wengine, walijiimarisha kwenye chama wakati Mbowe yuko gerezani. CCM na serikali wakakosa mtu wa “kuridhiana” naye kwa sababu aliyekuwa akiwasaidia walimweka gerezani. Alipoachiwa, chama kiliishaenda mikononi mwa radicals. Mbowe aliwahi kuionya serikali lakini haikujali. Aliyeshauri Mbowe awekwe ndani, shetani anamuona

2. Kukataa Maridhiano kabla ya Uchaguzi wa 2025.
Radicals ndani ya CCM walikataa maridhiano kabla ya uchaguzi. Wangeweza kwenda mezani na “kuwatuliza” radicals wa CDM na kuwaingiza kwenye uchaguzi halafu goli la mkono lisingekomba kila kitu bali lingeacha masalia ya wabunge na madiwani. Kwa CCM kukataa maridhiano kukawafanya radicals wa CDM kugomea uchaguzi. Kilichotokea Oktoba 29 kingeepukwa kama CCM ingekubali maridhiano. Kukataa maridhiano lilikuwa kosa kubwa la kimkakati.

3. Kumweka ndani Tundu Lissu.
Radicals ndani ya CCM na mfumo walishinikiza Lisu akamatwe na kufunguliwa kesi mbaya. Hatua hii ika-radicalize sehemu kubwa ya CDM. Pia, hatua hii ikaigawa hata CCM, jumuia ya kimataifa, hata na taasisi nyeti zenye utakatifu fulani ndani na nje ya serikali. Utekaji wa wana CCM na wapinzani, ukafunga uwezekano wa maridhiano. Kwa mara ya kwanza, hata viongozi wakuu “wakaonekana” kupoteza mwelekeo na kuwa radicals. Badala ya maridhiano wakaanza kuimba “surrender” - kujisalimisha tu!

Mpaka hapa tukubaliane: Tulimfunga Mbowe, radical wakachukua chama. Tumemfunga Lissu, chama chote kimekuwa radicals. Kuwekana ndani si dawa nzuri ya kushughulikia upinzani.

Makosa haya matatu ya kimkakati yameifanya nchi ionekane imejiteka, imejifunga pingu na kupoteza funguo. Fursa nyingi za kumaliza jambo hili kisiasa zimepotea. Mahakama zinateseka kulimaliza huku zimefungwa au kujifunga pingu mikononi na miguuni.

CDM ina misimamo mikali. CCM ina misimamo mikali na jeuri. Mbowe alipokuwa madarakani alidhalilishwa na CCM mpaka CDM ikamweka chini. Sasa dola inamwona Mbowe wa maana wakati ni yenyewe ilimwangusha?! CDM sasa inamzodoa aliyekuwa mwamba wao. Mwe! Bora ukose akiba ya chakula lakini uwe na akiba ya maneno.

Kama hayati Lowasa. Alichafuliwa na kusafishwa na vyama vyote CCM na CDM. Alikufa akiwa mshindi kwa vyote.

Wazee wa Kikurya husema “Mdharau mwiba..”, lakini wajanja wa Kijaluo wao husema, “unaweza kudharau siafu lakini usiwakalie kwa makalio yasiyo na kinga”.
 
Hakika amenena. Na haitakuwa kama walivyozoea teeena!
 
Askofu nae kawageuka walugaluga na waporipori waliovamia siasa kutoka vijijini
 
useless Kalikawe B with nonsense articles 🐒
 
CVM ni chanzo cha ugaidi, uhaini na umwagaji wa damu nchini.

Samia ndiye nyuma ya haya yote.
 
Screenshot_20260816-150515~2.png
 
Back
Top Bottom