Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwaka 1982, kijiji cha Lubasazi kilichopo Kata ya Kolero, Wilaya ya Morogoro Vijijini, kilipata msiba mzito. Mzee wa heshima kijijini hapo alifariki. Halikuwa jambo la kawaida watu walianza kusema yule Mzee hakufariki kifo cha kawaida, kuna mkono wa watu. Baada ya mazishi maisha yaliendelea kama kawaida, shughuli za hapa na pale zikawa zinaenda kama ilivyo kawaida.
Baada ya Miaka kupita serikali iliamua kujenga shule ya msingi pale kijijini, wakazi wa kijiji kile waliambiwa wahamishe makaburi ya kifamilia kwenda eneo jipya kupisha ujenzi wa shule ya msingi. Moja ya makaburi hayo lilikuwa la Bibi Ajuza.
Bibi Ajuza alikuwa mganga wa jadi. Alisaidia watu wengi, lakini pia alihusishwa na uwezo wa ajabu. Watu waliogopa kumuudhi hata baada ya kufaliki alikuwa akiheshimika sana. Baada ya kuzikwa upya, ndipo mambo ya ajabu yakaanza.
Usiku wa kwanza baada ya kaburi lake kuhamishwa, walinzi wa shule mpya walisema kuwa walisikia sauti ya mwanamke mzee akiimba kwa sauti ya huzuni nyuma ya darasa la pili. Walipowasha tochi hawakuona mtu. Lakini pale kwenye lile Kaburi jipya mchanga wa kaburi ulikuwa bado unatoa joto. Hali ile ilishangaza sana watu wa kijiji kile.
Baada ya siku kadhaa, wakazi wa kijiji walianza kuota ndoto za ajabu. Kila mtu aliyepita karibu na kaburi alipata hisia za kama kuna mtu anamtazama. Watoto walikatazwa kucheza karibu na eneo hilo, waliambiwa “Bibi wa kaburini anahema.”
Siku moja, mida ya usiku moja ya kijana wa kijiji kile aliyekuwa amechelewa kurudi kutoka shambani alipita karibu na kaburi hilo. Alisikia sauti za ajabu sana, Alirudi kijijini akikimbia, akisema alisikia kaburi likisema: “Kwa nini mlinihamisha? Hapa si nyumbani.”
Mara moja Wazee wa kijiji waliitwa kujadili juu ya swara hilo la kushangaza pale kijijini. Walijaribu kufanya tambiko dogo, wakimwaga maziwa na asali kama ilivyo mila na desturi zao. Lakini mambo yalizidi kuwa mabaya. Siku iliyofuata, mwalimu mkuu wa ile shule alipata vidonda miguuni pasipo sababu.
Ndani ya mwezi mmoja, walimu wawili walihama toka kwenye ile shule na kuhamia shule nyingine, huku wakidai kuwa wanaota mwanamke mzee akiwaambia warudishe kaburi lilipokuwa awali. Jamaa mwingine alidai kuwa alilazimika kuhamia Ifakara baada ya kuugua bila kwa ghafla.
Mwenyekiti wa kijiji aliamua kuita mtaalamu kutoka Ifunda. Huyu mzee wa mitishamba alifika na alikaa usiku kucha karibu na kaburi. Aliporudi kijijini asubuhi alisema kuwa
“ule sio mzimu wa kawaida.una masikitiko. Alizikwa bila heshima ya mwisho.”
Baada ya uchunguzi, iligundulika kuwa Bibi Ajuza hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa mlinzi wa kiroho wa familia na ukoo mmoja pale kijijini. Kaburi lake liliwekwa mahali maalum na hakupewa tambiko alilowaachia kwenye wosia.
Wazee waliamua kufanya tambiko rasmi. Walichinja mbuzi mweupe, wakaimba nyimbo za jadi, na wakaweka vitu vyake vya zamani hirizi, shanga, na kibuyu cha dawa juu ya kaburi lake.
Tangu siku hiyo, sauti za usiku zilitoweka. Watoto walianza tena kucheza karibu na eneo hilo. Watu walisema, “Bibi ameridhika.” Lakini hadithi haikuishia hapo…
Lakini Mwaka 2018, kijana mmoja alihamishwa kutoka shule ya mjini aje kufundisha Lubasazi. Alikaa kwenye nyumba za walimu karibu na kaburi hilo. Miezi miwili baadaye, alianza kusikia sauti usiku zikimuita kwa jina lake.
Wakati mwingine sauti hiyo ilimuita kwa upole, ikimwambia: “Hujaomba ruhusa.”alienda kuwaeleza walimu wenzake, alielezwa kuwa kabla ya kuishi karibu na kaburi la Bibi Ajuza , lazima utoe heshima hata kwa kutoa tu maua au dua kama heshima kwake.
Alipofanya hivyo, matatizo yote aliyokuwa anakutana nayo kama vile, kutoelewana na wanafunzi, ndoto mbaya, uchovu usioeleweka vilitoweka.
Mpaka leo, wakazi wa Lubasazi wanaamini Ajuza Bibi bado anaangalia kijiji. Wengine hupeleka watoto wake wagonjwa karibu na kaburi lake na kuomba kwa upole na watoto wale hupona.
Wakuu wa wilaya waliowahi tembelea eneo hilo walisema wanalitambua kama “eneo la urithi wa utamaduni.” Lakini wenyeji wanaona zaidi ya urithi wanaona uhai wa kweli.
Kuna msemo maarufu kijijini husema "Ukimuona Bibi Ajuza usiku, ujue kuna ujumbe toka kwake. Msiogope, msimkimbie – msikilizen."
Siku hizi, kaburi lake linatunzwa. Wageni wanaonywa kuwa si kila mahali ni pa kupiga picha. Heshima ni muhimu. Hata wakati wa kiangazi, eneo la kaburi lake hubaki na mvuke na harufu ya manukato ya jadi.
Watu wa Lubasazi hawasemi tena “kaburi linaloongea kwa hofu, bali kwa heshima. Kwani, kwao, bibi Ajuza hakufa. Anaishi, kupitia kumbukumbu, ndoto, na sauti za usiku