Haya yanayotokea sasa ni Marudio yalishatokea. "NITAUFANYA MGUMU MOYO WA FARAO ....."

Haya yanayotokea sasa ni Marudio yalishatokea. "NITAUFANYA MGUMU MOYO WA FARAO ....."

Hivi hawa Chadema kusema uchaguzi usifanyike hadi Reforms zifanyike ili uwe uchaguzi wa HAKI NA HURU ni kosa?
Sasa ona masahibu wanayopitia. Viongozi wao wanatekwa,kuuawa, kushambuliwa, sasa hivi wanazuiwa kusafiri, chama kinyimwa ruzuku, chama kimewekewa zuio haramu kufanya kazi, na kubwa kuliko yote Kiongozi mkuu kawekwa gerezani kiuonevu tuu kwa kesi mbaya sana.
Jee wanastahili hayo yote wakati wanayafanya kikatiba?
Hivi hao washauri wa Farao hawamshauri vizuri kuhusu hili au wao ndio wanachochea ili machafuko yatokee wakimbie wakafaidi rasilimali walizojichotea?
Au haya ni mapenzi ya MUNGU ili litimie analolitaka?
Maana Waisrael walipotaka kuondoka utumwani Misri Farao alikataa na kuongeza mapigo. Na demand ilipoongezeka Mungu naye akaufanya moyo wa Farao uwe mgumu ili aje ajidhihirishe na historia ije iandikwe!
Jee Farao wetu anaenda kuandika historia mpya baada ya moyo wake kufanywa mgumu?
NO REFORMS, NO ELECTION.
 
Faraoh amesaidia kuipeleka No Reforms No Elections kwa wananchi. Sasa hivi asiyepata tiba hospitali anafahamu kwamba tunahitaji reforms, anaewekwa mahabusu kwa uonevu anafahamu tunahitaji reforms. Hata lile panga lililopita wilayani katika kinyang’anyiro cha ubunge limewaacha wengi wakitafakari kuhusu reforms.
Hakika
 
Hivi hawa Chadema kusema uchaguzi usifanyike hadi Reforms zifanyike ili uwe uchaguzi wa HAKI NA HURU ni kosa?
Sasa ona masahibu wanayopitia. Viongozi wao wanatekwa,kuuawa, kushambuliwa, sasa hivi wanazuiwa kusafiri, chama kinyimwa ruzuku, chama kimewekewa zuio haramu kufanya kazi, na kubwa kuliko yote Kiongozi mkuu kawekwa gerezani kiuonevu tuu kwa kesi mbaya sana.
Jee wanastahili hayo yote wakati wanayafanya kikatiba?
Hivi hao washauri wa Farao hawamshauri vizuri kuhusu hili au wao ndio wanachochea ili machafuko yatokee wakimbie wakafaidi rasilimali walizojichotea?
Au haya ni mapenzi ya MUNGU ili litimie analolitaka?
Maana Waisrael walipotaka kuondoka utumwani Misri Farao alikataa na kuongeza mapigo. Na demand ilipoongezeka Mungu naye akaufanya moyo wa Farao uwe mgumu ili aje ajidhihirishe na historia ije iandikwe!
Jee Farao wetu anaenda kuandika historia mpya baada ya moyo wake kufanywa mgumu?
Yezabel ameshipaza shingo, ila hatatoboa!! Lazima shingo ivunjike!
 
Faraoh hakua binadam wa kawaida .
Tulishaambiwa na wanazuoni wakubwa wa kidini kuwa kuna watu wanaoa majini na kuzaa nayo watoto

Kwa hiyo bila shaka kabisa tunaishi au kutawaliwa au kuongozwa na Watu wenye vinasaba vya kijini . Hao sio watu wa kawaida na huo sio mpango wa Mungu kwa Mwanadamu.
Huo ni uzao wa Nyoka kama alivyokua Kaini .
Uzao wa Nyika unatawala kwa damu na haumthamini binadamu zaidi ya mali ,madaraka na kusujudiwa .

Ndio maana Mungu alimleta Yesu ambaye hakuzaliwa kwa mbegu za baba na mama bali kwa neno la Mungu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili aje kwa ajili ya kuwashinda na kuangusha tawala za majini duniani ili binadamu aishi kwa haki na kwa amani .

Tumuombe sana Mungu ili ufalme wake uje na yale yanayofanyika mbinguni yafanyike na hapa duniani .

Mkonda sio muadilifu kama Gambo .
Mpina sio mtu wa kukosa nafasi ya Kuingia kwenye mchujo .
Biteko sio muadilifu kama Majaliwa .
Lukuvi ni muadilifu sana ila kosa lake hakutaka Zanzibar ipate uhuru kamili maana wataleta ugaidi . Ni kweli mana kule Zanzibar majini ni wengi wanaofugwa na kuolewa na kuzaa watoto.

Lisu hajawahi kuwa Mhalifu. Lisu hakuwahi kuwa Mwana usalama kuwa ameasi au kutoa siri za usalama kama walivyomuua Imrani Kombe . Lisu ni Mwanasiasa . Chadema ni chama cha siasa chenye uvumilivu mkubwa sana . Niliona kijana akiuawa na makada wa CCM wanaoitwa Watendaji kwa Kutuhumiwa tu kuiba komputer.
Hao ndio CCM wanaopewa madaraka kuua binadamu . Bila shaka CCM imejaa majini wengi sana nyonya damu .
Ni kweli kabisa ndugu mwandishi sio Kila binadamu umuonaye ni mwanadamu wengine ni majini kama Hawa watawala wetu.

Mwanzo 6:1–2(Biblia) – Andiko Halisi:

1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi, na wana wa kike walizaliwa kwao,
2 wana wa Mungu waliona ya kuwa binti za wanadamu ni wazuri; wakajitwalia wake wowote waliowachagua.

Mathayo 13:24–26 – Mfano wa Magugu na Ngano

24 Akawaambia mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika shamba lake;
25 lakini watu walipokuwa wamelala, adui yake akaja, akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Basi, ile mbegu ilipochipuka na kuzaa matunda, ndipo magugu yalipoonekana pia.

Majini nayo yanazaa na wanadamu ambao ndio viongozi wetu Hawa yanayopenda kuua na kumwaga damu kumfurahisha baba Yao ibilisi ila jambo njema ni kwamba mipango Yao yote itaaribiwa kwa Damu takatifu ya Yesu.
 
Tutaa dika sana ila reform labda CCM wapende wenyewe, ila sio kwa hizi kelle za chura ambazo hazimzuii Ng'ombe kunywa maji
Reform zinakuja na nilazima wala sio swala ccm kutaka hii ni lazima watake wasitake by the way tupo pazuri sana
 
Ni kweli kabisa ndugu mwandishi sio Kila binadamu umuonaye ni mwanadamu wengine ni majini kama Hawa watawala wetu.

Mwanzo 6:1–2(Biblia) – Andiko Halisi:


2 wana wa Mungu waliona ya kuwa binti za wanadamu ni wazuri; wakajitwalia wake wowote waliowachagua.

Mathayo 13:24–26 – Mfano wa Magugu na Ngano


25 lakini watu walipokuwa wamelala, adui yake akaja, akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Basi, ile mbegu ilipochipuka na kuzaa matunda, ndipo magugu yalipoonekana pia.

Majini nayo yanazaa na wanadamu ambao ndio viongozi wetu Hawa yanayopenda kuua na kumwaga damu kumfurahisha baba Yao ibilisi ila jambo njema ni kwamba mipango Yao yote itaaribiwa kwa Damu takatifu ya Yesu.
Mkuu andiko lako hili limetulia. Na linataka tafakari ya kina sana.
Ningetamani sana wale wana CCM wafia chama walisome huku wakiweka ushabiki pembeni ndio watajua huwa wanashabikia maviumbe ya ajabu. Wajichunge, wanaweza kuwa wanajipendekeza pengine hata kwa mapopo Bawa wakaishia kulambwa!
 
Back
Top Bottom