Haya yote aliyofeli Rais Magufuli ni madogo sana, mradi wa Stiglers Gorge ndiyo utakuwa tsunami kwenye kushindwa!

Haya yote aliyofeli Rais Magufuli ni madogo sana, mradi wa Stiglers Gorge ndiyo utakuwa tsunami kwenye kushindwa!

Tatizo la huyu jamaa sio mbunifu, yeye ile miradi ambayo wenzake waliona ni hasara kwa taifa ndiyoo anajitutumua nayo ili aonekane kuwa Tanzania hii hajawahi kutokea na hatakaa atokee kama yeye. Mfano tu ni huo wa stieglers gorge na kuhamia dodoma
 
Amefeli kwenye nini kwa mfano?

Maana stiegler gorge tokea ianze kutekelezwa miezi sita haijafika na mradi wa miaka mitatu,utasema umefeli au unaombea afeli?

Na akifeli wewe utafaidika na nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Jitahidi uwe unasoma mada na kuielewa kabla ya kukimbilia kutoa mapovu. Mbona mada inaeleweka hata kwa std 4 wa st. kayumba
 
yaani umeandika kiumbea balaa, unapenda sana kuona jpm akifeli. kwanza ulicho andika ni kama vile hata wewe huna uhakika kama atafeli, jpm ndo rais wetu hadi 2025
 
JPM amebakiza miaka 7 ya kutawala Tz.
Muhimu jitahidini thread za JPM ziwe fupifupi maana miaka 7 ni mingi mnaweza pumzi ikakata

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi bakiwa na miaka 7; kwani 2020 anaondoka ; na Mimi ndie nitakayemuondoa kupitia ccm pale chimwaga mjini dodoma.

Hakuna mwana ccm atakayesimama kuchukua form but mimi nitasimama na nitamtoa nje ya ulingo.

Muda utaongea; subiri uone maajabu.
 
Uzushi mtupu .mnaombea mabaya wakati mazuri yanakuja
Hakuna mazuri; huyu bana amevuruga sana uchumi wa nchi na uchumi wa wananchi hivyo hata sisi wana ccm hatumtaki sema wengi wetu ni waoga na tunatetea matumbo yetu endapo tukimpinga unajua hasira/visasi vya huyu jamaaa.
 
Sijui ilianza sukari, uhakiki, kodi za hovyo, makinikia, mbaazi, korosho, ndege vyote hivyo Rais wetu anashindwa vibaya sana na hii ni kutokana na one man show.

Ngoja niwapeni kuhusu mbaazi. Aliyekuwa msambazaji mkuu wa zao hilo kule kwa wahindi alikuwa Yusuph Manji. Serikali ikampiga stop kisha waziri wa kilimo akaenda huko kudai kuwa sasa atakayekuwa msambazaji mkuu wa mbaazi kwao ni serikali ya Tanzania badala ya Yusuph Manji. Akajibiwa kama ni hivyo basi hata hizo mbaazi zenu hatuzitaki tena. Soko likaenda shimoni.

Kaenda kwenye makinikia kisha sasa wanatoa kinyemela kupeleka Japan kusafisha. Matokeo yake mategemeo yao yamekuwa sifuri na imekuja hasara ya kufa mtu.

Rais Magufuli amefeli kila jambo. Sasa kuna mradi mmoja huko nyanda za juu wa umeme unaojulikana kama Stiglers Gorge. Huu mradi kwanza huo umeme tunaoambiwa kuwa tutapata hautofikia hata nusu yake. Mradi ukikamilika pamoja na kutumia fedha nyingi sana za ndani (maana nje tumenyimwa) utaenda kuwa msiba kwa mazingira, hasara ya mradi husika na hatimaye utatuletea umeme wa kusuasua. Tusubiri tuone! Wapi amewahi kufanikiwa? Mbona wenzake wote hawakuthubutu kuugusa? Si ulikuwepo? Haya tuone ila hajawahi kufanikiwa.

Ngoja niishie hapo maana mtu unaweza kula kifungo cha maisha jela kutokana na uhochezi na hakimu akapewa "promosheni" mchana peupeeee! Mambo ni vululu vululu ukiugusa utawala na dola ni kifungo cha kufa mtu.
Amefanikiwa kulipa mishahara kwa watumishi kwa wakati muafaka.
 
Ule usemi aliokuwa anapenda kuusema "Tuna hela" naona umepungua sasa hv, nadhani akili imeanza kumkaa sawa!!!!
Na itamkaa sawa pale atakapoona 2020 watu wamemgeuka pale chimwaga ukumbini ili hali yeye ni mwenyekiti wa chama chetu.

I swear ; in 2020 ndani ya chama nitasimama kuchukua form ya kumpinga huyu jamaaa ili mimi ndo nipeperushe bendera.

I will rule only for 5 years ili niipitishe nchi katika kipindi cha mpito 2025 namwachia mwingine wakati huo kila kitu nimekirekebisha
 
Zidumu fikra za mwenyekiti wa chama
Mwisho ni 2020; nitakuwa mgombea mpinzani wa huyu jiwe ndani ya chama. Japo najua upo chama kile but so long as najua misimamo yako nitakukumbuka katika ufalme hapo magogoni.....hahahaha

It sounds like a joke but we have to wait, muda utakuwa hakimu mzuri
 
Mwisho ni 2020; nitakuwa mgombea mpinzani wa huyu jiwe ndani ya chama. Japo najua upo chama kile but so long as najua misimamo yako nitakukumbuka katika ufalme hapo magogoni.....hahahaha

It sounds like a joke but we have to wait, muda utakuwa hakimu mzuri
Hata kupika chai na kukuletea ofisini, mradi jina langu liko kwenye payroll niachane na kupika chapati.
 
Back
Top Bottom