Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu napenda niwaambie kuwa Tanzania itajengwa na sisi wenyewe watanzania, Hatuna mtu atakuja kutujengea nchi yetu, Katika kufikia ndoto ya Tanzania tuitakayo na kuwa Kama ulaya Ni lazima tufahamu kuwa Kuna kipindi Cha mpito.
Lazima tupitie maumivu Kama walivyo pitia mataifa ya ulaya .walitozana Sana kodi, Tozo na ushuru kufikia hapo walipo, walijifunga mikanda, walijinyima ndio wakazijenga nchi zao
Hata sisi katika kuijenga nchi yetu hakuna njia fupi ya kutufikisha waliko fika wenzetu kimaendeleo, tusidanganywe na mtu kuwa tutaendelea pasipo kuwajibika kulipia na kugharamia miradi yetu, lazima tuighalamie na kuwa na uchungu wa kuilinda miradi yetu kwa kutambua kuwa tukiharibu tutaijenga wenyewe tena,
Uzuri wa serikali hii imekuwa na uwazi mkubwa katika matumizi yake, kwani hamuvioni vituo vya Afya, zahanati,shule na hata Barabara zilizojengwa kwa tozo na Kodi zetu, mnataka fedha zitoke wapi tusipochangishana mifukoni mwetu, mnataka kila siku tukakope tu, Ni lini tutaijenga wenyewe nchi yetu. hapana
Ni Sasa wakati wa watanzania Kuendelea kuijenga nchi yetu na kusimamia kile tukijengacho kwa mikono yetu
Hatuwezi tukawajazia madeni ya kulipa kizazi kijacho badala ya kukipa nafasi ya kujenga nacho maisha na mstakabari wake, lazima tujitwishe mzigo wetu wenyewe, Tumuunge mkono mh Rais katika kuijenga nchi hii, Tuwe wa kwanza kuilinda miradi yetu kwa uchungu.
Tuwawajibishe tutakao ona wanapalamia pesa zetu tunazotaka kujengea nchi yetu
Rais wetu anauchungu mkubwa na nchi hii na Tuendelee kumwamini, penye kurekebisha atarekebisha na panapohitaji kuangalia upya Sheria iliyosainiwa atafanya hivyo, Mh Rais wetu Ni msikivu Sana na Mwenye huruma Sana ,hivyo nchi ipo mikono salama, Kama una ushauri wa chanzo kingine zaidi Cha mapato wewe toa na ujumbe utafika kwa mh Rais na ataupokea na kufanyia kazi Kama unafaa maana mh Rais Ni msikivu sana