Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Kuna mambo ambayo binadamu sisi wasahaulifu sana. Wale walamba miguu waliojua kumpaka mzee mafuta kwa mgongo wa chupa walijawa unafki na hawa ndio waliokua wakimwibia na kumdanganya. Sitaki kulisema hili sana nakazia pia alivyosema Mtani wangu James Ile Millya.
Kama kweli hayati Rais Magufuli aliweza kupambana na ufisadi haya mabilioni ya bandarini hayakuibwa akiwa mzima? Haya mabilioni ambayo inasemekana kuna tatizo BoT si ndio wasimamizi ni wale wale aliowaweka yeye? Waliiba vipi wakati wao ndio waliokua wakiimba kua mzee anapambana na mafisadi na waliompinga pia mafisadi?
Mabilioni yaliyochotwa bandarini na tetesi zilizopo BOT inakosemekana kuna shida huko, huu ni mwanzo tu. Vipi kuhusu pesa zinazotolewa kujenga SGR na STIGLERS kule? Vipi mamlaka ziingine kama TANAPA na TRA hawaibi kweli?
Nilichogundua huenda awamu hii ufisadi ulikua mkubwa kuliko awamu zilizopita na ilikua ngumu watu kujulikana maana walilala kwenye kumsifia mzee ili asiwastukie. TAKUKURU wachape kazi hii nchi bado inapigwa sana na Rais wetu Mama Samia asimame imara.