Hayati Dkt. Magufuli alishindwa kupambana na ufisadi, alikuwa mkali tu

Huwezi kupambana na ufisadi kwa one man show, kuudhubiti ufisadi ni suala la kimfumo zaidi.
Kwenye uongozi wa kiafrika ukishaleta mambo ya kujuana ushkaji basi


Ova
 
jaman anko alijitahidii kwa upande wake hivyo inapaswa tumpe sifa kwa hilo
 
Chadema Ninyi hamna jema lolote Nyie mmelifanyia nini taifa hili? Mliapata ridhaa ya kuongoza Majiji mlifanya nini?

Kipindi cha jakaya mliponda hivi hivi tena mkasema Anatakiwa Rais Mkali Adhibiti wizi rushwa na Ufisadi kaja Magufuli Mnageuza tena nakuanza kuponda.

Mwingine Mchungaji msigwa kwenye Msiba kalamba Matapishi Yake zitto kabwe naye kalamba matapishi yake.


Wacheni unafiki wenu. Kila kitu mnajifanya mnajua mkipewa nchi hata robo ya Laliyofanya Magufuli Hamtaweza kufanya. Kama mmeshindwa hata kujenga Ofc za chama mtaweza kuongoza nchi? Nchi sio kijiwe cha kahawa.
 
Kuna wajinga huko TBC utawakuta wanamsifia.

Karudisha nidhamu kazini.

Mtu mwenye nidhamu anaweza kuficha hadi milion mia4 ndani!

Hovyo kabisa.
mil 400 za wapi tena mkuu? Mbona wanakula sn kodi zetu hawa
 
Alishindwa au alikuwa sehemu ya ufisadi? Kama ndege kanunua bila idhini yabunge, SGR, Stiglers, nk una semaje hakuwa sehemu ya ufisadi?

Ukiona kiongozi ana zuia uhuru wa habari, huyo ni ukoma. JPM alikuwa namna hiyo. Mungu amuweke anapi stahili.
Chato International Airport?
 
Alishindwa au alikuwa sehemu ya ufisadi? Kama ndege kanunua bila idhini yabunge, SGR, Stiglers, nk una semaje hakuwa sehemu ya ufisadi?

Ukiona kiongozi ana zuia uhuru wa habari, huyo ni ukoma. JPM alikuwa namna hiyo. Mungu amuweke anapi stahili.
Of course alikuwa fisadi naye. Hakuna mwana CCM msafi, hata iweje
 
Umerudi tena. Keshakufa huyo anza na walio hai
 
Ngoja nikuulize swali kwa maksudi mazima; na usikurupuke kunijibu, kwa sababu ni swali fikirishi.

Ni kipi bora (hili neno "bora", sikupata mbadala mzuri katika kueleza hali hii):

Kumpiga risasi Lissu takribani 32, kwa lengo la kutaka kumuua, au kumpiga risasi na kumuua fisadi/mwizi aliyetambuliwa kitaratibu kuwa ni fisadi/mwizi?
 
Tumuache Hayati JPM apumzike kwa amani katuachia kila kitu kaenda mwenyewe, maana hata hajapiga chafya.

Koo ile mahakama ya mafisadi kazi yake ilikuwa ya akina nani?
Alikuwa anawatafuta wapinzani tu ndio awashitaki huko
 
Kwangu mimi magufuli alikuwa siyo fisadi na pia alikuwa hapendi ufisadi. Ila alikuwa na udhaifu ambao wengi waliutumia kujinufaisha. Magufuli alikuwa hapendi mawazo mbadala. Alikuwa anapenda watu wa ''ndiyo baba'' na watu wa kumsifia. Matokeo yake ''wajanja'' walitumia hii loophole kupewa uteuzi ili wapige. Hii ni cha mtoto. Mtu kama Makonda, Kigwangala, na wote waliokuwa wanasifia kama wanamsifu Mungu wamepiga fedha ndefu sana. Kingine alikuwa hatengenezi system bali alikuwa anafanya one man show. Tanzania ni kubwa hangeweza kudhibiti kila mtu yeye peke yake. Na mabaya zaidi aliua upinzani ambao ndiyo ungeweza kusema vitu kama hivi.
 
TANROAD SYNDICATE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…