Hayati Dkt. Magufuli alishindwa kupambana na ufisadi, alikuwa mkali tu

Richmond, APTL sijui,MKURABITA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtu mmoja aliamua aweke mabilioni ndani Kama sehemu ya mavuno yake ya wavuja jasho, Hapo no mzunguko wa pesa mtaani mabilioni yamepotea alafu anazidi kukamua watu kitaa hii ni hatari kwa Taifa
 
Wewee wacha porojo zako. Bandarini zimeibwa au hazijaibwa? Madege yenu hayajalitia taifa hasara?

Wapumbavu wachache ninyi mnaoliibia taifa mkimdanganya Rais na kumsifia. Mmemaliza pesa za umma mnadanganya Watanzania
 

Mkuu maana hasa ya ufisadi ni kwenda kinyume cha maadili, taratibu, kanuni, na sheria ili kutimiza maslahi binafsi.

Kwa mfano, kujichotea fedha bila kufuata mipango iliyoidhinishwa na Bunge na kukiuka taratibu za manunuzi ili utekeleze miradi kama kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwako, kununua ndege kwa cash, nk. Halafu kuzuia ukaguzi usifanyike wala habari za utekelezaji zisiyolewe ndio ufisadi wenyewe huo.
 
Hapana. Ni mapema Sana kusema Kuna ufisadi.

Auditor siku zote huwa anaandika tu upotevu pale asipopata documents kwa wakati.

Nenda taratibu kutoa tuhuma ambazo hata wewe mwenyewe unamashaka nazo.

Subiri uchunguzi kwanza.
 

Mbwa Mkali na asiyeng'ata hana Faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…