Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Mwambieni Gwajima amfufuwe, yeye si Askofu wa Ufufuo na uzima?

Tumechoka makelele yenu, Dikteta is died and buried. Fullstop.
Hayo ni yako hayako kwenye mada yangu. Mwenyekelel ni weye unaeropoka bila kujua mada yahusu nini!
 
Tunataka tu iwe fundisho kwa viongozi wetu kwamba wao sio miungu na ipo siku watu watakuwa huru kuongea. Ukijua maovu ya bwana huyu hutamuonea huruma yoyote, aliharibu mno, hayo lazima tuyazungumze akiwa hai au mfu.
Kuongea na maiti au marehemu, ni fundisho gani! Kila mtu atakufa ufanye yaliyo mema au maovu. Kikubwa hukumu hutoa Mungu!
 
Sentensi ipi imeokotezwa mkuu? Wewe ulikuwa unamjibu mtu kuwa Mungu ndo hupanga kifo. Unajichanganya sana kwa maelezo yako.

Huyo shetani bora alivyokufa, kila mtu alifurahi including me. Sijali nitakufaje but atleast nimeshuhudia kafa, yeye hatashuhudia nikifa.
Narudia soma mada nzima uelewe usiokoteze sentensi na kukalia kuongelea hiyo sentensi muda wote. Be wide and think wider! Kama yey ni shetani basi shetani uhujuana kwani hakuna mwanadamu alie muona shetani! Na marehemu utukane yeye hakusikii wala hana haja ya kifo chako. Kikubwa ni Hukumu ambayo hutolewa na Mungu! Si hukumu ya mwanadamu.
 
"Takeni sana kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna atayemuona baba asipokuwa nao" mkuu koleza kwa wino mweusi huo mstari wa kwanza, amani na watu wote. Ilmradi hukuthubutu kufungua mdomo wakati haya yanatendeka acha historia iwe mwalimu.
Mwenye hukumu ni Mungu pekee na si mwanadamu.
 
Tulisema sana humu wewe ulikuwa wapi! Hakuna kitu kibaya kama mahaba ni kama rushwa ambayo tabia yake kubwa ni kupofusha macho.
Siongelei mahaba hapa naongelea mwenye uwezo wa kuhukumu ni Mungu pekee. Hiyo misemo yenu ya mahaba wala kwangu haina maana na wala haina athari kwangu. Watu manapenda kukariri. Nakupeni ukweli sibabahiki na vijisemo vyeno unadhani vitaninyamazisha. Hukumu utolewa na Mungu!
Sina tabia ya kujipendekeza, bali usema ukweli! Na mtu hata mahakani akifa kesi au jalada ufungwa. Kama ulisema ilikuwa kwa muda huo sasa kesha ondoka hata akusikii.
Usihukumu ukaja hukumiwa!
 
Si ndio sasa akatenda kwa wakati muafaka.
Mungu ufikiria tofauti na binadamu! Mungu si mwanadamu mpaka apangiwe! Lililo la Mungu si la mwanadamu! Tusijiweke sawa nae, na kuongea kauli kuona Mungu ni wakawaida tu!
 
Narudia soma mada nzima uelewe usiokoteze sentensi na kukalia kuongelea hiyo sentensi muda wote. Be wide and think wider! Kama yey ni shetani basi shetani uhujuana kwani hakuna mwanadamu alie muona shetani! Na marehemu utukane yeye hakusikii wala hana haja ya kifo chako. Kikubwa ni Hukumu ambayo hutolewa na Mungu! Si hukumu ya mwanadamu.
Hiyo sentensi moja tu imetosha kujua jinsi hujui kitu. Umekomaa nisome mada nzima, unauhakika sijasoma? Sasa ngoja nikuoneshe vile huelewi
 
Hiyo sentensi moja tu imetosha kujua jinsi hujui kitu. Umekomaa nisome mada nzima, unauhakika sijasoma? Sasa ngoja nikuoneshe vile huelewi
Unajiona unajua, wendawazimu ni kufanya jambo kwa staili ilele na kurudia yaleyale na kujiona unaakili! Kuna msemo usemao, baharini avumae ni papa lakini....! So usijione much know nakuleta lugha za dharau. Mtu mwelevu hata sikumoja ajisifii bali usifiwa!
Kuja na lugha za kujifanya unajua huo ni ulimbukeni na ushamba! jenga hoja acha kujifanya unadharau! Unajitutumua weee! pole sana!
 
Kifo ni tukio la kiasili. Katika imani kadhaa za kidini zina elezea kifo kilitokea baada ya Adamu na Hawa (Eva) kwenda kinyume na mapenzi ya muumba wao (MUNGU). Ndipo Mungu alitamka kuwa tutakufa, au kurejea katika mavumbi.

Binadamu wa kwanza kufa alikuwa Abeli. Ambaye aliuliwa na kakaye aitwae Kaini. Kaini japo alimuuwa Abeli, bado Mungu alimlinda Kaini na hata akasema atakae muuwa kaini basi atalaaniwa. Hivyo Mungu alimpeleka Kaini nchi ya mbali. Hii yote kumuepusha na kumlinda na mabaya. Mungu alifanya haya yote japo Kaini alikuwa na dhambi ya kumuuwa nduguye.

Mungu utazama tofauti, na macho ya binadamu. Na Mungu ndiye mwenye uweza wa kuhukumu. Siku hizi Tanzania hii kumezuka, tabia ambayo inaonesha watu kufurahia kifo au vifo vya watu wengine. Na kama walikuwa hawampendi huyo mtu au watu; ndo watazusha mengi. Wabaya wake watajifanya wao ni mungu (Mungu), watahukumu, watasema huyu alifanya mabaya ndo maana kafa.

Watajiona wao waliobaki ndo wajanja, hawana makosa au dhambi mbele ya Mungu. Najiuliza hivi kuna mahala popote pale iwe katika misaafu au maandiko yoyote ya kidini na imani zinginezo, pana sema mtu anae kufa mapema au kabla ya wenzie ana dhambi na Mungu kaamua kumkomoa?

Nachojua Mungu alisema tutakufa, hakuna atakaeishi milele hapa duniani. Ndo maana watu ufa wakiwa watoto wachanga, wakiwa vijana, wakiwa wazee, na hata watoto wengine ufia tumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa.

Tukidai kufa mapema ni kukomolewa na Mungu, ebu tuangalie, hawa mitume wetu, walikufa bado wakiwa vijana, na walikuwa na maadui wengi, hawakupendwa. Yesu kristo aliishi miaka isiyozidi thelathini na tatu. Na alianza kazi ya kuhubiri akiwa na miaka thelathini tu. Vile vile kwa mtume Muhamad S.W.A alikufa mapema. Si hao tu ni wengi!

Hivyo kifo ni asili. Nachoamini kila mtu anakusudi la kuwepo duniani. Na pia ana muda wake wa kuishi. Haijalishi ni miaka mingapi. Muda ukifika Mungu ndo mwamuzi wa yote, uondoke au aseme bado ubaki.

Katika kila jambo Mungu anamakusudi yake. Laweza kuwa baya au zuri, lakini Mungu anatazama tofauti na tunavyotazama sisi wanadamu.

Kikubwa tusijipe kazi ya Mungu ikawa kazi yetu. Tusijipe kuhukumu kwani hukumu ya maisha yetu utolewa na Mungu. Usihukumu usije hukumiwa.

Nimeongea haya yote ni kutokana na watu wengi, wapinzani na wana CCM kuonekana kumhukumu alie kuwa Rais wa Tanzania, J.P. Magufuli na hata kumzodoa kuwa kafa mapema, yako wapi, kuonesha tu Mungu ati kamuondoa kwa mabaya yake. Nilishangaa hata Mchungaji mmoja anajiita mzee wa upako kuongea kama vile nae anaonesha kufa kwa magufuli ni kama adhabu, eti kisa Lowasa hakuchaguliwa Urais na kuwataka watu wakamuombe Msamaha Lowasa.

Mimi niseme kwa maandiko viongozi wote wakuu wa nchi uwekwa na Mungu. Mungu angeamua Lowasa kuwa Rais angekuwa tu. Mchungaji kasahau maandiko anatumia akili za kibinadamu. Kufa kwa Magufuli si kwamba Mungu hakutaka Magufuli awe Rais, la asha. Mungu hutenda kwa wakati wake.

Jiulize katika maandiko tunaambiwa kuwa Yusufu aliuzwa utumwani na nduguze, bado huyo Yusufu akafungwa gerezani. Lakini cha ajabu akaja kuwa ndiye waziri mkuu wa nchi. Hata nduguze walipojihisi atalipiza kisasi kwa kuwafanyia mabaya, aliwaambia. Mlikusudia mabaya kwangu, lakini katika hayo mabaya Mungu alikusudia mema ili nije niwaokoe katika baa la njaa.

Mungu uona mbali zaid ya binadamu. hatujui ni kwanini Mungu aliepusha Lowasa asiwe Rais japo ilitumika njia mbaya au nzuri, lakini Mungu anakuwa na makusudi yake. Mchungaji katafakari neno la Mungu ndo utoe tamko. Hakuna lifanyikalo duniani bila Mungu kuridhia. Mungu huyo aliruhusu Ayubu apate mateso, akaruhusu watoto wake Ayubu kufa na hata mali kuharibika na kupotea lakini alikuwa na kusudi. Kifo cha Magufuli kinakusudi liwe baya au zuri ila watanzania tutajifunza kutokana na hicho kifo siku moja. Kikubwa tusijichukulie mamlaka ya kuhukumu na kusema kafa kwa sababu alikuwa katiri na kadharika. Mbona Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji?

Hivi kazi yetu ni kuhukumu, kwani tuliobaki hatutakufa? wangapi tumefiwa na ndugu na wazazi, je kutangulia kwao ni kwamba walitenda mabaya Mungu kawahukumu? Kwa uzoefu wa haraka tu mara nyingi watu wema hawadumu? Iwapo hadi sasa unaishi lazima ujiulize, unatakiwa kulifanyia nini Taifa lako la Tanzania, na familia yako. Si kushambulia marehemu, na kujifanya wewe ni mungu unahukumu. Leo hata viongozi wetu utasikia, oooh! Magufuli hakutenda haki, alikuwa kiongozi mbaya, alikuwa muuwaji, alitisha, hakuwa na demokrasia!

Hivi ninyi viongozi mnao sema haya si mlikuwa nae ktk uongozi wa serikali? Kwanini amkumwambia wakati huo akiwa hai kuwa ni kiongozi mbaya.

Nacho jua Magufuli alikubali kukosolewa. Naibu Waziri wa afya kipindi hicho alimkosoa kuhusu matumizi ya kujifukiza. Akamwondoa katika nafasi. Lakini baadae alimrejesha ktk wizara tofauti.

Leo wanao mkosoa magufuli haohao, wanapinga Mhe. Rais Samia kukosolewa. Wakati Rais alidai kuwepo uhuru wa kukosoa. Lakini chama chake na Bunge Wanataka asikosolewe, tumsifie hata kwa yale yasio sifiwa. Wakati wanadai wao ni wanademokrasia. Ukikosoa unahesabika msaliti, Bunge litakuita kwenye Kamati. Chama kitakaa kukuita kikuhoji kwa nini huko kinyume na Rais. Chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambae ni Rais alie ruhusu kokosolewa.

Mungu hapendi wafitini na watu waongo, wenye roho za usaliti. Viongozi mjitafakari. Na msijione ninyi hamta kufa. Kifo kipo akijali madaraka yako. Hakuna atakae ishi milele. Kuwepo kwako pengine Mungu anataka utimize mambo fulani. Ghazabu ya Mungu ni kubwa tusihukumu tukaja hukumiwa. Magufuli kaondoka kamaliza yake. Alifanya kwa nafasi yake na kwa staili yake. Watu wote hatufanani.

Tusijione sisi ni bora kwakuwa tu watu wanatuchekea na kutusifia. Tukachekelea na kuota kiburi kuona tuko sahihi na hatukosei! Pamoja na yote Magufuli aliwapenda watanzania. Hakuwahi kusema waondoke wakaishi Burundi.

Leo kauli hiyo inaongewa na kiongozi aliepewa dhamana na watanzania. Viongozi wamejiona wako juu ya sheria, wanauwezo wa kusema chochote. Viongozi wamekuwa na dharau. Wanajiona nchi ni yao. Hata wananchi kulalamika hawaoni haja ya kuomba msamaha.

Hata kiongozi wa nchi hawakanyi anawaacha je naye kafurahishwa na hayo maneno? Je kawatuma?
Harafu hawa hawa ndo wanasema watakuwa wapole na kuwabembeleza wananchi kuliko JPM ambaye kapewa mabaya yote.
Tukumbuke kutangulia kufa si dhambi. Na ukibakia si ujanja wa kufanya kutukana waliotangulia. Bali chukua muda wa kujitafakari.

Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji wa nduguye. Mungu ndiye mwenye kuhukumu. Na ndiye ajuaye mwisho wa maisha yetu. Jiulize hapo ulipo matendo uyafanyao ktk vificho au wazi, je ni mema? Je wewe ni msafi zaidi ya waliotangulia kufa?

Je, wajua kifo chako kitakuwaje? Lini utakufa? Je utakufa ukiwa na umri gani? Je alie kutangulia kafa akiwa na miaka mingapi?
Si ujanja wala umaarufu kutukana marehemu, au kutafuta umaarufu ati unajilinganisha na marehemu. Huyo kesha maliza wakati wake hayupo tena. Tuache kashfa hatujui kesho yetu. Tanzania ya leo imekuwa na siasa za kujipendekeza, sifa za kijinga, badala ya kufikiria maendeleo ya kweli. Walio tangulia tuwaache, tujenge nchi.
Mkuu maisha ya Yesu hayahusiani na upuuzi wa magufuli na hata vifo havifanani. Yesu yupo hai kama wewe ni mmuumini wa dini ya kikristo. Kusema aliishi miaka 33 sijui nini unamaanisha.

Pia, nakusihi, usifananishe maisha na kifo cha MTUME MUHAMAD na takataka.
Wewe simamia hukumu ya huyo marehemu.

Pia usijidandanye viongozi wote wa nchi huwekwa na Mungu. Umetumia maandiko gani? Acha kupotosha watu ukidhani maandiko hatuyajui.

Unaandika mambo ya imani unachanganya na siasa, ndio ulitaka nisome huu upupu
 
Wewe nadhani hujui uttheolojia, Maisha ya Yesu duniani yalikuwa miaka mingapi, na alianza kazi ya mahubiri yake akiwa na miaka mingapi! Usilinganishe Thelojia na kuwa nyumbani ukasoma Biblia.
Unaposema Yesu yupo hai kwa maana ipi? Tofautisha kuishi kwa Yesu duniani akiwa kama mwanadamu, na uishi wa kiroho ambao uwezi ongea. Na uelewe sijamfananisha Yesu na Mtume Muhamad S.W.A ila nimeongelea kuwa walikufa wakiwa na umri mdogo bado vijana. Huku si kufananisha.
Naona akili yako ipo kutafuta vijisababu. Narudi kwenye Mada. Kufa mapema si tatizo, Siri ya kifo aijue Mungu. Na hukumu hutoa Mungu si Mwandamu.
Usihukumu ukaja kuhukumiwa!
 
Mkuu wewe ni mkristo? Tuanzie hapo. Unajua kwanini yesu alikuja duniani? Unajua kwanini aliishi maisha dunian kama binadamu wa kawaida? Unajua lengo la yeye kukubali kufa? Je alijua kuwa atakufa au hata kufa?

Nimejaribu kuyasema hayo ili nikuoneshe kuwa kuna vitu hujui. Huyo magu kuna mtu kamchoma moto au kumpeleka peponi? Nani kamhukumu?
Mseme hapa kuwa flani baada ya jiwe kufa, sasa roho yake umeipeleka kuzimu.

Furaha siyo hukumu, huyo kafa duniani tunafurahi. Mungu naye atatoa hukumu yake kulingana na matendo ya marehemu wakati wa maisha yake.

Huelewi mkuu, unaweka mifano ya MITUME then unakanusha tena. Unasema Mungu hupanga kifo baadae unakanusha.
 
Mkuu wewe ni mkristo? Tuanzie hapo. Unajua kwanini yesu alikuja duniani? Unajua kwanini aliishi maisha dunian kama binadamu wa kawaida? Unajua lengo la yeye kukubali kufa? Je alijua kuwa atakufa au hata kufa?

Nimejaribu kuyasema hayo ili nikuoneshe kuwa kuna vitu hujui. Huyo magu kuna mtu kamchoma moto au kumpeleka peponi? Nani kamhukumu?
Mseme hapa kuwa flani baada ya jiwe kufa, sasa roho yake umeipeleka kuzimu.

Furaha siyo hukumu, huyo kafa duniani tunafurahi. Mungu naye atatoa hukumu yake kulingana na matendo ya marehemu wakati wa maisha yake.
Hukumu utolewa na Mungu, Ole wake anaehukumu nae atahukumiwa! Over!
 
Wewe nadhani hujui uttheolojia, Maisha ya Yesu duniani yalikuwa miaka mingapi, na alianza kazi ya mahubiri yake akiwa na miaka mingapi! Usilinganishe Thelojia na kuwa nyumbani ukasoma Biblia.
Unaposema Yesu yupo hai kwa maana ipi? Tofautisha kuishi kwa Yesu duniani akiwa kama mwanadamu, na uishi wa kiroho ambao uwezi ongea. Na uelewe sijamfananisha Yesu na Mtume Muhamad S.W.A ila nimeongelea kuwa walikufa wakiwa na umri mdogo bado vijana. Huku si kufananisha.
Naona akili yako ipo kutafuta vijisababu. Narudi kwenye Mada. Kufa mapema si tatizo, Siri ya kifo aijue Mungu. Na hukumu hutoa Mungu si Mwandamu.
Usihukumu ukaja kuhukumiwa!
Unawezaje kumfananisha Yesu na shetani?

Kama unawafananisha mwambieni na yeye afufuke sasa kama Yesu kisha apae mbinguni kwenda kuwafagiloa malaika.
 
Watumushi wa umma hatutomsahau maisha yetu yote...[emoji124][emoji124]
 
Back
Top Bottom