Hayati Dkt. Magufuli ndiye Rais aliyefaa kuiongoza Tanzania

Hayati Dkt. Magufuli ndiye Rais aliyefaa kuiongoza Tanzania

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Habari wanaJamiiForums

Natumaini ni wazima wa afya binafsi nilikuwa naumwa Sana angalau sasa hiv nina unafuu nilikuwa nina Malaria tuombeane nipone kabisa.Tuje kwenye mada husika hapo juu unajua nimekuwa mfuatiaji kiasi fulani wa jukwaa Hili nimegundua kuwa members wa jukwaa hili hawana tofauti na ushabiki wa Simba na Yanga au Teams zile ambazo zipo mitandaoni sijui Team diamond,Team kiba n.k tunachukulia siasa kama ushabiki badala ya kuchukulia kama maisha.

Kupitia siasa nchi ndio inajengwa watu wamekuwa wakiabudu viongozi as if ni Mungu wakiwasapoti hata kama wanakuosea hapo unajiuliza hawa wanatofauti ipi na Team diamond au Team kiba? Wanaushabiki wa vyama as if hivyo vyama vinawasaidia kuondoa umasikini wa maisha yao wamefanywa mandondocha na wanajiona ok yaani Unaweza kukuta mshabiki wa Chadema anamshambulia shabiki wa CCM analipwa kutetea ujinga lakini na yeye mwenyewe anafanya kile kile anachofanya mwenzake.

Nije kwenye lengo kuu la uzi wangu kiukweli kutokana na hii nchi ilivyo mtu kama Magufuli ndio mtu pekee ambaye alituonesha uelekeo mzuri wa kutupeleka mbali. Hii nchi kuna baadhi ya mnatatizo yanazalishwa na watu kwa lengo lakupiga pesa na kama hakuna strong President ambaye ni mzuri kwenye ufuatiliaji kupigwa kuzidi kutaendelea, Mfano mzuri tangu aingie Magufuli madarakani hakujawi kuwa na shida ya maji kama ilivyo sasa hiv huku kwetu Kimara hii inaenda siku ya 5 maji hayatoki Waziri husika uko alipo anafanya Nini wanawanchi wanateseka jitu limekaa linakula kiyoyozi watu wa aina hii wakitumbuliwa baadhi ya watu especially wenye itikadi ya vyama wanasema Magufuli ana roho mbaya wakati hata yanatokea Mama samia anazurura nchi za nje.

Umeme sasa umekuwa unatikatika tofauti na kipindi Cha Magufuli kama unakumbukumbu vizuri Magufuli kama ajaingia madarakani wakati wa kampeni aliwapiga beat Tanesco na kweli tangu aingie ukusikia hata ile kasumba ya maji ya kidatu yamepungua.

Magufuli kakuta nchi ambayo nchi jirani zinachukua rasimali zetu ovyo ovyo Mara unasikia twigs kapandishwa ndege n.k lakini mwamba tangu aingie kuna wachina wameukumiwa vifungo virefu, mambo ya kutoroshwa mali asili kazibiti.

Kiufupi hii nchi Magufuli aliichukua likiwa imeoza na ndio maana akawa anajenga misingi we jiulize mtu kafariki muda mrefu still anapokea mshahara ndio maana akaanzisha kampeni ya kushafisha mafanyakazi hewa.

Kuna miradi Mingi hapo awali inachukua muda mrefu kukamilika ingawa haikustahili ifike huko ni kwasababu viongozi wetu hawakuwa wasimamizi tofauti na Magufuli ndio maana umeona chini yake flyover imekamilika kwa wakati madaraja mengi yamekamilika kwa wakati kwasababu hakiona mkandarasi haendi sambamba na kasi ya mradi anamfukuza hii imesaidia sana.

NB: Tanzania ina muhitaji mtu kama Magufuli ili ipige maendeleo tofauti na hapo nchi itakuwa unarudi nyuma kwa mambo mengi sana.
 
Kwenye suala la strong institution ya urais ambayo itazuia mambo ya kijinga na kuchezeana kama ulivyosema kwenye suala la umeme nakubaliana nawe, lakini inapozidi mpaka kugharimu maisha ya watu (wapinzani) hapo sikubalini nawe, inshort Magufuli alikuwa na mazuri yake na mabaya yake.
 
Tunaenda pata magufuli mpya 2025. Wajibu wa mama nikutufikisha 2025 tuweze mpata magufuli mpya. Wapo wachumia tumbo utawasikia 'mama hadi 2030' wakati mama mwenyewe kashasema viatu vya magufuli havimtoshi. Mama ni mzalendo analijua hili. Wajibu wa wazalendo wote ni kumkinga mama na vibaraka wa ubeberu na kuhakikisha anazungukwa na watu wazalendo wenye weledi.
 
Calibre ya ukali na kutobembelezana ndio itayotutoa hapa na kutufanya tusonge mbele kwa haraka!

Tatizo wabongo wanapenda kubembelezwa ukiwa kauzu wanakuchukia😂! Hao ndio wanaonufaika na TZ ya sasa ya chief Hangaya! Wadokoe hela wasiguswe wafanye kazi kwa kujiskilizia hivi na hela wapate kwa wakati!
 
Calibre ya ukali na kutobembelezana ndio itayotutoa hapa na kutufanya tusonge mbele kwa haraka!

Tatizo wabongo wanapenda kubembelezwa ukiwa kauzu wanakuchukia[emoji23]! Hao ndio wanaonufaika na TZ ya sasa ya chief Hangaya! Wadokoe hela wasiguswe wafanye kazi kwa kujiskilizia hivi na hela wapate kwa wakati!
Wabongo wanapenda dezo dezo
 
Weak mind

Rais ndo asisafiri kuzuia umeme usikatike Ki mara?

Rais hata maji Kimara nayo kazi ya Rais?

Nchi inahitaji watu wafatiliaji sio walalamikaji

Ulienda kuuliza why maji now yanakatika?

Why umeme?

Kufatilia kila kitu ndo kumemuua

Kajipa stress za nchi nzima hadi afya ikazorota...nchi haijengwi na Rais
Unamuona JK bado ana afya? Why? Ku take things easy

Kama Watanzania kwa upumbavu wetu hatujali kabisa huduma za jamii Hadi Rais afatilie basi Bora asifatilie

Hata kujenga masoko nayo Rais aseme?

Halmashauri iko wapi? Madiwani?
 
Acha Wenge,Mbona hausemi siku hizi watu wasiojulikana hawapo?

Enzi za Magu umeme ulikuwa unakatika tu labda wewe ulikuwa unakaa line ya ikulu.

Jengo la Taneco alibomoa ili iweje? Mbona hausemi alikuwa na Roho Mbaya?
Hii nchi inahitaji kiongozi mwenye rohombaya, kuna uzembe mkubwa sana wamakusudi unafanywa na baadhi ya viongozi kwenye secta zao.

Wewe mwenyewe apo kama zinachaji lazima unamkubali hayati kimyakimya.

Jengo limebobolewa sababu lilikuwa katika aneo la hifazi ya barabara full stop.

Vipi, sasaivi unaonaje kimara maili moja watu wanavyo jiachia katika njia 8.
 
kiukweli kutokana na hii nchi ilivyo mtu kama Magufuli ndio mtu pekee ambaye alituonesha uelekeo mzuri wa kutupeleka mbali.Hii nchi kuna baadhi ya mnatatizo yanazalishwa na watu kwa lengo lakupiga pesa na kama hakuna strong President ambaye ni mzuri kwenye ufuatiliaji kupigwa kuzidi kutaendelea,
Enyi Muabudio maiti, ni nani aliewaroga,
DAWA NI KATIBA MPYA,
kwa nini mnajitia uwendawazimu msiokuwa nao.
Magufuli ni maiti , kafa fafafa, kaoza.
 
Hii nchi inahitaji kiongozi mwenye rohombaya, kuna uzembe mkubwa sana wamakusudi unafanywa na baadhi ya viongozi kwenye secta zao.

Wewe mwenyewe apo kama zinachaji lazima unamkubali hayati kimyakimya.
Jengo limebobolewa sababu lilikuwa katika aneo la hifazi ya barabara full stop.
Vipi, sasaivi unaonaje kimara maili moja watu wanavyo jiachia katika njia 8.

Sukuma GANG mlivyo wanafiki , hamsemi kabisa maauji na utekaji wa Magufuli kwa watanzania.
 
Back
Top Bottom