Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Kwa sababu mwenye ashafariki mengi mtaandika
 
Chanzo cha pesa za Lowassa zilikuwa ni nini?
Alianza kidogo kidogo akiwa CCM mikoani.aliposhinda ubunge 1990 na kuwa ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa alizipiga kweli,akiwa ardhi ndio balaa kajimilikisha ardhi na viwanja vingi sana prime areas,kaingia mikataba ya kimagumashi sana,aliwahi kumtapeli hadi john malecele mgawo wa rushwa,malecela skiwa bosi wake,jamaa slikuwa fisadi kweli sio uongo
 
Chuki zako hazisaidii kitu
 
Nyerere nae mnamtukuza sana,kwa hio Nyerere akikataa kitu ndio wote tukione hakifai,ni binadamu yule wkt mwingine na yeye alikua ana interest na mtu flani kwa maslahi yake,tusimuone Mtakatifu sana,nae alikua mjanja mjanja tu
 
SaLim alizid kuwa muungwana
Hakuwa na timu ya wahuni,siasa za siku hizi bila wahuni basi tegemea bahati tu
Sahihi Salim Ahmed Salim alikuwa muungwana mno kiti Cha Uraisi angepata Bila shida Wahuni kamati za fitna na majungu za Zanzibar ndizo zilihakikisha hapati

Tungepata Raisi Mzuri sana Salim Ahmed Salim angepata uraisi
 
Ni vema kuweka records Sawa.
1995 majina matatu yalipelekwa mkutano mkuu.
Wagombea walikuwa
Cleopa Msuya (Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais)
Benjamin Mkapa (Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia)
Jakaya Kikwete (Waziri wa Fedha)

JK aliongoza kwa kura akifuatiwa na BWM na Msuya akawa wa 3.
Katiba ya CCM ilitaka mshindi awe na zaidi ya 51%, kitu ambacho JK hakufikisha.

Ni uongo kuonesha JK alionewa.

Ndio maana aliposhinda kwa wingi wa kura 2005 kwa kuwabwaga SAS na Mark Mwandosya, alikuja na kauli..."safari hii, kura zimetosha".

Hoja za wazi ni vema zikajengewa hoja kwa uwezi maana kumbukumbu za 1995 tunazo.

Wasalaam!
 
Kwani JK hakuwa mwana mtandao?

Ninapata hisia kuwa JK alimkata EL kwa kukumbuka maelekezo toka Nyerere.

Pili kumbe JK ameanza uharibifu kitambo na amekuwa sugu ikiwa ndiye alipewa;
Maelekezo kuhusu Monduli
Kuhusu Kighoma Malima nk
 
Hatujui kwanini Jakaya baada ya kushinda kwny CCM 1995 iliamriwa kura zipigwe tena na baada ya hapo akaomba fursa azungumze japo vijana wenzie tulitamani agome
Niliona Ile hotuba kupitia TBC baada ya Mkapa kutangazwa mshindi 1995 Kikwete aliongea hotuba Moja mzuri sana. Kiasi Cha kufanya Mwalimu Nyerere asimame kupiga makofi na ukumbi mzima ukamfuta Nyerere kusimama na kupiga makofi. Marehemu Mkapa akakimbia kwenda kumkumbatia Jakaya kwa hisia kali kama mtoto anayenyonya aliyekosa kumuona mama yake siku mbili. Jakaya was matured but at that time Nyerere alikuwa sahihi juu ya kumpa Marehemu Mkapa. Jakaya alihitaji kukua zaidi.
 
JK alimzidi BWM kwenye kura za mwisho ila akatangazwa BWM,maana hakuwa na makundi na aikuwa clean,tulichotangaziwa ni tofauti na yaliyotokea chumba cha kuhesabia kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…