Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Kumbe!!?

Sasa jk kwanini.ana cognitive ability ndogo kihivyo!!?

Kumbe alionywa kabisa asiambatane na edo hakuelewa!!?

Good story!!
 
Taarifa zikamfikia mwalimu Nyerere kuwa kijana Lowassa anagawa pesa kama njugu na amekodi ndege,na akaambiwa anaambatana na mtoto wa rafiki yake marehemu Mrisho Kikwete ,yaani Jakaya .
Mwalimu akamuita Jakaya Msasani ili kumuonya akae mbali na EL,

Uje uweke na stori ya namna Mrisho na Kambarage walivyoingia makubaliano ya kwamba lazima mtoto wa Mrisho aitwaye Jakaya aje kupewa nchi...
 
Huyu Mzee mwenye mvi alikuwa mbaguzi wa wazi dhidi ya watu wa kaskazini
Tumeshazika sasa tunajibu hoja kwa hoja

Walioshadadia Kashfa ya Monduli

1) Freeman Mbowe
2) Godbless Lema
3) Chrstopher Ole sendeka
4) Anne Kilango Malecela

wote hawa wanatokea unapotokea Wewe mbaguzi

au wakati wa Kashfa ya Richmond mlikuwa bado wadogo

Waliotupiwa zigo la Monduli walifanyie kazi walikuwa Home boy ambao leo ndio hao hao wanalalamikia wakwere walivyokuwa akili nusu Mlingoti

hao hao ndio walikuwa wanamtukana Mkwere kuwalinda wana mtandao!
Mwanasiasa Mahiri na madhubuti lazima uwe mtulivu, akili nyingi sana na mvumilivu na sifa zote hizo Adui yenu mkuu anazo

Sifa kubwa sana ambayo Mkwere na Mzee wa Monduli pamoja na kutofautiana walikuwa nayo ni kutopenda kulalamika lalamika

ukim snitch anaku snitch na wakikutana kila mmoja anajibu am fine

Walimzunguka Bosi kwny Richmond nae akawapelekea moto kwa kutumia hiyo hiyo Richmond

walipotolewa nje ya Game wakaunda magenge mengi sana ya hujuma hadi migomo mikubwa mikubwa akapiga kimya akawasubiri 2015 akala kichwa

Wakahamia upande wa pili wamuoneshe show kwa kuwa wana watu na pesa nae akawaonesha ana akili na dola wakamalizana kibingwa

na wote hawakuwahi kulalamika hadharan

Kitu cha kujivunia Jk alisikiliza kilio cha Wengi cha kulipasua Kundi lake la Wanamtandao

2017 alimtumia Mzee wa Kundi Samwel Sitta kumpumzisha Ngoyai na 2010 akatumia nguvu na ushawishi wa Ngoyai kupitia NEC kuweka vipengele cha Jinsia kumpumzisha Uspika Mzee Sitta

2011 akamtumia aliekuwa Mwanamtandao wa Mzee Sumaye Ndugu Nape akampa Ukatibu wa Itikadi akaanza ku deal na mapacha watatu na Tajiri wa Igunga akavua jezi

na 2015 akakamilisha madaraka yake kwa kuhakikisha Wanamtandao hawapo tena kama kundi


Pamoja na tofauti zote na rafu zote za Siasa hakuwa na muda kuhujumu uchumi au biashara ya Mtu japo alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo

alijua Michezo ya Siasa itaishia kwny Siasa sio kutafutana kwenye Bank Accounts na Assets za mtu
 
JK bado ni mwanasiasa nguli Africa ni dhairi kuna mchezo ulichezwa kumpoka kura na hakuwa na nyongo ,angereact angechafua hali ya hewa
 
Ulikuwepo ndugu ama umesimuliwa, ama umehisia?
 
Kwa hiyo tuseme toka moyoni jk chaguo lake ama mbadala wake alikua Jpm?
 
Kwani JK hakuwa mwana mtandao?

Ninapata hisia kuwa JK alimkata EL kwa kukumbuka maelekezo toka Nyerere.

Pili kumbe JK ameanza uharibifu kitambo na amekuwa sugu ikiwa ndiye alipewa;
Maelekezo kuhusu Monduli
Kuhusu Kighoma Malima nk
Jk ni Mwanasiasa, Mwanajeshi, mwana …………,.

moja ya Sifa yake kubwa sana ni kuwa na Marafiki wa dhati kwny kambi pinzani na hilo lilimsaidia, linamsaidia na litamsaidia sana Inshallah na uzuri wa hilo mkimalizana kwny Siasa kamalizana na Wewe na ukibaki na kinyongo kimpango wako
Kawapa sana mashavu maadui zake wa Kisiasa akijua kabisa hawamkubali
 
Huyu mzee amebeba mengi moyoni mwake, tokea ile 95 na harakati zote hadi leo hii na hatma ya uongozi wetu wakati huu tulio nao
 
Wee jamaaa unajua sana, salute 🫡
 
Kwani JK hakuwa mwana mtandao?

Ninapata hisia kuwa JK alimkata EL kwa kukumbuka maelekezo toka Nyerere.

Pili kumbe JK ameanza uharibifu kitambo na amekuwa sugu ikiwa ndiye alipewa;
Maelekezo kuhusu Monduli
Kuhusu Kighoma Malima nk
Ni kweli alimshughulikia Kighoma Malima barabara

Ufisadi fisadi wa kwanza mkubwa alikuwa waziri alikuwa Kighoma Malima mtu wa swala Tano ila fisadi hatari na sigda yake usoni na swala Tano akiwa waziri wa Fedha mikashfa kibao ya kifisadi

Raisi Mwinyi akaona atafute mtu serious kweli akampa Kikwete uwaziri wa fedha na akamtoa Kighoma Malima na akampa Kikwete , Kikwete alimshughulikia barabara bila kujali ni mtu wa Pwani mwenzie au Muislamu mwenzie account zake nje alikoficha pesa Kighoma Malima alisafiri hija kumbe anaenda kutaka kukimbia nchi akatoe pesa kule kaweka nje akaenda hija na nyumba ndogo bi mdogo kisha akaenda huko ulaya atoe pesa wale maisha ulaya huko akakuta Kikwete waziri wa fedha kazipiga pin Akaunti Zote hakuna pesa ya kutoa

Akapata presha akafa wakarudisha kuzika Tanzania Kwa hasira familia yake waliogoma hawakutaka Serikali ihusike Hadi Mwanawe mkuu wa mkoa Sasa hivi alitorokea upinzani

Kikwete ndio alikuwa waziri wa kwanza Enzi hizo kupambana na fisadi mkubwa Malima aliyekuwa waziri wa fedha Kabla yake

Kwa Hilo apewe hongera na maua yake
 
Nyerere nae mnamtukuza sana,kwa hio Nyerere akikataa kitu ndio wote tukione hakifai,ni binadamu yule wkt mwingine na yeye alikua ana interest na mtu flani kwa maslahi yake,tusimuone Mtakatifu sana,nae alikua mjanja mjanja tu
Huo ujanja ujanja ndio ulimfanya kuogopwa na kila mtu kule chamani hata baada ya kustaafu,idadi ni kubwa,Malechela,Kolimba,Seif Sharif Hamad,EL,JK ni waathirika wa ujanjaujanja wake.
 
Hizi porojo zako baki nazo huko kijiweni kwenu
 
Ulivyomtaja Makonda nimeacha kuendelea kusoma upuuzi mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…