Hayati Lowassa alivyomponza Kikwete akatimuliwa Msasani kwa kufokewa na Mwalimu Nyerere

Maelezo sahihi haya! Shukran.
 
Najua hauna kumbukumbu za idadi halisi ya kura alizopata kila mgombea zaidi ya kutajiwa fulani kapata asilimia fulani na hujawahi kujiuliza kwa nini?
 
Kwa hiyo tuseme toka moyoni jk chaguo lake ama mbadala wake alikua Jpm?
Rejea hotuba za Magufuli

nakukumbusha tu

alisema hadharani hakuwa na Mpango wa kuchukua fomu ila alienda Ikulu kumshtaki Saada Mkuya kwa kutompa pesa za kulipa wakandarasi 900 billion , Jk akamuuliza Wewe huchukui fomu ?akamuuliza ninatosha ? akamjibu Wewe kachukue kutosha au kutotosha tutajua Sisi

Hapo maana yake Rais alikuwa na Plan Kadhaa kutokana na yatakayojiri

waki react hivi itakuwa hivi na jinsi walivyo react wakaamua kadri walivyoamua na iliyobaki ni historia

Sina uhakika ila ninaamini

Jakaya, Mkapa, Mangula na Kinana walikaa kama kamati kuamua nani awe nani kwa kutumia report na ushauri wa Mamlaka za kiuchunguzi na pale Dodoma walienda kutekeleza tu maamuzi maana hata Mgombea mwenza Samia anatuambia Kamati kuu walikuwa wanakula biscuit wakati vingunge wanakamilisha taratibu kupitia chumba maalum
 
Najua hauna kumbukumbu za idadi halisi ya kura alizopata kila mgombea zaidi ya kutajiwa fulani kapata asilimia fulani na hujawahi kujiuliza kwa nini?
Kama wewe unazo kumbukumbu, weka hapa, ili kuni-prove wrong.

Ila kumbukumbu ya kuwa JK hakuzidi 51% ziko wazi kwa 1995 kama ambavyo alivyowazidi Mwandosya na SAS kwenye duru ya kwanza ziko wazi.

Uwezo wa BWM kwa aliyofanya, yana-prove, alikuwa na Rais mwenye merits.
 
Siyo JK alihusika hapo. Ni UK na kuna sababu za ugomvi kati ya UK na Kighoma.
 
Kando ya Kambarage. Mkwere ni nguli wa siasa za Tanzania watoto wadogo hawawezi kulielewa hili.
 
Sasa kama ni hivyo mbona walikuja kuhitilafiana kiasi kile, mbaya, kwa nini yule hakuonyesha shukurani aliye kutangulia kwa vile alipita kwa nasibu kiasi hiko.
 
Jakaya Kikwete alikuwa pale CCM Singida na baadaye huko Mtwara ndipo alipofanyiwa lobbying kwa Mzee Mwinyi na swahiba wake hayati Ukiwaona Ditopile Mzuzuri ndipo alipoteuliwa na Mzee Mwinyi kuwa Naibu Waziri !!

Hii maneno ya kuwa alikuwa karibu sana na Mwalimu sijawahi kusikia hii kitu kabisaaa !! πŸ˜…πŸ™πŸ™
 
Kuweka rekodi sawa hata Mama Samia akipofuatwa na Kikwete kuwa awe mgombea mwenza wa Raisi Magufuli alikataa hakuwa na mpango Kabisa Hadi alilia kukataa
Akaambiwa tunakupa taarifa tu safari mgombea mwenza CCM tunataka wanawake mumeshakomaa kiongozi Wewe umeshakuwa Hadi Spika bunge la katiba tunakutaarifu tu Wewe ndie utakuwa mgombea mwenza ukikwama utasaidiwa Chama, Serikali wasaidizi wako wa kutosha akajaribu kusema aka sitaki akasikia tu mgombea mwenza safari hii Mwanamke Kwa mara ya kwanza Toka Tanzania ipate uhuru makofi yakarindima kuwa tunakubali mengine Historia mama Samia huyo anachapa kazi halali
 
Ilikuwaje kwenye uongozi wake akakumbwa na kashfa za ufisadi mkubwa?
Escrow, Richmond, umeme wa Tegeta ile 300B?
 
Umemwaga nondo ile balaaaaaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…