Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Vyanzo vya maji kwa ajili ya Mabwawa makubwa matatu ya kuzalishia umeme, yaani Bwawa la Mtera, Kidatu, na Kihanzi, vyote kwa asilimia tisini (90%) vinategemena na sehemu kubwa vinatokana na vyanzo vile vile. Kwa mfano sehemu kubwa ya maji yanayojaza bwawa la Mtera na Kidatu chanzo chake ni kile kile.
Kwa miaka miwili mfululizo kumekuwa na ukame mkubwa sana kwenye maeneo yanayotoa maji kwa ajili ya mabwawa ya Mtera na Kidatu. Wiki hii nilikuwa Mtera na kwa kweli hali ni mbaya sana kiasi kwamba inawezekana upungufu wa maji mtera umeweka historia kwa miaka ya hivi karibuni.
Sasa kama sehemu kubwa ya umeme wetu tunategemea umeme unaozalishwa kwa maji, na ukame ndiyo huu umeshika kasi, tunategemea muujuzi gani utakaotuzalishia umeme?
Enzi za Magufuli kulikuwa hakuna mgao mkubwa wa umeme, lakini jee pia kulikuwa kuna ukame kama ulioko sasa? Mara hii tumeshasahau ni kwa nini Enzi za Kikwete wafugaji walihamishwa toka hifadhi ya bonde oevu Ihefu?