Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Huu ulikuwa uwezo wa kipekee sana Sijapata kuona ! Inafahamika kwamba Viongozi karibu wote wa ccm wanatengeneza Makundi, lakini Mara zote viongozi hao hutengeneza makundi ya kampeni, yaani wanatengeneza wapambe wa kufanya kampeni, kwamba angalau pamoja na kuiba kura, angalau viongozi wa ccm waliopita waliunda hata timu ya kushawishi wananchi ili wawachague.
Dr Magufuli aliunda kikundi cha hiyari cha "kumuabudu" nasema cha hiyari maana sikuwahi kuona watu wakilazimishwa kujiunga nacho, hiki kikundi hakikuwa cha Kampeni, maana Magufuli hakuwahi kuamini katika demokrasia, hili kundi lilikuwa kama zile Praise team za makanisa, ni kulinda imani kufa na kupona, kwamba chochote atakachokifanya hata kama kilikuwa hatari kwa nchi, kama kuvunja kienyeji mikataba na wawekezaji wa kimataifa, jambo ambalo ni hatari lakini kikundi hiki kilishangilia kufa na kupona.
Kilikuwepo hata kikundi cha kutukana Wazee, wastaafu na Wanasiasa wa vyama vyote ikiwemo CCM, hakuna yoyote aliyepingana na Magufuli hata kwenye mambo ya msingi ambaye hakushambuliwa na kikundi hiki, mmemsahau Musiba na yale Magazeti yake yaliyodaiwa kuchapishwa na Usalama wa Taifa?
Inasemekana Magufuli alipenda sana kusifiwa, kwahiyo jamii inatambua wako waliokuwa wanamsifia na kujikuta wakiingizwa kwenye praise team na kuteuliwa.
Sasa mshangao wangu ni huu, Mtu huyu ambaye hakuwa na ushawishi wowote Majukwaani aliwezaje kutengeneza kikundi cha kumuabudu na kumtii mithili ya Machifu wa enzi za Ujima?