Bellagio
Member
- Feb 12, 2022
- 52
- 75
Huu ulikuwa uwezo wa kipekee sana Sijapata kuona ! Inafahamika kwamba Viongozi karibu wote wa ccm wanatengeneza Makundi , lakini Mara zote viongozi hao hutengeneza makundi ya kampeni , yaani wanatengeneza wapambe wa kufanya kampeni , kwamba angalau pamoja na kuiba kura , angalau viongozi wa ccm waliopita waliunda hata timu ya kushawishi wananchi ili wawachague .
Dr Magufuli aliunda kikundi cha hiyari cha "kumuabudu" nasema cha hiyari maana sikuwahi kuona watu wakilazimishwa kujiunga nacho , hiki kikundi hakikuwa cha Kampeni , maana Magufuli hakuwahi kuamini katika demokrasia , hili kundi lilikuwa kama zile Praise team za makanisa , ni kulinda imani kufa na kupona , kwamba chochote atakachokifanya hata kama kilikuwa hatari kwa nchi , kama kuvunja kienyeji mikataba na wawekezaji wa kimataifa , jambo ambalo ni hatari lakini kikundi hiki kilishangilia kufa na kupona .
Kilikuwepo hata kikundi cha kutukana Wazee , wastaafu na Wanasiasa wa vyama vyote ikiwemo ccm , hakuna yoyote aliyepingana na Magufuli hata kwenye mambo ya msingi ambaye hakushambuliwa na kikundi hiki , mmemsahau Musiba na yale Magazeti yake yaliyodaiwa kuchapishwa na Usalama wa Taifa ?
Inasemekana Magufuli alipenda sana kusifiwa , kwahiyo jamii inatambua wako waliokuwa wanamsifia na kujikuta wakiingizwa kwenye praise team na kuteuliwa .
Sasa mshangao wangu ni huu , Mtu huyu ambaye hakuwa na ushawishi wowote Majukwaani aliwezaje kutengeneza kikundi cha kumuabudu na kumtii mithili ya Machifu wa enzi za Ujima ?
ivi unajielewa ulicho andika [emoji2955][emoji2955]