Hayati Magufuli alifanikiwa kutengeneza kundi lililomuamini na kumtii mithili ya wafia Dini

Hayati Magufuli alifanikiwa kutengeneza kundi lililomuamini na kumtii mithili ya wafia Dini

Kitambulisho cha Mjasiriamali
Unaweza kutuambia hela zile zilienda wapi ?

2082683_FB_IMG_1559946076802.jpg
 
Mfumuko wa bidhaa za vyakula,vitambulisho vya machinga 20000/= KWA mwaka ni bora kuliko sasa!!

Wanamgambo KWA mama ntilie hawakuwepo kuwasumbua!

Elimu bure pia iliwasaidia!

Ongezea na mengineyo!

Alikataa lockdown ambayo ingeua watu zaidi hasa maskini wangekufa njaa Baadae Dunia nzima ikaona lockdown ni uzembe tu wa kufikiria HADI leo haipo na coronavirus bado ipo na Maisha yanasonga!!

Ongezea nyama hapo!!!
Rwanda waliweka lock down wangapi walikufa ?
 
Kwenye inshu ya kuteuwa mtu yeyote kutoka upinzan au mtaani hii mbinu nayo alifanya ashangiliwe na kila mjinga mwenye njaa akiamini siku yoyote anaweza teuliwa

Kingine alichofanikiwa ni kuhakikisha vyombo vyote vya habari vinatangaza na kusifia maujinga yake,huwez amini mpaka bbc na sahara media waliufyata maana bbc akizingua sahara inabeba mzigo wa makosa
 
Alikuwa na karama tofauti na wewe ery au mbowe. Ndio maana tulikusanywa kumuabudu.

Na wewe ukifanya mambo makubwa tutakusanywa kukuabudu.
Mimi sitaki laana ya Mungu
 
Haya alishakufa miaka 2 sasa ilitosha kusifiwa akiwa hai. Mtu akifa na bado akaishi mioyoni mwetu hakika hakulazimisha kupendwa ila alipendwa kwelikweli. Tanzania watu waliowahi kupendwa wa kwanza ni magufuli akifuatiwa na nyerere
Kwani nimebisha basi ! Walaaa !!
 
Mimi siyo mwanasiasa,Ila ukweli Ni kwamba hata mbowe ni mungu wenu pale chadema.

Na ameisimika vema ideology yake maarufu ya "Mimi ndiye chadema na chadema ndiyo mimi. Nitakufa nikiwa mwenyekiti,Mimi ndiyo mbowe".

Hiyo ni ibada kamili, vinginevyo neno ibada umelipa maana yako ya kujitungia,tofauti na uhalisia wake.

Toeni kwanza hilo boriti kabla hamjamtaja Magufuli kila saa.

Siasa zenu bongo mmeweka unafiki mbele.
Acha uongo
 
Unasema hakuwa na ushawishi?!

Kwa taarifa tu hakuna kiongozi aliyekuwa anafutaliwa kama Magufuli akiwa anaongea

Mwenye radio alihakikisha mawimbi hayayumbi asikie kinachojiri

Naweza kusema ukimtoa nyerere ndiyo kiongozi pekee alieyekuwa na hotuba za kugusa wananchi

Kosa kubwa alilofanya ni kuwatetea ngozi nyeusi angejali masilahi yake na biashara zake hadi leo huenda anagekuwepo!

Afrika ukiwa rais ukasimamia haki ni ngumu kudumu!
Unazisikia tena hotuba zake TBC ? yaani kusema kwamba " nitapiga hadi shangazi zako" ndio hotuba za kugusa wananchi hizo ?
 
Unasema hakuwa na ushawishi?!

Kwa taarifa tu hakuna kiongozi aliyekuwa anafutaliwa kama Magufuli akiwa anaongea

Mwenye radio alihakikisha mawimbi hayayumbi asikie kinachojiri

Naweza kusema ukimtoa nyerere ndiyo kiongozi pekee alieyekuwa na hotuba za kugusa wananchi

Kosa kubwa alilofanya ni kuwatetea ngozi nyeusi angejali masilahi yake na biashara zake hadi leo huenda anagekuwepo!

Afrika ukiwa rais ukasimamia haki ni ngumu kudumu!
haki ya kupoteza watu ni haki hiyo ?
 
Hatukukusanywa,
Maana hata mtoa mada amekiri kwamba JPM hakuwa na ushawishi, Sasa kukusanywa hiyo ilitoka wapi?
Elewa tu ilitoka mioyoni.
Wengi wetu tunashawishiwa kwa matendo zaidi kuliko maneno.
Je, wewe washawishiwa kwa maneno?
Utaingia Chaka sana,
Kama ni ke utatiwa mimba Hadi tano pasipo kupata mme wa kukuoa..
kama ni ME ?
 
fb_img_1652379712226-jpg.2574374

Kati ya hizi picha mbili ni ipi inayotoa taswira ya wafia dini? Nani anayefoka mithili ya Wainjilisti ?Muwe wakweli.....btw picha zote kwa hisani ya CHADEMA Ufipa Digital Propaganda studio
jamiiforums1267461471_387x387-jpg.2572374
Moja ya kampeni za wazi hadharani , nyingine ya kupanga mipango isiyojulikana gizani
 
Hata Mbowe licha ya kupata ziro form six , kuuwa chama kutoka wabunge 100 hadi 1, kushindwa kujenga ofisi ya chama lakini bado kuna kikundi kikiongozwa na Erythrocyte kina amini Mbowe ni bonge la kiongozi na ataivusha nchi kiuchumi wakati hata uchumi wa kujenga ofisi nzuri y chadema umemshinda kwa miaka 30 aliyoongoza chama.
Miaka 30 umeitoa wapi ? liongo liikubwa weee !!
 
Jamaa hawawezi kupitisha wiki bila kutaja Mwamba.
R. I. P my president.
 
Nchi ilizizima Kwa furaha alipokufa watu mabaa yalifunguliwa upyaaaaa na yaliyobakiza wanywaji wawili kufumba na kufumbua kukawa na wateja kama wote Arusha mbeya dar acha kabisa Arusha ngombe na mbuzi walichakaa!
Acha uongo, huoni hata aibu!
 
haki ya kupoteza watu ni haki hiyo ?
Hakuna utawala ambao haujawahi kuua, kuteka wala kupoteza watu kwa africa

Katiba zetu mbovu ndiyo zinawafanya watawala wafanye wanavyotaka

Kwani Dr mwamboka alitekwa kwenye utawala wa Magufuli? Na Mawazo aliuwawa kwenye utawala wa Magufuli?!
 
Back
Top Bottom