Hayati Magufuli alifanikiwa kutengeneza kundi lililomuamini na kumtii mithili ya wafia Dini

Kuna mambo yanafurahisha sana kwenye siasa!!

Hivi unaanzaje kumsema Mwamba yule kuwa hakuwa na ushawishi wowote majukwaani!?

Labda nikusaidie tu. Kuelekea uchaguzi wa 2025 tutajua kama Magufuli hakuwa na ushawishi wowote kwa Watanzania kama unavyotaka kutuaminisha hapa. labda ungesema Magufuli hakuwa mwanasiasa mzuri bali alikuwa Rais anayejituma, kufanya kazi kwa bidii na aliipenda nchi yake. Huenda alikuwa na madhaifu yake lakini yule mzee tuacheni unafiki alikuwa anapiga kazi. Na hadi vizazi na vizazi atabaki kwenye historia.

Sasa nyie mnaojiita wana demokrasia shangilieni sasa kwani sasahv hakuna rushwa, maisha ya wananchi yamekuwa mazuri, demokrasia imeleta watalii nchini, kodi na tozo hakuna tena, umeme na maji vinapatikana kwa wingi, deni la taifa limepungua na pia demokrasia imeimarisha uwajibikaji kwa mawaziri na watumishi wa serikali. Sasa hivi ukienda maofisini watu wanachapa kazi.

Ama kweli demokrasia imefungua nchi. Ripoti ya CAG inafanyiwa kazi kwani demokrasia imesababisha wala Rushwa wachukuliwe hatua za haraka. Machinga wanafanya biashara kwa uhuru. Nani kama Wapinzani walioleta maridhiano?

Magufuli kwakweli aende zake in Peace!
Umemaliza kila kitu Mkuu !! Kongole 🙏🙏
 
Marekani Ina watu wengi wazuri wa kuongoza sio lazima yule hayawani
Wamarekani wapiga kura wanamtaka Trump arudi kushika usukani !! Hao waliopo kwa sasa wanaweza kusababisha vita kuu vya tatu ambayo ndivyo vitakavyokuwa vita vya mwisho kupiganwa duniani !! Trump alishasema America first “. Hawezi kupoteza pesa za walipa kodi wa 🇺🇸 USA kupiganisha vita visivyokuwa vinawahusu !!
 
Kitu Chadema na CCM hadi sasa mmeshindwa kufanya. Hii nchi watu pekee walioweza kushawishi watu hivyo hadi siku yao ya mwisho dunia ni Nyerere na Magufuli tu wengine wamefeli. Hamna cha Mbowe, JK, Sa100 na waswahili wengine mnao wapenda lakini bahati mbaya wanavutia vikundi vichache.
Mtu amekufa lakini hadi sasa anakunyima usingizi wakati Rais aliyeopo madarakani anavurunda kuliko kawaida. Anyway mpo wired hivyo.
mbona Hittler anajadiliwa hadi leo ?
 
Huu ulikuwa uwezo wa kipekee sana Sijapata kuona ! Inafahamika kwamba Viongozi karibu wote wa ccm wanatengeneza Makundi, lakini Mara zote viongozi hao hutengeneza makundi ya kampeni, yaani wanatengeneza wapambe wa kufanya kampeni, kwamba angalau pamoja na kuiba kura, angalau viongozi wa ccm waliopita waliunda hata timu ya kushawishi wananchi ili wawachague.

Dr Magufuli aliunda kikundi cha hiyari cha "kumuabudu" nasema cha hiyari maana sikuwahi kuona watu wakilazimishwa kujiunga nacho, hiki kikundi hakikuwa cha Kampeni, maana Magufuli hakuwahi kuamini katika demokrasia, hili kundi lilikuwa kama zile Praise team za makanisa, ni kulinda imani kufa na kupona, kwamba chochote atakachokifanya hata kama kilikuwa hatari kwa nchi, kama kuvunja kienyeji mikataba na wawekezaji wa kimataifa, jambo ambalo ni hatari lakini kikundi hiki kilishangilia kufa na kupona.

Kilikuwepo hata kikundi cha kutukana Wazee, wastaafu na Wanasiasa wa vyama vyote ikiwemo CCM, hakuna yoyote aliyepingana na Magufuli hata kwenye mambo ya msingi ambaye hakushambuliwa na kikundi hiki, mmemsahau Musiba na yale Magazeti yake yaliyodaiwa kuchapishwa na Usalama wa Taifa?

Inasemekana Magufuli alipenda sana kusifiwa, kwahiyo jamii inatambua wako waliokuwa wanamsifia na kujikuta wakiingizwa kwenye praise team na kuteuliwa.

Sasa mshangao wangu ni huu, Mtu huyu ambaye hakuwa na ushawishi wowote Majukwaani aliwezaje kutengeneza kikundi cha kumuabudu na kumtii mithili ya Machifu wa enzi za Ujima?

Siasa ni imani
Dini ni imani

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI CCM
 
mbona Hittler anajadiliwa hadi leo ?
Hivi wewe unafikiria kabla hujajibu? Hitler? Kwenye International stand kati ya viongozi makatili Magufuli hayupo. Ruto na Uhuru wali orchestrate mauaji 2007 hadi wakaenda The Hague lakini hamna mtu anawaita makatili sembuse Magu ambaye hana hata body count yoyote chini ya jina lake. Acheni kuishi kwa ubabaishaji. Kwa hoja zenu hizo mlitakiwa mseme BM alitoa order watu wapigwe risasi huko Zanzibar na Mwembe Chai. Hii issue za kutekwa na kupotea hadi leo zinaendelea kwahiyo Sa100 na yeye ni muuaji? Watu siyo wajinga.
 
Wamarekani wapiga kura wanamtaka Trump arudi kushika usukani !! Hao waliopo kwa sasa wanaweza kusababisha vita kuu vya tatu ambayo ndivyo vitakavyokuwa vita vya mwisho kupiganwa duniani !! Trump alishasema America first “. Hawezi kupoteza pesa za walipa kodi wa [emoji631] USA kupiganisha vita visivyokuwa vinawahusu !!
Acha uzwazwa ww usa bado wapo presidential materials wa kutosha hiyo takataka Trump ipambane kwanza na kesi zake za kuhonga wacheza porn.
 
Hivi wewe unafikiria kabla hujajibu? Hitler? Kwenye International stand kati ya viongozi makatili Magufuli hayupo. Ruto na Uhuru wali orchestrate mauaji 2007 hadi wakaenda The Hague lakini hamna mtu anawaita makatili sembuse Magu ambaye hana hata body count yoyote chini ya jina lake. Acheni kuishi kwa ubabaishaji. Kwa hoja zenu hizo mlitakiwa mseme BM alitoa order watu wapigwe risasi huko Zanzibar na Mwembe Chai. Hii issue za kutekwa na kupotea hadi leo zinaendelea kwahiyo Sa100 na yeye ni muuaji? Watu siyo wajinga.
Wewe huna hoja hata moja , pumzika huyawezi haya mambo
 
Mikutano ya Siasa imeruhusiwa, Mbona mimutano yenyew hamfanyi hatuwaoni 😂😂
 
"Strongmen brook no rivals and they're served by faceless men". That goes the old say. Haa waliokuwa wakimtii ni kikundi cha waovu wenzie ili watese watu.
 
Huu ulikuwa uwezo wa kipekee sana Sijapata kuona ! Inafahamika kwamba Viongozi karibu wote wa ccm wanatengeneza Makundi, lakini Mara zote viongozi hao hutengeneza makundi ya kampeni, yaani wanatengeneza wapambe wa kufanya kampeni, kwamba angalau pamoja na kuiba kura, angalau viongozi wa ccm waliopita waliunda hata timu ya kushawishi wananchi ili wawachague.

Dr Magufuli aliunda kikundi cha hiyari cha "kumuabudu" nasema cha hiyari maana sikuwahi kuona watu wakilazimishwa kujiunga nacho, hiki kikundi hakikuwa cha Kampeni, maana Magufuli hakuwahi kuamini katika demokrasia, hili kundi lilikuwa kama zile Praise team za makanisa, ni kulinda imani kufa na kupona, kwamba chochote atakachokifanya hata kama kilikuwa hatari kwa nchi, kama kuvunja kienyeji mikataba na wawekezaji wa kimataifa, jambo ambalo ni hatari lakini kikundi hiki kilishangilia kufa na kupona.

Kilikuwepo hata kikundi cha kutukana Wazee, wastaafu na Wanasiasa wa vyama vyote ikiwemo CCM, hakuna yoyote aliyepingana na Magufuli hata kwenye mambo ya msingi ambaye hakushambuliwa na kikundi hiki, mmemsahau Musiba na yale Magazeti yake yaliyodaiwa kuchapishwa na Usalama wa Taifa?

Inasemekana Magufuli alipenda sana kusifiwa, kwahiyo jamii inatambua wako waliokuwa wanamsifia na kujikuta wakiingizwa kwenye praise team na kuteuliwa.

Sasa mshangao wangu ni huu, Mtu huyu ambaye hakuwa na ushawishi wowote Majukwaani aliwezaje kutengeneza kikundi cha kumuabudu na kumtii mithili ya Machifu wa enzi za Ujima?
Roho ngumu na kusimamia anacho kiamini ili mfanya afanikiwe
 
Ngoja aje johnthebaptist na genge lake!
 
Back
Top Bottom