Hayati Magufuli aliichangamsha Tanzania

Hayati Magufuli aliichangamsha Tanzania

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Kuna watu huku JF ukitaja JPM wanakosa raha na wanafanya kila liwezekanalo ili wazime nyota yake.

Ila sipo uko

Kipindi cha JPM watanzania tulitembea kifua mbele sana.

JPM alifanya Tanzania tujulikane nje ya Tanzania sana kwa wale ambao wanatembea sana katika nchi nyingine watakubaliana na mimi ila kwa wabishi watabisha.

Kuna siku mwalimu wangu wa shule huku Canada alifanya reaction ya video za JPM ndani ya darasa sijui alimuona wapi yeye alikuja ndani ya darasa kabla ya kuanza kufundisha akaweka video ya JPM ile video yake ambayo alikuwa anapiga ngoma.

Halafu akatuhuliza eti amesikia huyu (JPM) ni raisi lakini alikuwa hajui ni wa nchi gani, wanafunzi wenzangu wakajibu na kusema ni Rais wa Tanzania kwao na akina wakataja jina langu.

Nilivimba ndani ya darasa wanafunzi wote wakaanza kusema il est meilleur président africain (yaani ni Rais bora Afrika)

Halafu mwalimu wangu akasema nimependa uchangamfu wake sana

Siyo hivyo tu kipindi cha JPM kila mtu alikuwa anajua Tanzania kwa style yake.

Tulikuwa tukisema nimetoka Tanzania utasikia wanasema kwa Magufuli
Wengine kwa yule Rais aliyekataa kufunga mipaka yake

Kama ninyi ni wafuatiliaji wazuri wa mitandao ya kijamii South Africa kuna comedian fulani hivi alikuwa anahojiwa kwa bahati mbaya alitaja jina la JPM vibaya alitukanwa na watu kwenye comment.

Nakumbuka kuna mtandao mmoja wa Ghana ulipost picha ya JPM halafu wakaandika maneno haya JPM Rais mpendwa zaidi Africa comment zilishuka apo mpaka raha.

Ukuu wa JPM uko nje ya Tanzania.

Sasa hivi nchi imepoa kama ugali wa muhogo, tulikuwa tumeshazoea matukio na vimbwanga vya mwanaume wa shoka.

FB_IMG_1663202208135.jpg

Screenshot_20221019_152608_com.facebook.katana.jpg
 
Kweli kabisa.kwa sasa zile amsha amsha hazisikiki tena.tulizoea kwenye mikutano wananchi wanatoa kero zao zilizoshindikana kutatuliwa wakizisema mbele ya jpm na kutatuliwa hapohapo.Lakini kwa sasa hamna hou utaratibu na kero za wananchi hazitatuliwi .Bora siku ziende haraka ili hii awamu iishe haraka labda tunaweza kupata wa kuichangamsha nchi kama alivyokuwa rais mzalendo magufuli.
 
siyo lazima ukashfu wengine unapomsifu magufuli. mbona sisi tukimsifia mzee wetu rukhsa hatukashfu wengine?....... jifunze ustaarabu
 
Ukiwa mwovu sana, Dunia yote itakufahamu.

Kuna mtu hapa Tanzania ambaye hajawahi kuwasikia PANYAROAD?
Huyu alikuwa mwanaume kweli wa africa. Kila kiongozi wa africa alitamani kuja kuonana nae. Viongozi walikuwa wanamfuata hadi chato.
Nakumbuka Kenyatta alisema nimekuja huku chato ukiwa likizo ili nipate muda mzuri na wewe.
 
Ukiwa mwovu sana, Dunia yote itakufahamu.

Kuna mtu hapa Tanzania ambaye hajawahi kuwasikia PANYAROAD?
Sasa inategemea the way wanavyo kufahamu
 
Damu ya huyu mzee lazima itaondoka na mafala kadhaa. Huwezi kuwadhulumu mamilioni ya watu nje na ndani ya Tanzania rais wao halafu ubaki salama. Iwe kiroho au kimwili.

Auwaye kwa upanga atakufa kwa upanga. Kama aliua kwa upanga naye ameondoka kwa upanga.
 
Kumepoa kwa kweli.
He is gone ila Bado wanamtaja Hadi midomo inakauka.
Na humu JF wanamwandika Hadi vidole vinakuwa kama Tangawizi za Busokelo
 
Back
Top Bottom