Hayati Magufuli alikamata kila mwenye akili ya kuhoji, alitaka kuongoza nchi ya Wajinga tu, Hata hivyo ilishindikana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ikiwa tumeingia mwezi wa 3 , ambao kwa mahesabu ya Tanzania na wanazuoni ni mwezi wa Mungu ( wenye akili wameelewa ) , tutajitahidi kuanzia leo na kuelekea mwisho kuwaletea makala za kusikitisha za uozo wa serikali ya awamu ya 5 na viongozi wake , wakiwemo waliokufa na walio hai , wakiwemo wenye madaraka hadi leo na wale ambao wako Benchi .

Tunachoahidi ni kuhakikisha kwamba kila hoja zetu zitakuwa na ushahidi uliotukuka bila longolongo yoyote , kikubwa twende na kanuni ileile ya kwamba AKUANZAE MMALIZE

Pichani ni Tito Magoti aliyetekwa na kunusurika kuuawa na utawala huo akipelekwa mahakamani, nusura yake ilitokana na makelele ya Watu kutaka apatikane akiwa hai , hii ni baada ya Mashuhuda kuona namna alivyotekwa tangu mapema kabisa , huyu aliponea tundu la sindano



Ombi letu ni hili , kila mwenye ushahidi wa mambo yote machafu ya awamu ya 5 ajitokeze kuuleta , katika makala zetu hizi kabambe za Mwezi huu wa Mungu , HATUTAKUWA NA MSWALIE MTUME .

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO
 
Mbowe ashindwa mahakamani, sasa nyumba yake kufilisiwa baada ya kudhulumu waandishi wa habari.

Lisu alijipiga golori ili kumzuia Magufuli asijenge bwawa la umeme ili mabeberu yake yanayomlea Ubelgiji yaendelee kutuletea generator na umeme wa capacity charges lakini Magufuli hakutishika na sasa bwawa limekamilika na umeme umeingizwa gridi ya taifa.
# tutashitakiwa MIGA.
 
Usisahau kuwaweka CHADEMA kwa kutengeneza mazingira hayo. Ya Kujiteka, na Kujipiga risasi.
 
Wewe ni mjinga kama wajinga wengine.
 
Sasa kwa kanuni za Akuanze mmalize, wapo wengi ambao hawakumalizwa. Wewe endelea kuchochea Uhasama na Visasi na Vinyongo halafu watu wakitumia hiyo kanuniyenu ya CHADEMA ya akuanzae mmalize uone Matokeo
 
Halafu wananchi wakiwakataa kwenye maandamano yenu uchwara mnasingizia mmerogwa. Mnacheza muziki wa Mbowe bila kutafakari. Mwenzenu kahongwa amtukane jiwe mpaka kajenga mjengo huko kijijini. Jpm keshawapoteza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…