Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Moja ya takwa la mtu kuwa kiongozi mzuri ni kufahamu takwimu na kuziheshimu. Kama hili eneo upo mtupu huwezi kuongoza vizuri.
Kwa mfano, Tanzania ni nchi ambayo raia wake wengi hawana umeme. Magufuli alilijua hili. Kwa Africa nchi za kiarabu, karibu asilimia 100 ya wananchi wao wanapata umeme.
Kusini mwa Sahara nchi zinazoongoza ni South Africa kwenye 85 na Ghana 83. Kenya asilimia 70 ya wananchi wao wana umeme. Sasa vipi Tanzania? Asilimia 40 tu ya wananchi ndiyo wana access ya umeme.
Magufuli kama mpenda takwimu alitambua hili. Akaanzisha mpango wa ujenzi wa bwawa la Nyerere. Lakini kikubwa alifanya ni kushusha bei ya kuunganisha umeme. Nafikiri hakuna kipindi watu wengi wameunganishiwa umeme kama kipindi cha Magufuli. Sasa awamu ya sita imetengua hilo, kama vile lilikuwa ni anasa tu.
Mtu hawezi kuwa kiongozi mzuri kama hafahamu wala haheshimu takwimu.