Hayati Magufuli alikuwa kiongozi muovu katika kundi la waovu, na alikuwa kiongozi mwema na mwenye huruma katika kundi la watu wema

Alipokuwa Waziri katika Wizara mbalimbali alikuwa mtiifu na mzalendo.Hata alipochaguliwa kuwa Rais 2015 alionekana mtu wa kuja kuiongoza nchi vizuri sana kuliko waliomtangulia lakini kinyume chake baada ya kumaliza miezi sita ya mwanzo aligeuka kuwa chatu mmeza mbuzi.
 
Rekodi yako wewe inajulikana wazi,wala hujifichi,lkn ukweli unajulikana,magufuli amekufa akiwa mstari wa mbele akiipambania nchi yake,
 
Wanalipwa mkuu,
 
Kama yeye alikuwa mwema kwanini alibagua watu kwa vyama, makabila na ukanda? Leo anasema jambo moja kesho anafanya kitu tofauti! Kwanini alishirikiana na watu kama Sabaya, Makonda, Hapi, TISS, DPP na DCI, mahakama na Polisi kuteka, kunyang'anya pesa na mali za watu na kuua kisha anajifanya mcha Mungu?!
Kubambikia watu kesi kisha pesa za plea bargain anapelekwa kuzificha China?! Wema gani huo?! Si ndio maana Mungu akamuona kazidi na akiendelea kuishi ataumia watu wengi sana, mwisho akatoa kibali akafa kibudu kama kuku wa kideri ili kuokoa raia!
Wema upi kwani angetumia kanuni za kawaida za kisheria na kikatiba asingekuwa Rais?
Mrundi atuhañgaishe hivyo!
 
Kwani wale waliopeleka China kwa hapa wapo kundi gani chief
 
Huyu magufuli unaemsema hapa, ni yule alyesema ukichagua mpinzani sahau maendeleo? Ni yule aliyeagiza nyumba za kimara zibomolewe na za Mwanza ziachwe? Ni yule aliyesema kaskazini wasubiri? Ni yule aliyekuwa rais wakati raia wanapotea, wanaokotwa kwenye viroba, Lissu anapigwa risasi na hakutaka uchunguzi ufanyike? Ni yule aliyefupisha ajira ya CAG professor Assad baada kufukua upotevuwa 1.5t? Ni yule muwongo aliyeokota vichwa vya treni bandarini? Ni yule aliyesema mapapai, mbuzi na oil zimepatikana na corona?
 
Alipokuwa waziri alikuwa kwenye mipaka kimamlaka, hangeweza kutenda uovu alotenda baada ya kuwa rais.
 
Mambo aliyoyafanya jpm kwa Taifa hili yako wazi,kila mtu anayajua na Dunia nzima inayajua, hebu nidhibitishie tuhuma hata moja ya jpm?,uwe na ushahidi usiatia mashaka hata kidogo,
 
Serikali ingekuwa na mpango wa kumuua lissu isingefanya huo upumbavu wa kijinga,
 
Hata Yesu Kristo alipoondoka duniani walisema yule mla rushwa, jambazi, anayekula nacwenye dhambi!

Kwahiyo hii ni tabia yamtu asiyependa haki, lazima apindishe maneno ili aonekane mwema, mnaaibika sana aisee!
 
Ule umati wa Malaika waliokimbia kilomita 9 kumsindikiza Rais Magufuli ipo siku watarudi tena kumtetea itakuwa too late kwa wote wanaomsema vibaya.
 
Na wale watanzania waliomaliza vyuo na kuwafungia ajira watamwonaje, wale ambao alizuia wasipandishwe madaraja yao km sheria inavyotaka miaka yote ile je watamwonaje?
 
Crap
 
Alikuwa mzuri sana kwa wajinga, wasio na upeo, waliopungukiwa akili, uelewa na maarifa.

Marehemu hachukiwi, lakini uongozi wake ulikuwa mbaya sana, ulijaa matamanio lakini uliopungukiwa maarifa.
 
Dah.. Natamani niwe kama Magufuli.

Nikifa kila siku watu waniandike mimi. Miaka miwili sasa jamaa alikufa ila kama anaishi
Amua uwe jambazi haramia kupindukia, unaandikwa mara nyingi na wakati wote.

Wewe unamfahamu aliyekuwa kiongozi mkuu wa Ujerumani kabla na baada ya Hitler. Karibia kila mtu mwenye uelewa kiasi anamfahamu Hitler.

Ukitaka ukumbukwe sana, uandikwe sana, na usemwe sana, uwe jambazi kupindukia.Hitler, Musollin, Stallin, Pinochet, Botha, Amin, Bokasa, Nguema, Mobutu, hawa watakumbukwa daima ndani na nje ya mataifa yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…