Hayati Magufuli aliona mbali kuhusu chanjo, ona sasa huko Ulaya wanavyoanza kupukutika


ni kama kuna jambo linaharakishwa kupitia chanjo mhh
 
Kwaiyo tumetumia chanjo yoyote au mama kaleta chanjo yoyote?

Hayati aliona mbali na alikuwa na maono na ndio maana hadi leo tupo hapa kuhusiana na Corona.
Chanjo ni sababu ya wave inayoweza kuja tena na elements zilizobaki za ugonjwa.

Pia itakua requirement kama yellow fever kwamba huwezi safiri nchi yeyote bila vaccine ya Covid.

Tukishafika huko ndio uje umsifie huyo marehemu ambaye licha ya kumsifia hapa alikua anatumia mashine za mabeberu kurefusha maisha ya moyo wake!!!

Kama alikua na jeuri si angetoa mashine amtegemee Mungu tu!!

NB: Hizo kejeli hazisadii kama wakatoliki wamepoteza mapadri na walei 60 ina maana kma chanjo ingekuwepo au measures za Covid number ingeshuka kuliko hapo.
 
Haya magonjwa ya milipuko na mengine yako tangu karne nyingi zilizopita, na binadamu anatafuta namana ya kupambana nayo ili yasimzuru kwa kiwango kikubwa na kumuua, aendelee kuishi kwa muda mrefu, hivyo chanjo ni ktk mahangaiko ya binadamu kutetea uhai wake, na chanjo inaweza kuleta mazara kidogo ila ikasaidia WATU Wengi wasife kwa ugonjwa huo au ikasababisha mazara makubwa zaidi, au hata bila kutumia dawa yeyote bado ugojwa unaweza kuondoka bila hata kujua. kuna magonjwa mengi hata binadamu hajui kama yapo, na binadamu bado anatafuta njia nyingine mbali mbali kupambana na maadui wanaomkabili, Hakuna haja ya kuwasema wengine vibaya wala kuwashutumu, WOGA na WASIWASI ni adui mkubwa, tusiwatishe watu, Tudumishe UPENDO na kutiana moyo na maisha yataendendelea kwa MAFANIKIO.
 
Nawaza sana juu ya tume ya rais isije pendekeza tuchanjwe ilihali Mungu katuepusha sana na janga hili.
 

Hapa ninapata shida kidogo, hão watu 40 walikufa kwa covid ama kwa mkanyagano? Pili je kuna uwakika na hilo ama kuna watu walitaka kupaka matope msiba ili kutisha watu kuwa kuna corona
 
Jambo lipi Si kuna Moderna na Pfizer au zile za warusi nani kaganda damu? Kuna mtu kawazuia msitumie?

Tuache kuleta taharuki isiyo ya lazima

fanya uchunguzi wako binafsi ndg. uwe na siku njema
 
Jambo lipi Si kuna Moderna na Pfizer au zile za warusi nani kaganda damu? Kuna mtu kawazuia msitumie?

Tuache kuleta taharuki isiyo ya lazima
Urusi nchi ya kidikteta hata wakiganda nani athubutu kuandika,hakuna dawa isiyo na side effects.
 
Nawaza sana juu ya tume ya rais isije pendekeza tuchanjwe ilihali Mungu katuepusha sana na janga hili.
Nashauri pia tuache kutumia ARV na neti za mabeberu ili tumtegemee Mungu atuponye VVU na Malaria. Au unaonaje mkuu?
 
Hakuna dawa inayomkubali kila mtu duniani... kinachoangaliwa ni katika watu wanatumia ni asilimia ngapi inawaathiri vibaya. Kama faida ni kubwa kuliko hasara, twende kazi.
 
Urusi nchi ya kidikteta hata wakiganda nani athubutu kuandika,hakuna dawa isiyo na side effects.
Msikuze mambo walioganda hata 30 hawafiki kati ya sample ya watu million 20.... Wewe unafaham the higher the sample ndio less margin of error so huwezi conclude kwamba watu 6 wafanye dozi ipigwe marufuku!! That is not right haifiki hata 0.0001
 
Chanjo sio kitu cha kukurupukia ni hatari sana kwa sababu inacheza sana na masuala ya hali ya hewa hasa joto hivyo hata ukipoteza 0.1 ⁰c unatengeneza kitu kingine cha ajabu ambacho madhara yake huyajui.
Kutokana na hali yetu ya kiuchumi na maendeleo ya kisayansi Nafikiri hatutakiwi kukurupukia hii kitu bali tufanye jitahada hizi za kuendelea kuchukua taadhari....
Hivi HIV inachanjo?....
Nijuavyo kwa uchache kirusi n tabu sana kukiangamiza kutokana na sifa zake.

Ngoja wataalamu wa masuala ya tiba tuwasikilize nao wanasemaje
 
Namhurumia Kamanda Mbowe, umri wake ni chini ya 60, alafu kachoma chanjo "inayogeuza dna iende rivasi"
 
Ukiweka pembeni sayansi

Sayansi ni 'open ended discipline'. Nadharia moja huendelea kufanyiwa kazi mpaka hapo nadharia nzuri zaidi itakapopatikana. Na ndiyo maana mwanzoni watu waliamini 'dunia ni mviringo' mpaka hapo nadharia ya kusema dunia siyo mviringo, bali ina umbo la yai (oval) ilipopatikana na ndiyo inayofanyiwa kazi. Akija mwanasayansi mwingine akisema dunia ni 'pembe tatu' na hoja zake zikakosa upinzani (zikapita bila kupingwa), then tutaanza kufanyia kazi nadharia hiyo. Vivyo hivyo, katika nyanja mbalimbali. Hivyo, kwa sasa wanasayansi bado wanatafiti juu ya chanjo ambazo zimeshapatikana kuona kama ni effective na faida zinazidi hasara au hasara zinazidi faida. Hadi sasa ukilinganisha watu ambao wameshafariki kutokana na kutumia chanjo na wale ambao bado wanaishi kutokana na kutumia chanjo, bado inaonekana faida ni nyingi kuliko hasara. Kwenye majaribio ya sayansi, matokeo chanya au hasi ya jaribio ni kitu cha kawaida sana. Ndiyo maana majaribio lazima yarudiwe rudiwe ili kujiridhisha na usahihi wa matokeo yake. Kuna jambo lingine ambalo lipo katika wasomi mbalimbali - mitazamo tofauti kuhusu jambo fulani na ujengaji wa hoja tofauti. Hili nalo lina umuhimu wake. In conclusion, niseme hadi sasa wanasayansi wamefanya kazi kubwa kudhibiti maambukizi ya Covid-19. Ukiangalia takwimu za nchi ambazo zinashirikiana kupambana na Covid-19 (ukiondoa zile ambazo zina dash-dash) watu 241, 257,65 9 (99.6%) duniani wako katika mild condition (wenye maambukizi yasiyowadhuru), watu 106,591 (0.4%) wako katika hali ya hatari, watu 111, 647, 084 (97%) wamepona na watu 2,986,118 (3%) wamefariki. Kwa takwimu hizi, we on track kutokana na juhudi ambazo zimechukuliwa worldwide. Source: Worldmoter report (last updated: April 15, 2021, 06:28 GMT).
 
JPM alikuwa hard working. Alikuwa halali mapema kwa sababu yako na mimi.

Alikuwa anakesha anawaza na kufanya uchunguzi kwa ajil yangu na wewew.

Rest easy JPM.
 
J & J imeleta madhara kwa watu wawili, mmoja amefariki na mwingine yupo mahututi... Mbona unautisha umma
Vifo ni vingi, vinafichwa kwa lengo la kuipa dunia matumaini katika usalamo wa chanjo. Vifo hivyo vingekuwa vinatokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe Africa hadi picha zingewekwa hadharani. Ni vifo vya wakubwa kw ajili ya biashara za wakubwa. Acha tuone.
 
Endeleeni na propaganda na kujipa moyo. Ni kweli hadi sasa j & j na astrazeneca zimegundulika kuwa na tatizo la blood-clot, kiufupi ni idadi ndogo ya watu wanaoathirika na tatizo hilo. Nadhani pia litafanyiwa kazi.

Sioni kama changamoto hii ndogo ndio sababu ya kukimbilia kufusha na miti shamba. Hii ina sehemu yake, lakini katu siamini kama bila ya sayansi tutavuka kwenye covid-19. Mungu yupo, lakini tusipange lazima dawa itoke kwenye miti shamba.

Ikiwa Malaraia na magonjwa mengine yote tunatumia dawa za sayansi, basi na hili pia lazima sayansi itumike. Untengenezaji na testing ya hizi vacine za covid ulikuwa mfupi kwa pressure ya watu kutaka tatizo liondoke. Ndio chanzo kikuu cha issue ndogo ndogo kama hizo za blood-cloting hazikuonekana wakati wa testing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…