Hayati Magufuli aliona mbali kuhusu chanjo, ona sasa huko Ulaya wanavyoanza kupukutika

Sasa hivi tunawachanja Astrazeneca watu wenye kuanzia umri wa miaka 55 na kuendelea huko, tupo vizuri na Astrazeneca zetu.
 
Kwani chanjo inazuia kifo?
Hapana. Lakini inaongeza (sana) uwezekano uishi hadi umri unaolingana na maumbile yako na mazingira yako.
Hayati Magu aliaga dunia mapema kidogo kwa sababu alikuwa na matatizo ya moyo (ambayo yangemwua tayari miaka 100 iliyopita katika mazingira tofauti pasipo na tiba ya kisasa na mitambo yake) na katika udhaifu huo hakuweza kuvumilia maambukizo ya Covid - ambayo angeshinda kama angepokea chanjo.
Hivyo ndivyo naona uwezekano mkubwa nikiangalia habari zote zinazopatikana.
 
Unajua maana ya nabii wewe?
Nabii ni yeyote hata wewe. Ila kwa waswahili waliokombwa akili vichwani lazima nabii awe mweupe au mwarabu. Kimsingi, hata mimi ni nabii humu JF tokana na kuwapa mawazo yenye kuwavusha katika mengi. Si vibaya kusema Magufuli, Nyerere, Mkapa, Mwinyi minus Kikwete ni manabii.
 
Kwako wazungu ni binaadamu spesho ni tofauti na viumbe wengine,hapo ndio panapofanya tusielewane. Yani kwa sababu wanatengeneza ndege au madawa ni sababu ya uzungu wao kwamba uzungu ndio huwafanya waweze kufanya hayo yote.
 
Kwahiyo tuseme chanjo za China sio bora ndio maana pamoja na Magufuli kuchanja ila kafa kwa corona?
 
Hujalazimishwa wacha tu ukafe maana huna cha kuacha zaidi ya card ya uvccm
Unasema sijalamishwa wakati siwezi kwenda kuhiji bila kudungwa chanjo, yani nalazimishwa nidungwe chanjo ndio nikagandie damu huko Saudia bila ya hivyo huwezi kwenda.
 
Kama ni kawaida kwanini zinazungumziwa na baadhi ya nchi kuchukua hatua mbalimbali kama kusitisha matumizi kwa vijana?
 
Hili la chanjo kugandisha damu walikuwa wanalijua hao wanasayansi?
 
Kama ni kawaida kwanini zinazungumziwa na baadhi ya nchi kuchukua hatua mbalimbali kama kusitisha matumizi kwa vijana?
Wenzetu ni waoga sana na medical malpractice. Kitu kidogo tu, wanalipishwa fidia kubwa sana, ndio maana wako cautious. Lakini namba hazidanganyi, walioathirika ni kidogo mno, negligible
 
mnasumbuka sana nyie magafulists kwa hoja za kuokoteza hamjambo
 
Jiulize wachina ambako wao ndio wa mwanzo kukabiliana na covid, basi nao pia wanatumia vacine kupambana na janga hili. China iko mbali sana kwa sayansi ya miti shamba kuliko TZ!
 
Jiulize wachina ambako wao ndio wa mwanzo kukabiliana na covid, basi nao pia wanatumia vacine kupambana na janga hili. China iko mbali sana kwa sayansi ya miti shamba kuliko TZ!
Kwahiyo ulitaka kusema nini?
 
Kwahiyo ulitaka kusema nini?
Miti shamba haifanyi kazi kwa covid-19, nina hakika wachina walijaribu mitishamba kwanza maana imo ndani ya utamaduni huo. Na kwa kweli wako fiti sana na miti shamba.
 
Miti shamba haifanyi kazi kwa covid-19, nina hakika wachina walijaribu mitishamba kwanza maana imo ndani ya utamaduni huo. Na kwa kweli wako fiti sana na miti shamba.
Sijui hata unaongea nini mkuu, hivi unaposema mitishamba haifanyi kazi kwa covid sijui hata wewe kama unaelewa vizuri hiyo kauli.

Chanjo sio tiba ya covid Hivyo hadi sasa huko China hawana dawa ya Covid, kwahiyo tuseme sayansi haifanyi kazi kwa covid?
 
Hivi kipindi Jpm yupo hai mlimpigia kelele sana kuhusu corona mbona sasa hakuna hizo kelele tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…