Hayati Magufuli aliona mbali kuhusu chanjo, ona sasa huko Ulaya wanavyoanza kupukutika

Hayati Magufuli aliona mbali kuhusu chanjo, ona sasa huko Ulaya wanavyoanza kupukutika

Idadi waliopata tatizo la kuganda damu walikuwa 4-5 kati ya milioni 1 wastani. Ambayo ni kawaida kwa chanjo. Nadhani wengi wetu wamepata chanjo ya ukambi / measles. Hata baada ya chanjo ya ukambi kuna mshtuko wa mfumo wa kinga (anaphylactic shock) kwa watu 3.5-10 kati ya milioni.
Kama marehemu rais angejipatia chanjo angekuwa hai.
Kwani chanjo inazuia kifo?
 
Anhaaaa sasa unaonaje tuandae petition tuzuie ARVs ili sasa wagonjwa wetu wa VVU wamtegemee tu Mungu na kula malimao?

Vilevile Radiotherapy,MRI na CT scan zipigwe marufuku, Chermo na insuline pia zizuiwe maana fatality rate yake ni kubwa sana. Mind you zote ni za mabeberu walewale tu
Hiyo midawa ukianza kutumia halafu ukiicha ghafla unakufa. Halafu nakushangaa sana mkuu unataka tuabudu wazungu nini? maana hutaki wakosolewe kabisa maana kama hili la chanjo hata wao wanaona mambo hayapo na kuacha hatua kadhaa ila wewe hutaki tulizungumzie hilo kisa waafrika na hao ni wazungu hivyo hawakosei.
 
Kweli kuna binadamu wanaishi maisha na wengine wanawasindikiza maisha
Kwa hiyo hata ukifa na ugonjwa wowote huna umuhimu duniani,
Msubiri "Mungu" atakuja kukuwekea mambo sawa......
 
Mwanzo na nani? Mie msimamo wangu siku zote ni kwamba dawa zote duniani zina side effects ila cha msingi ni kwamba maadam 99.9% wanaipata successfully then hyo 0.001% ikipata madhara sio issue kubwa.

Sasa watu zaidi ya 17 M wamedungwa Astra Zeneca alafu waliopata blood clots ni watu 18 cjui.... Hvi kweli ni percentage ya kudoubt dawa?

Chanjo na tiba naziongelea sababu zote zina side effects as long as zinaingia kwenye mzunguko wa damu. Na kama hufahamu katika kila watu laki 2 mmoja anakufa kwa chanjo ya YF Vax uya homa ya manjano ambayo kila mbongo mwenye passport amedungwa ukiwemo wewe.

Una maoni gani? Ipigwe marufuku pia
View attachment 1752813
WHO walikuwa wakataa kabisa kuhusu Astrazeneca kugandisha damu na wewe kila pale watu wanaposema Astrazeneca inagandisha damu. Wewe mara useme sio lazima Astrazeneca zipo chanjo zengine mara kila chanjo ina side effects mara waliyotumia Astrazeneca bila kupata madhara ni wengi kuliko waliopata madhara.
 
Bahati mbaya unabishana na watu waliokwisha amua kutokuwa rational kabisa wakifuata nyayo za Hayati.

Mwanzoni, propaganda yao kubwa ilikuwa chanjo inaletwa ili kutumaliza waafrika/Watanzania kuwezesha “mabeberu” wachote rasilimali zetu! - dhana ya vita vya kiuchumi ya JPM.

Huwezi kuwaelewesha kitu watu wa aina hii. They’ve chosen to be completely irrational.
Drifter umeniwahi,
I was about to let zitto junior, not to waste his time na hawa covidiots
Kama maisha yao ni kusindikiza maisha, they have nothing to lose, have they... ?
 
Kwahiyo hizi chanjo cha corona zipo kwenye majaribio?
Hata kama haziko kwenye majaribio, lazima wanasayansi mbalimbali wazifanyie utafiti kujiridhisha kama zina ubora au la. Ni kama wewe unapoenda kununua kitu kipya dukani, huamini tu kama ni kitu kipya, utafanya juu-chini ujiridhishe kama ni kitu kipya kweli.
 
Dawa ni kwa ajiri ya wagonjwa ila hapa tunazungumzia chanjo sio dawa, kama kuganda damu ni moja ya side effects za hizo chanjo basi wangetuambia kabisa ili tujue.
Tatizo ni ubishi usiokuwa na maana.... ungesema waliopewa chanjo ni watu kadhaa, kati ya hao kadhaa wamekufa kwa kuganda damu, ili tujue risk factor zake. Hata ARV kuna watu wakitumia side effects zake ni kupata temporary insanity. Kama nilivyosema hakuna medical product inayomkubali kila mtu. Hata dawa za headache kuna watu zinawakataa. Tatizo kwenye hili jambo tumetanguliza politics over science.
Kinachotokea huko kwa wenzetu lakini si unakiona mkuu na hatua wanazochukua kuhusu hizo Astrazeneca? mwanzoni mlikuwa mnakataa kuwa hizi chanjo hazigandishi damu ila sasa hivi hilo suala lipo wazi na tumeona wengine wamesitisha kwa wenye miaka chini ya 60 na sio Astrazeneca tu bali sasa hivi na Johson& Johnson nazo tunasikia zina tatizo hilo.

Sasa hapo hao nao ni wabishi?
Side effects ni jambo la kawaida, nimekwambia issue ni wangapi wanapata faida vs wanaopata hasara. Hizo ndio namba muhimu. Hata magari yanaua watu, sijawahi kusikia mtu akisema tuzuie magari kabisa
 
Hiyo midawa ukianza kutumia halafu ukiicha ghafla unakufa. Halafu nakushangaa sana mkuu unataka tuabudu wazungu nini? maana hutaki wakosolewe kabisa maana kama hili la chanjo hata wao wanaona mambo hayapo na kuacha hatua kadhaa ila wewe hutaki tulizungumzie hilo kisa waafrika na hao ni wazungu hivyo hawakosei.
Wewe mbona ARV unatumia na hazikugandishi damu?
 
WHO walikuwa wakataa kabisa kuhusu Astrazeneca kugandisha damu na wewe kila pale watu wanaposema Astrazeneca inagandisha damu. Wewe mara useme sio lazima Astrazeneca zipo chanjo zengine mara kila chanjo ina side effects mara waliyotumia Astrazeneca bila kupata madhara ni wengi kuliko waliopata madhara.
Hujalazimishwa wacha tu ukafe maana huna cha kuacha zaidi ya card ya uvccm
 
Kwani alipata kama sadaka kwamba ni msaada?
Oooh kumbe usipopewa msaada wanageuka Wadau wa maendeleo ila ukipewa bure ndio wanakua mabeberu?

Mbona hamueleweki msimamo wenu? Kama mabeberu ni wabaya na wanataka kutuua hamuogopi Bombardier zao watazihack zilipuke ili waje kuchukua rasilimali zetu? Hahahaha
 
Sasa mbna imemdedisha????
Kile tunachofahamu juu ya vidonge vya damu visivyo vya kawaida vilivyounganishwa na chanjo ya J & J .

Wataalam wanafikiria jinsi ya kugundua haraka na kutibu mgando usio wa kawaida unaosababishwa na dozi za Johnson & Johnson na AstraZeneca.

Wakati mamilioni ya watu wanapata chanjo, waganga wanatarajia maeelfu kadhaa watakua na damu yenye vinasaba au visababishi vya kugandisha damu.

"Chanjo imeunganishwa wazi na shida hii adimu," anasema Warkentin, ambaye ni mwandishi mwenza kwenye moja ya majarida ya NEJM. "Tuna bunduki inayofuka moshi ."

Hatujui bado ikiwa kuna viambatisho vya maumbile au utabiri mwingine dhahiri ambao unaweza kuwafanya watu waweze kukabiliwa na hali hii. "Tunajua kutoka kwa utafiti wa HIT kwamba hatuwezi kutabiri ni nani atakayekuza shida hii," anasema Warkentin.

Kinachojulikana ni kwamba huwa inawagonga wanawake wadogo. Wagonjwa wote sita hukomarekani walikuwa wanawake kati ya umri wa miaka 18 na 48, na idadi kubwa ya wagonjwa huko Ulaya walikuwa chini ya miaka 60. Wataalam hawawezi kusema kwa hakika, lakini wana dalili za kwanini damu huganda.

Hizi dawa za chanjo naona kama zinafanyiwa majaribio direct kwa binadamu na sasa majawabu yanaanza kujitokeza. Kama haitoshi chanjo hizo aina mbili zimestishwa mpaka litakapotolewa tangazo jingine.
 
Wanasayansi walikiuka utaratibu wa majaribio ya Chanjo.

Sjawahi kuona ugunduzi wa tiba unaanza majaribio moja Kwa moja Kwa binadamu, ndio mara ya Kwanza.

Wanajua wanachoitafutia hii dunia yenye uwingi wa watu na majengo mengi yanayotaka kuielemea dunia.
Suala hapa no Udharura mkuu ...Corona ni balaa
 
WHO walikuwa wakataa kabisa kuhusu Astrazeneca kugandisha damu na wewe kila pale watu wanaposema Astrazeneca inagandisha damu. Wewe mara useme sio lazima Astrazeneca zipo chanjo zengine mara kila chanjo ina side effects mara waliyotumia Astrazeneca bila kupata madhara ni wengi kuliko waliopata madhara.
The thing is 99% hawagandi damu so bado WHO wapo sahihi..... Watu 20 out of million 17 is too little to observe as a setback!!

Hata waliotumia ARV kuanzia 2010 ukiwahoji leo trust me 10% wanadevelop complications nyingine ila sababu ni sample ndogo hawawezi kuzipiga marufuku same to Astra zeneca walau ikifika 1% ndio itakua too big to neglect.
 
Back
Top Bottom