chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Wanasiasa usiwaamini
Sisi tukishangilia hotuba za JPM zilizoutukuza umasikini wetu, na kwa kweli watanzania wengi tuliona fahari kubwa sana kuwa masikini na kuwa wanyonge. Mtu yeyote aliyejifanya kutafuta utajiri tulifanya hima kimchongea Kila mahala, na kama ana shamba, basi tulilivamia, na tukampachika majina yote mabaya.
Kumbe upenuni tu Kuna vijana wake walitopea kwenye utajiri wa kutisha kabisa, Sasa kwa nini alituhadaa tuutukuze umasikini wakati vijana wake aliwapa fursa ya kutajirika?
Maana mtu masikini ndiye alionekana mzalendo, Sasa hawa inakuwaje wanatajirika wakati wanatuimbia kwamba umasikini ndio uzalendo?