Hayati Magufuli aliwezaje kukopa kwa Wazungu ikiwa aliharibu uhusiano na nchi za Ulaya?

Jiwe alikopa nchi za kiarabu mfano Kuwait fund, Morocco, UAE, n.k

Hakupenda kwenda kukopa nchi zinazokazia utawala bora maana alikuwa dikteta
Hakuna nchi inayokazia utawala bora, ni suala la maslahi tu
 
Unamaanisha Mrusi anaweza kumkopa mmarekani katika Hali ya sasa? Au Ukraine akamkopa urusi?
 
Unakimbia hoja elekezi, aliwezaje kukopa ikiwa aliharibu uhusiano?
Mbona nimetoa jibu. Aliharibu uhusiano na nchi za ulaya na Marekani wanakosimamia misingi ya utawala bora. Ndiyo maana akaenda huko kwa madikteta wenzake. Upo hapo?
 
Mikopo ya biashara au benki binafsi hata Putin akitaka Kukopa Marekani atapewa maana ina riba kubwa na mda mfupi wa marejesho..

Ila concessional loans hupewi na Wala ile mikopo yenye sura ya msaada kama wa covid hupewi
Putin ana sanctions Marekani, so that's most likely a stretch.


But I get your larger point.
 
Mbona nimetoa jibu. Aliharibu uhusiano na nchi za ulaya na Marekani wanakosimamia misingi ya utawala bora. Ndiyo maana akaenda huko kwa madikteta wenzake. Upo hapo?
Ulaya na Marekani hawahawa wanaoshirikiana na:
• Serikali ya Saudi Arabia inayouwa wapinzani katika balozi zao nchi za kigeni?
• Serikali ya China pamoja na kuwatesa Waislam wa Uyghurs, ku-limit demokrasia, n.k?
• Wanaoshindwa kukubaliana kuweka vikwazo vya uhakika kwa nishati ya Urusi?
• Serikali ya Myanmar pamoja na kuuwa maelfu kama siyo mamilion ya Warohingya?
• N.k?

Hao wanaangalia masilahi yao mkuu, usidanganyike na porojo za utawala bora.
 
Mkuu acha basi kutuona na sisi Wakinga huku ndani kama ndugu zako wa huko vijijini,yani hadi sisi humu unataka kutudanganya kuwa miradi ilijengwa na fedha za ndani??
 
Reactions: Qwy
Kutokutaka kuwa wanyonge solution ndio ilikuwa kwenda kukopa kwenye benki za kibiashara. Kuamia Dodoma kulikuwa na ulazima gani??
 
Sawa. Ni kweli, kila kizazi kina wajibu wake katika taifa na inapotokea kizazi fulani hakifanyi sehemu yake basi Taifa linabaki nyuma na ule mzigo unabebwa na kizazi cha mbele.

JPM alijaribu kurekebisha hilo, ni jambo zuri ila unalibeba kwa kiwango gani? Kwa gharama gani?

Nikuulize: nini kanatokea pale utakapojaribu kurekebisha madhaifu ya babu zako wote ndani ya miaka ya ujana wako?
Uhakikishe wajukuu wa babu zako wana nyumba, wana usafiri.

Kitakachokupata ni kwamba watoto wako wa kizazi chako watateseka kwa matatizo waliyorithi kutoka kwa babu zao na watakuchukia kwa kuwalazimisha kurekebisha udhaifu wote wa babu zao ndani ya kipindi cha maisha yao.

Ukumbuke raisi wa nchi ni binadamu kama wewe ila yeye anapigiwa saluti, na vizazi vyake vina urithi huenda kwa miaka mingi mbele.

Tofauti ni kuwa, wewe mlipa kodi wa kawaida unatakiwa uijenge nchi yako na katika kuijenga unatakiwa kuhakikisha umeacha mirija ya uchumi katika vizazi vyako vya mbele.

Hakuna mzazi atakayetaka mtoto wake azaliwe akute Taifa tuna mandege na matreni yaliyonunuliwa ndani ya awamu moja na raisi wake anasifiwa kwa kufanya hivyo ila yeye hana ardhi wala nyumba sababu baba yake alitumia uchumi wake kuijenga nchi.

Tuijenge nchi kwa kubeba kile ambacho mwili wetu unaweza kubeba katika wakati husika ili vizazi vyetu vitakapokuja vimsifu kiongozi wetu na viwabariki wazazi kwa kuwaandalia maisha mazuri.
 
Mbona nimetoa jibu. Aliharibu uhusiano na nchi za ulaya na Marekani wanakosimamia misingi ya utawala bora. Ndiyo maana akaenda huko kwa madikteta wenzake. Upo hapo?
So waarabu ni madikteta?
 
Mkuu,
Siyo kwamba hatuna uwezo wa kupambana na matatizo yetu.

Magufuli ametuonesha kwa vitendo inawezekana kabisa kujenga nchi kwa kodi zetu wenyewe, na mikopo michache sana.

Ukumbuke pia hilo deni la karibu Trillion 30 linahusisha na madeni yaliyoiva ya nyuma ambayo amepambana sana kuyalipa.

Ametufundisha inawezekana kabisa kuendesha nchi vizuri bila misaada ya mabeberu na tukapata maendeleo.

Sote tu mashahidi wa hili, na namba hazidanganyi. Si dhambi kufanya kwa kasi kubwa kama uwezo upo.
 
Mkuu acha basi kutuona na sisi Wakinga huku ndani kama ndugu zako wa huko vijijini,yani hadi sisi humu unataka kutudanganya kuwa miradi ilijengwa na fedha za ndani??
Kwani hakuna Miradi iliyojengwa kwa fedha za ndani? Unafahamu kama kuna Miradi ilifanyika kwa kuahirishwa shughuli fulani za Serikali na pesa kupelekwa kwenye hiyo Miradi?
 
Hoja nzito sana!

Magufuli hajawahi kwenda kubembea Dubai ila huyu mmh!
 
Unakuta choo kimeandikwa: kwa hisani ya msaada wa fedha za oviko 19..hahahaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…