Hayati Magufuli aliwezaje kukopa kwa Wazungu ikiwa aliharibu uhusiano na nchi za Ulaya?

Hayati Magufuli aliwezaje kukopa kwa Wazungu ikiwa aliharibu uhusiano na nchi za Ulaya?

Jiwe alikopa nchi za kiarabu mfano Kuwait fund, Morocco, UAE, n.k

Hakupenda kwenda kukopa nchi zinazokazia utawala bora maana alikuwa dikteta
Hakuna nchi inayokazia utawala bora, ni suala la maslahi tu
 
Swali lako ni la kipumbavu. Lina akisi upeo mdogo ulionao. Mikopo ni biashara ya mabenki. Yeyote mwenye dhamana anakopa hata adui yako. Magufuli amekopa kwenye commercial banks sana kama ifuayavyo;
-Credit Suisse
-African Development Bank
-Standard Chatered Bank
-East African Development Bank
- Exim Bank of China
Unamaanisha Mrusi anaweza kumkopa mmarekani katika Hali ya sasa? Au Ukraine akamkopa urusi?
 
Unakimbia hoja elekezi, aliwezaje kukopa ikiwa aliharibu uhusiano?
Mbona nimetoa jibu. Aliharibu uhusiano na nchi za ulaya na Marekani wanakosimamia misingi ya utawala bora. Ndiyo maana akaenda huko kwa madikteta wenzake. Upo hapo?
 
Mikopo ya biashara au benki binafsi hata Putin akitaka Kukopa Marekani atapewa maana ina riba kubwa na mda mfupi wa marejesho..

Ila concessional loans hupewi na Wala ile mikopo yenye sura ya msaada kama wa covid hupewi
Putin ana sanctions Marekani, so that's most likely a stretch.

But I get your larger point.
 
Mbona nimetoa jibu. Aliharibu uhusiano na nchi za ulaya na Marekani wanakosimamia misingi ya utawala bora. Ndiyo maana akaenda huko kwa madikteta wenzake. Upo hapo?
Ulaya na Marekani hawahawa wanaoshirikiana na:
• Serikali ya Saudi Arabia inayouwa wapinzani katika balozi zao nchi za kigeni?
• Serikali ya China pamoja na kuwatesa Waislam wa Uyghurs, ku-limit demokrasia, n.k?
• Wanaoshindwa kukubaliana kuweka vikwazo vya uhakika kwa nishati ya Urusi?
• Serikali ya Myanmar pamoja na kuuwa maelfu kama siyo mamilion ya Warohingya?
• N.k?

Hao wanaangalia masilahi yao mkuu, usidanganyike na porojo za utawala bora.
 
Mikopo mingi iliyotolewa awamu ya tano ni ile iliyosainiwa awamu ya nne na kuiva kipindi ambacho Magufuli yupo madarakani, hili Wanasiasa wanalifahamu lakini hawawezi kusema.

Magufuli alikuwa makini sana kwenye suala la matumizi ya fedha, asingekubali kuchukua Mikopo yenye Masharti magumu, ndiyo maana wakati wa kuanzisha Mradi wa Reli "SGR" waliomba Mkopo lakini ukawa na masharti magumu, wakaacha na kuanza kujenga kwa fedha za ndani.
Mkuu acha basi kutuona na sisi Wakinga huku ndani kama ndugu zako wa huko vijijini,yani hadi sisi humu unataka kutudanganya kuwa miradi ilijengwa na fedha za ndani??
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Tulipopata uhuru Mwl. Julius Nyerere alitutangazia maadui watatu: maradhi, ujinga na umasikini. Awamu zote zimekuwa zikipambana nayo kwa nafasi yake bila mafanikio ya kuridhisha.

Aina ya uongozi wa Magufuli ulilenga walau kufanya mambo kwa utofauti na matokeo chanya tuliyaona ndani ya muda mfupi. JPM hakutaka kufanya kila kitu peke yake, ila alitaka walau tuwe tulipopaswa kuwa baada ya miaka 60 ya uhuru.

Ukweli ni kuwa tupo nyuma sana, miaka 60 ya uhuru:
• Hatuna vyanzo vya uhakika vya umeme
• Tuna mfumo na miundombinu duni ya elimu
• Hatuna miundombinu bora ya usafiri kuanzia nchi kavu, maji na hata anga
• Hatuna huduma na miundombinu bora ya afya
• Tumeshindwa hata kuhamia Dodoma
• You name them

Kama Rais Mzalendo, asingeweza kufanya mambo kwa mazoea. Tuna utajiri mwingi sana lakini sisi ni masikini sana, yote ni kwa kuwa tuna ombwe la uongozi.

Marekani na mataifa mengine wana malengo na masilahi yao. Kama wataona una-serve interests zao watakuwa na wewe, kama hauwasaidii chochote wataachana na wewe na kama utawaletea vizingiti kwenye ku-achieve interests zao watapambana na wewe. Ndiyo mfumo wa dunia ulivyo.

Rais na Mzalendo wa kweli ni yule atakayesimamia malengo ya nchi na wananchi wake.

Magufuli hakutaka tuwe wanyonge mbele ya mataifa ya kinyonyaji. Na ndio sababu he pulled us out of a handful of unfair deals and contracts. Kwamba wao wakichukua madini ya kila aina ya thamani kubwa eti watupoze kwa vyandarua na au ARVs. Yes, tunavihitaji hivyo vitu lakini not at the expense of unfair deals.

Alitaka tufaidike na kupata stahiki yetu halali. Hakufanikiwa sana, ila walau alituweka sehemu nzuri. Mambo ni mengi, ila kwa kuhitimisha, asingeweza kuepuka kukopa, lakini tumhukumu kwa kuangalia effectiveness ya hiyo mikopo.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
Kutokutaka kuwa wanyonge solution ndio ilikuwa kwenda kukopa kwenye benki za kibiashara. Kuamia Dodoma kulikuwa na ulazima gani??
 
Tulipopata uhuru Mwl. Julius Nyerere alitutangazia maadui watatu: maradhi, ujinga na umasikini. Awamu zote zimekuwa zikipambana nayo kwa nafasi yake bila mafanikio ya kuridhisha.

Aina ya uongozi wa Magufuli ulilenga walau kufanya mambo kwa utofauti na matokeo chanya tuliyaona ndani ya muda mfupi. JPM hakutaka kufanya kila kitu peke yake, ila alitaka walau tuwe tulipopaswa kuwa baada ya miaka 60 ya uhuru.

Ukweli ni kuwa tupo nyuma sana, miaka 60 ya uhuru:
• Hatuna vyanzo vya uhakika vya umeme
• Tuna mfumo na miundombinu duni ya elimu
• Hatuna miundombinu bora ya usafiri kuanzia nchi kavu, maji na hata anga
• Hatuna huduma na miundombinu bora ya afya
• Tumeshindwa hata kuhamia Dodoma
• You name them

Kama Rais Mzalendo, asingeweza kufanya mambo kwa mazoea. Tuna utajiri mwingi sana lakini sisi ni masikini sana, yote ni kwa kuwa tuna ombwe la uongozi.

Marekani na mataifa mengine wana malengo na masilahi yao. Kama wataona una-serve interests zao watakuwa na wewe, kama hauwasaidii chochote wataachana na wewe na kama utawaletea vizingiti kwenye ku-achieve interests zao watapambana na wewe. Ndiyo mfumo wa dunia ulivyo.

Rais na Mzalendo wa kweli ni yule atakayesimamia malengo ya nchi na wananchi wake.

Magufuli hakutaka tuwe wanyonge mbele ya mataifa ya kinyonyaji. Na ndio dababu he pulled us out of a handful of unfair deals and contracts. Kwamba wao wakichukua madini ya kila aina ya thamani kubwa eti watupoze kwa vyandarua na au ARVs. Yes, tunavihitaji hivyo vitu lakini not at the expense of unfair deals.

Alitaka tufaidike na kupata stahiki yetu halali. Hakufanikiwa sana, ila walau alituweka sehemu nzuri. Mambo ni mengi, ila kwa kuhitimisha, asingeweza kuepuka kukopa, lakini tumhukumu kwa kuangalia effectiveness ya hiyo mikopo.

Mnyonge mbyongeni, haki yake mpeni.
Sawa. Ni kweli, kila kizazi kina wajibu wake katika taifa na inapotokea kizazi fulani hakifanyi sehemu yake basi Taifa linabaki nyuma na ule mzigo unabebwa na kizazi cha mbele.

JPM alijaribu kurekebisha hilo, ni jambo zuri ila unalibeba kwa kiwango gani? Kwa gharama gani?

Nikuulize: nini kanatokea pale utakapojaribu kurekebisha madhaifu ya babu zako wote ndani ya miaka ya ujana wako?
Uhakikishe wajukuu wa babu zako wana nyumba, wana usafiri.

Kitakachokupata ni kwamba watoto wako wa kizazi chako watateseka kwa matatizo waliyorithi kutoka kwa babu zao na watakuchukia kwa kuwalazimisha kurekebisha udhaifu wote wa babu zao ndani ya kipindi cha maisha yao.

Ukumbuke raisi wa nchi ni binadamu kama wewe ila yeye anapigiwa saluti, na vizazi vyake vina urithi huenda kwa miaka mingi mbele.

Tofauti ni kuwa, wewe mlipa kodi wa kawaida unatakiwa uijenge nchi yako na katika kuijenga unatakiwa kuhakikisha umeacha mirija ya uchumi katika vizazi vyako vya mbele.

Hakuna mzazi atakayetaka mtoto wake azaliwe akute Taifa tuna mandege na matreni yaliyonunuliwa ndani ya awamu moja na raisi wake anasifiwa kwa kufanya hivyo ila yeye hana ardhi wala nyumba sababu baba yake alitumia uchumi wake kuijenga nchi.

Tuijenge nchi kwa kubeba kile ambacho mwili wetu unaweza kubeba katika wakati husika ili vizazi vyetu vitakapokuja vimsifu kiongozi wetu na viwabariki wazazi kwa kuwaandalia maisha mazuri.
 
Mbona nimetoa jibu. Aliharibu uhusiano na nchi za ulaya na Marekani wanakosimamia misingi ya utawala bora. Ndiyo maana akaenda huko kwa madikteta wenzake. Upo hapo?
So waarabu ni madikteta?
 
Sawa. Ni kweli, kila kizazi kina wajibu wake katika taifa na inapotokea kizazi fulani hakifanyi sehemu yake basi Taifa linabaki nyuma na ule mzigo unabebwa na kizazi cha mbele.

JPM alijaribu kurekebisha hilo, ni jambo zuri ila unalibeba kwa kiwango gani? Kwa gharama gani?

Nikuulize: nini kanatokea pale utakapojaribu kurekebisha madhaifu ya babu zako wote ndani ya miaka ya ujana wako?
Uhakikishe wajukuu wa babu zako wana nyumba, wana usafiri.

Kitakachokupata ni kwamba watoto wako wa kizazi chako watateseka kwa matatizo waliyorithi kutoka kwa babu zao na watakuchukia kwa kuwalazimisha kurekebisha udhaifu wote wa babu zao ndani ya kipindi cha maisha yao.

Ukumbuke raisi wa nchi ni binadamu kama wewe ila yeye anapigiwa saluti, na vizazi vyake vina urithi huenda kwa miaka mingi mbele.

Tofauti ni kuwa, wewe mlipa kodi wa kawaida unatakiwa uijenge nchi yako na katika kuijenga unatakiwa kuhakikisha umeacha mirija ya uchumi katika vizazi vyako vya mbele.

Hakuna mzazi atakayetaka mtoto wake azaliwe akute Taifa tuna mandege na matreni yaliyonunuliwa ndani ya awamu moja na raisi wake anasifiwa kwa kufanya hivyo ila yeye hana ardhi wala nyumba sababu baba yake alitumia uchumi wake kuijenga nchi.

Tuijenge nchi kwa kubeba kile ambacho mwili wetu unaweza kubeba katika wakati husika ili vizazi vyetu vitakapokuja vimsifu kiongozi wetu na viwabariki wazazi kwa kuwaandalia maisha mazuri.
Mkuu,
Siyo kwamba hatuna uwezo wa kupambana na matatizo yetu.

Magufuli ametuonesha kwa vitendo inawezekana kabisa kujenga nchi kwa kodi zetu wenyewe, na mikopo michache sana.

Ukumbuke pia hilo deni la karibu Trillion 30 linahusisha na madeni yaliyoiva ya nyuma ambayo amepambana sana kuyalipa.

Ametufundisha inawezekana kabisa kuendesha nchi vizuri bila misaada ya mabeberu na tukapata maendeleo.

Sote tu mashahidi wa hili, na namba hazidanganyi. Si dhambi kufanya kwa kasi kubwa kama uwezo upo.
 
Mkuu acha basi kutuona na sisi Wakinga huku ndani kama ndugu zako wa huko vijijini,yani hadi sisi humu unataka kutudanganya kuwa miradi ilijengwa na fedha za ndani??
Kwani hakuna Miradi iliyojengwa kwa fedha za ndani? Unafahamu kama kuna Miradi ilifanyika kwa kuahirishwa shughuli fulani za Serikali na pesa kupelekwa kwenye hiyo Miradi?
 
Leo 10:15pm 07/05/2022

Kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani Mwaka 2015,Tanzania ilikuwa katika uchumi wa chini,ukiwa katika uchumi wa chini kabisa,sera ya taifa na lengo linapaswa kuwa kuelekea uchumi wa kati wa ngazi ya chini,hii ni hatua moja kutoka katika uchumi wa chini,adhma na ndoto ya Rais John Pombe Magufuli ilikuwa kuipeleka Tanzania uchumi wa kati,Benki ya Dunia hutazama pato la taifa kwa mfano kupitia jumla ya utajiri wa rasilimali zetu zote,Ujenzi wa miundo mbinu itayokuja kuiingizia Taifa fedha za kigeni kutokana na shughuli mbalimbali zitakazotokana na miundo mbinu hiyo na utajiri wa kifedha kugawanya na idadi ya watu wa Tanzania,

Kwa calculation zake Rais Magufuli iliwezekana,ndoto ya Rais Magufuli ilikuwa ni kuingia Uchumi wa kati,sasa ataingia vipi,Mambo mawili akataka kuyatimiza ambayo ndio yatakuwa kichocheo cha kuiingiza Tanzania katika uchumi wa kati,Mambo hayo ni Umeme wa Uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere,Rufiji na Uchumi wa Viwanda,hivi viwili kwa calculation zake vingeweza kutufikisha kwenye kundi la Nchi zenye Uchumi wa Kipato cha Kati (MIC),kwa hakika aliwaza vyema na alitimiza ndoto hiyo,ili kufanikisha hilo Rais Magufuli alihimiza mambo yafuatayo,

•Ujenzi wa Viwanda nchini Tanzania,viwanda vinahitaji malighafi (kilimo, mifugo, uvuvi, madini, nk);.
• Ujenzi wa bwawa la Umeme la Rufiji litalozalisha megawatts 2,115 ikiwa sasa hivi tunatumia megawatts 1,500 Ili Sekta hizo zizalishe malighafi za kutosheleza mahitaji ya matumizi ya ndani tunahitaji Umeme wa uhakika kutoka Bwawa la Julius Nyerere kule Rufiji,viwanda, na mauzo ya nje ya nchi, lazima kuwepo miundo mbinu bora na imara (usafiri ardhini, majini na angani, maji, nishati).
• Kumudu uendeshaji na ukarabati (Operations & Maintenance) wa miundo mbinu hiyo, kunahitaji rasilimaliwatu wenye uwezo na ujuzi;
• Kupata rasilimaliwatu wa aina hiyo kunahitajika Uzalendo kwa Taifa la Tanzania,huduma bora za jamii (elimu na afya),hii kwa ujumla ilimfanya Rais Magufuli kuanza kuijenga upya Tanzania,laiti Mungu angempa maisha marefu basi watoto na wajukuu wetu wangefaidi matunda ya utekelezwaji wa ndoto za Rais Magufuli.

-Ndoto ya Rais Magufuli kuipeleka Tanzania uchumi wa kati iliwachukiza wazungu na vibaraka wao.

Nimeona nukuu kutoka kwa Wassira ikisema "Magufuli alisema hatuhitaji mikopo tunajenga kwa kutumia fedha zetu, Tanzania ni tajiri lakini yeye ndiye aliyekopa sana kuliko Marais wote,alikopa mikopo yenye riba kubwa kwa kificho kutekeleza ujenzi,deni la Taifa limepanda sana ndani ya miaka 6 ya Uongozi wake" sasa niulize swali, Serikali ya CCM ya Awamu ya tano,iliyoongozwa na Rais Magufuli,ambayo haikuwa na mahusiano mazuri na nchi zote za Ulaya iliwezaje kukopa kwa Serikali za Ulaya ambazo haina mahusiano nazo mazuri!?

-Vibaraka walivyokwenda Ulaya kuzuia mikopo isije Tanzania,kimbilio la Rais Magufuli likawa Benki ya Maendeleo ya Afrika,AFDB.

Benki ya Afrika ndio ilikuwa kimbilio la Rais Magufuli,na hata mtendaji wake Mkuu alifika Chato,kuhani msiba wa rafiki yake,AfDB wamekuwa wakitoa fedha kwenye sekta za maji, nishati na nyinginezo nchini Tanzania na wameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji wa Jiji la Arusha mara baada ya kutembelea Matenki ya Maji ya Themi Hills, Ofisi ya Kanda ya AUWSA-Moshono, Kituo cha kusukuma Maji Namba 4 na Tenki la Maji la Seedfarm lenye ujazo wa lita milioni 10 mkoani Arusha,sasa wanaojua madeni ya awamu ya tano watuambie alikopa kiasi gani hapo Benki ya Afrika? na hicho alichokikopa ndio hicho wanachotuambia kikubwa!?

Vyama vya upinzani nchini Tanzania na wanaharakati wa haki za binadamu hapa nchini Tanzania na wa kimataifa walikuwa wakiweka shinikizo la kutotolewa mikopo kwa Tanzania hadi pale Tanzania itakaporuhusu wanafunzi wanaopata ujauzito waruhusiwe kuendelea na mfumo rasmi wa elimu,kiongozi wa chama upinzani cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe aliwahi kusema kuwa Benki ya Dunia haitakiwi kuikopesha Tanzania dola milioni 500 za elimu kabla ya mabadiliko ya kisera kufanyika.Kwa mujibu wa nyaraka za Benki ya Dunia, pamoja na mambo mengine, mkopo huu ulikusudiwa kwenda kusaidia upatikanaji wa elimu bora na kwa urahisi kwa wanafunzi waliokuwa wanarudi shule baada ya kuwa wamepata ujauzito. Lakini mradi huu wa elimu ulikuwa ni kupitia elimu mbadala na si katika mfumo rasmi.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Akinumwi Adesina,alifika mara kwa mara nchini Tanzania na alimpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa aliyokuwaanaifanya kuimarisha uchumi wa Tanzania na alijadiliana mambo kadhaa na Rais Magufuli yakiwemo namna benki hiyo ilivyosaidia juhudi za maendeleo za Tanzania tangu mwaka 1971 na inavyoendelea kusaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo,nikimnukuu katika moja ya mahojiano yake alisema
"Yote kwa yote nimemhakikishia Rais Magufuli kuwa AfDB itamuunga mkono katika mipango yake na maono yake ili tuweze kuisaidia Tanzania kukua zaidi, nimefurahi kuzungumza na Mhe. Rais na naona Tanzania ipo katika njia sahihi," alisema Dkt Adesina kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ikulu wakati wa Awamu ya tano,AfDB ilifadhili miradi ya maendeleo yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 3.457 (sawa na Shilingi Trilioni 7.78 Tanzania) zikiwemo fedha za miradi 25 zilizotolewa kuanzia mwezi Novemba, 2017 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.986 (Shilingi Trilioni 4.47 Kitanzania).

Nimalizie kwa kuishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) kwa kutoa mikopo kwa Serikali ya Tanzania kusaidia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyobuni ajira kwa Watanzania wengi na iliyotarajiwa kubuni ajira nyingi kwa Watanzania mara tu Bwawa la Julius Nyerere,Rufiji litakapoisha,ilitarajiwa tani zaidi ya laki tano za mpunga na mazao mengine kuzalishwa pembeni ya Bwawa la Umeme la Julius Nyerere pale Rufiji na tungeweza kuuza mchele (export) nje ya nchi na kuliingizia Taifa fedha za kigeni na hivyo kukuza thamani ya shilingi ya Tanzania,hivi ni kati ya vitu ambavyo viliivutia Benki ya dunia kuitangaza Tanzania kama taifa lenye kipato cha kati mnamo mwezi Julai 2020.

Mbali na uongozi thabiti wa rais Magufuli katika kudhibiti matumizi ya fedha na kukabiliana na ufujaji wake,taifa la Tanzania lilitarajiwa kuimarika kiviwanda hali ya kwamba lina karibia viwanda 60 tangu lilipojipatia Uhuru, huku uongozi wa rais Magufuli ukifanikiwa kuanzisha zaidi ya viwanda elfu nane katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake,hivi sasa nchini Tanzania tunaunganisha matinga humu nchini,tunaunganisha mabasi na kuzalisha nondo ,mabati na kadhalika,kufikia tar 01/07/2020 siku ya Jumatano,Benki ya Dunia,iliiorodhesha Tanzania katika orodha ya nchi za uchumi wa kipato cha kati,kabla ya lengo ya dira ya Taifa kuiingiza Tanzania katika uchumi wa kati mwaka 2025.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Hoja nzito sana!

Magufuli hajawahi kwenda kubembea Dubai ila huyu mmh!
 
Hata kama ni biashara bado mahusiano mazuri kati ya wanaofanya biashara ni muhimu.

Hivyo hiyo hoja inakosa nguvu.

Uzuri wake ni kuwa alikua anafanya mambo ambayo yanatunufaisha wote na yanaonekana na wote.

Sio sasa hivi tunachukua fedha nyingi kwa mambo yasiyokuwa na tija.

Mfano fedha za uviko tulilazimishwa kuchukua zikaishia kwenye vyoo.
Unakuta choo kimeandikwa: kwa hisani ya msaada wa fedha za oviko 19..hahahaaaa
 
Back
Top Bottom