Hayati Magufuli aliwezaje kukopa kwa Wazungu ikiwa aliharibu uhusiano na nchi za Ulaya?

mikopo ya kibiashara SWISS CREDIT walishawahi chukua mkopo wa usd milion 500 ndani ya muda mfupi walipe usd milllions 900
 
Mikopo ya biashara au benki binafsi hata Putin akitaka Kukopa Marekani atapewa maana ina riba kubwa na mda mfupi wa marejesho..

Ila concessional loans hupewi na Wala ile mikopo yenye sura ya msaada kama wa covid hupewi
Magufuli hakutaka mikopo ya kudhalikisha utu wetu( h
Kuwatambua mashoga nk,) full stop
 
Huo muda ulitumia kuandaa huu utopolo ungetumia kutafiti kidogo tu ungeona

 
Reactions: Qwy
Mkuu sang'udi, Kama uwezo upo ni sahihi kabisa, na sina tatizo kupata kiongozi mwenye uthubutu wa kiwango hicho na kwa hilo 👏👏👍👍 kwa JPM(RIP)

Nitaandika kwa urefu ila tafadhali kama hutojali soma ili uelewe hoja yangu.

Pamoja na hayo aliyofanya, biashara hazikupaswa zifungwe, account za wafanyabiashara hazikupaswa zifungwe, mishahara kwa kiasi fulani ilipaswa iongezwe, huduma za uuzaji mazao hazikupaswa kuondolewa kwa wafanya biashara na kufanya ni state business na mengine mengi.

Nasema hivi kwasababu hivi ndivyo vitu vinavyomwezesha raia wa kawaida kufanya maendeleo binafsi na kurithisha vizazi vya mbele wakati yeye akiendelea kupokea pension ya uraisi na kushuhudia vizazi vyake vikifurahia urithi alioacha na akiendelea kupokea sifa za treni na ndege alizoacha.

NITAKUPA MFANO HAI WA MAMBO YALIYOTOKEA CHINI YA SERIKALI YA JPM:

Wote tunajua sheria zetu wakati mwingine huwa zinakuwa na mapungufu ya kuzitekeleza, mfano sheria za kuwataka wenye kampuni za consultancy wajisajili na VAT na waandae mahesabu bila kujali uwezo wa mtaji.

Kama mtu ana kakampuni kake ka sheria, kameajiri watu 5, sheria inamtaka aandae mahesabu kila mwaka na ajiunge VAT. Gharama ya kuandaa mahesabu si chini ya Tsh 500,000 mpaka 1,000,000 nje ya gharama za uhasibu, gharama ya kufile VAT si chini ya 50,000 mpaka 100,000 kila mwezi.

Sasa huyu mwenye kakampuni hakuwa akifile hesabu za mwisho kwa kutokujua au kwa kupuuza kwa sababu ya gharama za ukaguzi na uhasibu, na akawa anaenda kufanya makadirio kila mwaka kisha analipa kodi anaendelea na biashara kama presumptive tax payers wanavyofanya ilihali yeye ni corporate.

Sasa serikali kwa sababu ina marejesho ya mkopo wa reli ikatumia sheria ya kutokupeleka hesabu TRA ya adhabu ya Tsh 225,000 kila mwezi, na ikatumia sheria ya kutoa assessment kukadiria kodi ambayo huenda ingepatikana kwa kufanya examination of books of accounts.

Ikachukua % ya turnover ya miaka 5 ikaiita profit ikacharge penalty na interest kila mwezi ikapata makisio ya kodi ikajumlisha na zile 225,000 kila mwezi za miaka 5 na kumtaka mfanya biashara alipe plus interest each month for 5 years na kuzuia akaunti yake ya biashara huenda yenye pesa za wateja ikimlazimisha kodi ilipwe, mfanyabiashara akashindwa, biashara ikafungwa. Ukumbuke kwa huo mfumo uliotumika inaweza kuja hata kodi ya M40-M50, pesa ambayo mfanya biashara huyo hajawahi kuota kuishika kwa pamoja.

Kisheria raisi alikuwa sahihi na atakuwa alipata rejesho, ila katika uhalisia aliwanyima raia wake haki ya kufanya maendeleo binafsi kwa kuchukua mishahara yao huenda ya miaka 10 mbele ambayo wangelipwa kama angetumia busara na hako kakampuni kakaendelea kuwepo.

Sawa atapeleka rejesho ila, wale watu 5 ambao mshahara wao ameuchukua? Watoto wao mbeleni itakuwa vipi watakapokuta baba zao walilipia treni ila hawana pa kulala?

Sasa ukute baba anahako kakampuni na mama ni mwajiriwa kwenye kahoteli kalikokuwa kanategemea vikao vya wafanyakazi wa serikali vilivyopigwa marafuku kufanyika kwenye mahoteli hako kahoteli kakafungwa huku mzee wao akiwa anacheti cha darasa la saba akaondolewa kazini akiwa na miaka 57.
 
"Mabeberu" watu wanao kimbilia ili neno wana nia moja tu, kulinda legacy. Kote ume ongea point ila umeharibu vyote kwa hapo
 
Magufuli alikuwa anakopa zaidi pesa kutoka benki za kibiashara ambapo riba huwa kubwa na huko hawana tatizo na mkopaji, maana ni suala la kibiashara na sio kisiasa.
Bank gani ambayo Inakopesha bila riba
 
Sasa si ndio wanakukopesha vizuri, tena kibiashara, ukiwakorofisha haupati mikopo ya bila riba, wapate kukumiliki vizuri.

Hujaona Magufuli alibana kwenye dhahabu mwishowe mwenyewe akaachia. Unafikiri kwanini?

H
 
Magufuli tutamkumbuka
Bwawa la umeme
Rel tren ya mwendokasi
Ikulu dodoma
Stand kuu kila mkoa
Masoko kila mkoa
Hospital kubwa kila mkoa
Fryover ubungo na tazara
Fryover zingine 4 zinajengwa
Idara za maji ziko vizuri

Naasingeuliwa vyote hivyo vingesha kamilika na angetuletea manufaa mengine

R.I.P JPM
 
Ninakupata sana mkuu.

Biashara hazijaanza kufungwa wakati wa JPM pekee, hata sasa kuna biashara nyingi tu zinafungwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo makadirio yasiyokuwa ya busara kwa walipa kodi.

Ninafikiri tatizo halikuwa kwa Magufuli zaidi ila watendaji wake, japo anawajibika kama mkuu wa taasisi. Hata hivyo ni wakati huu tulishuhudia TRA ikifanya kazi iliyotukuka na yenye manufaa kwa taifa arguably kuliko wakati wowote ule.

Ninakubali, kunapokuwa na overhaul ya taasisi ya ukubwa huo kuna baadhi ya watu wanakuwa vulnerable kuathirika kwa irregularities zinazojitokeza.

Ninafikiri hizi zinabaki kama changamoto ambazo pengine hakuzi-address ipasavyo hasa kwa kuwa na ile attitude ya wafanyabiashara hukwepa kodi.

Kuhusu vyeti vya kughushi ninaamini alifanya kazi nzuri sana. Hatuwezi kuwa taifa lenye "watalaamu" wasiokidhi vigezo. Hawa walikuwa moja ya sababu za kuwa na malfunctioning institutions nyingi ambazo hazikuwa na afya kwa taifa letu.

Ninafikiri hizi ni gaps ambazo wenzake wanapaswa kuzi-address.
 
Reactions: Tsh
Hapa tulipofikia inatosha kukubaliana na kushikana mikono. 🤝
 
Unamaanisha mrusi anaweza kumkopa mmarekani katika Hali ya sasa? Au Ukraine akamkopa urusi?
Hivi unajuwa kuwa USA walitaka kununua mafuta Venezuela mwezi Machi kwa Nicholas Maduro?
 
HISTORIA KIDOGO:

Kabla halijazuka shinikizo la kumtaka ajiuzulu mwaka 2011, aliyekuwa Waziri mkuu wa Italy - Silvio Berlusconi aliwahi kumtusi aliyekuwa 'Chancellor' wa Ujerumani kipindi hicho, Bibi Angela Merkel (Tusi linahusu makalio ya bibi Angela). Likatokea anguko la kiuchumi, ambapo hali ya Italy ikawa mbaya kiasi cha kuhitaji msaada - na taifa ambalo lilikuwa linatazamwa sana kuweza kuiokoa Italy ni Ujerumani. Wakati huo Silvio alikuwa hana mahusiano mazuri na Angela, walikuwa hawawezi kutazamana uso kwa uso; lakini ilipofika wakati wa Ujerumani kuisaidia Italy - Angela hakusita kwenda kuonana na Silvio akiongoza jopo la akina Sarkozy na wengineo; na bila shaka wakampa Silvio ofa ya Mkopo.

Lakini, nyuma ya huo mkopo kulikuwa na agenda ya siri - ambayo ilikuwa ni kumg'oa Silvio madarakani! Wenyewe wanasema ilikuwa ni "The kiss of death" kwa Silvio - kwasababu angekubali kupokea ule mkopo, ingekuwa ni kwisha habari yake, na angekataa kupokea mkopo pia - kwisha habari yake!! Kuna maelezo deep kidogo kwanini ilikuwa hivyo.

Pointi yangu ni kwamba, haya mataifa makubwa siku zote yanatanguliza maslahi na malengo yao kwanza. Kwahiyo, hata kama wewe ni adui yao, kama huo mkopo au msaada au makubaliano au chochote kile watakachokifanya kwako au kwa kushirikiana na wewe kinawasaidia wao kutimiza malengo yao... kwanini wasifanye?

"Keep your friends close and your enemies closer"
 
Naomba uniwie radhi kukuita goigoi wa kifikira... tumekuwa nchi huru more than 50 years lakini hatukuwahi kuja na mradi wenye kutoa suluhisho la kudumu la shida ya umeme.

Suluhisho la kudumu la usafiri wa anga kwa mfano leo kuna Royal Tour ya Mama Samia ili iweze ku mature usafiri wa anga utakuwa na mchango mkubwa sana.

Ili tuendeshe nchi kwa kutoa unafuu kwa raia, na ushindani wa soko lazima tuwe na low cost in production and distribution chain hapo bado tunaongelea usafiri wa kila aina kuanzia land, railway include SGR, usafiri wa njia za majini, barabara nk ambao ndio ilikuwa miradi ya kimkakati....

Kuanzisha viwanda ili kuongeza thamani ya malighafi zetu, kukuza kilimo ikiwemo uanzishaji wa kilimo cha mpunga pembezoni mwa mradi wa JNHPP ambapo kungepatikana ziada ya kuuza nje na ukiangalia miradi yote ya kimkakati mpaka sasa ikiweza kusimamiwa vyema itatuingizia fedha za kutosha... ikiwa ni pamojama kipata rejesho la mikopo nk. Itazalisha ajira na kupandisha pato la mmoja mmoja (GDP )
Ntaenda mpaka uanzishaji au ukuzaji wa Burigi kwa kufanya wild animal transfer kwa jamii ambazo hazikuwepo kwenye mazingira ya awali lakini mfanano wa mazingira na tabia nchi unafanana kwa wamwanya hamishiwa kuishi... mikopo hiyo hata kwa akili za kawaida unaona kabisa ilikuwa na uwezo wa kujilipa... maana mbali na kutatua changamoto za muda mrefu bado ilikuwa inaingiza fedha toka ndani na nje inazaa ajira.. hapo hatujagusa miradi mikubwa ya maji safi na maji taka.... hatujagusa miradi ya kiudhibiti kama mizani nk... swali ambalo ulitakiwa kujiuliza kabla je? tungeacha kipi na tufanye kipi ambacho sio kipaumbele.
 
Usichokijua ni kuwa ugomvi sio chanzo cha kunyimwa mkopo.

Mkopo unapewa sababu una masharti yanayokaa kwenye maandishi.

Wazungu hufanya kazi au mikataba yenye "interest " kwao bila kuangalia ugomvi.

US na China ni rivals ila iPhone iko designed China na inakua assembled California.

Ni biashara nyingi tu wanafanya hata US anazo bidhaa zake za kuuza China tu kwa Africa hamuwezi kumudu.

Hili linaenda sambamba na quality na geography ya eneo husika , nishawahi kuona bus za Yutong pale Haifa sio Yutong za aina hiyo zipo bongo.

Nchi nyingi zina ugomvi na Israel ila Haifa lipo eneo lina majengo ya KIA, Hyundai, Toyota , Nissan ,Suzuki , Ford na kadhalika.

Whites only work on interest basis.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…