Hayati Magufuli aliwezaje kutunyamazisha Watanzania milioni 60?

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Tangu nikiwa mdogo nilipenda kufuatilia visa vya viongozi waliotawala kwa mkono wa chuma kama vile Stalin, Mussolini, Lenin, Hitler, Suharto, Iddi Amin, Mobutu, Kagame, Bokassa na wengineo.

Nikawa najiuliza hawa wababe waliwezaje kuwanyamazisha wananchi wao kirahisi wasipate watu wa kuwapinga?

Hata nikadhani labda wananchi wao ni mazezeta.

Ila alichotufanya bwana yule nilikuja kuelewa somo kwa vitendo, nilipenda sana story za hawa wababe ila ghafla nilijikuta nabadili mtazamo wangu.

Kiukweli kabisa watanzania wote tuliufyata kasoro mtu mmoja tu Tundu Lissu nadhani kwa sababu alishaonja kuzimu labda akaona kumbe hakutishi kivile, tuliobaki tukubali tuliufyata mpaka wengine kufikia kumuita Mungu, nikikumbuka nacheka mwenyewe.
 
Familia ya Kim inawezaje kunyamazisha Korea yote?

Unadhani mababu walikuwa hawana akili hadi kuwabeba Waarabu kwenye mabega yao?

In fact ni rahisi Sana,kila sekta hasa vyombo vya Dola unaweka watu royal kwako na wawe wakatili, lazima watu waufyate..

Ila unaowaweka lazima uwalipe vizuri na baadhi ya dili haramu na upigaji unapotezea.

Pia unakuwa na vitengo vya propaganda kila sehemu ni nyimbo zako tuu,hata Nyerere ndivyo alikuwa.

Hapo lazima wote iwe hivi 👇

 
Kwani akina badluck walilipwa Bure na Leo wanaandaliwa Kinga ya kutoshiitakiwa🏃🏃🏃.
 
Sasa kuhusu picha za mababu zetu kuwabeba wakoloni niliwaza baada ya kugundua kuwa wale wakikuwa wakilipwa ujira,ile ilikuwa kazi ya heshima kama kumuendesha kiongozi kwa sasa,kuna marupurupu kwa madereva,wale walikuwa madereva tu tusiwalaumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…