Hayati Magufuli aliwezaje kutunyamazisha Watanzania milioni 60?

Hayati Magufuli aliwezaje kutunyamazisha Watanzania milioni 60?

Kasome katiba iliyopo ujue nguvu alizo nazo Rais wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ili ujue hizo nguvu zake... Rais wa JMT ana nguvu za kutisha mno.
 
Tangu nikiwa mdogo nilipenda kufuatilia visa vya viongozi waliotawala kwa mkono wa chuma kama vile Stalin, Mussolini, Lenin, Hitler, Suharto Iddi Amin na wengineo.

Nikawa najiuliza hawa wababe waliwezaje kuwanyamazisha wananchi wao kirahisi wasipate watu wa kuwapinga?

Hata nikadhani labda wananchi wao ni mazezeta.

Ila alichotufanya bwana yule nilikuja kuelewa somo kwa vitendo,nilipenda sana story za hawa wababe ila ghafla nilijikuta nabadili mtazamo wangu.

Kiukweli kabisa watanzania wote tuliufyata kasoro mtu mmoja tu Tundu Lissu nadhani kwa sababu alishaonja kuzimu labda akaona kumbe hakutishi kivile, tuliobaki tukubali tuliufyata mpaka wengine kufikia kumuita Mungu, nikikumbuka nacheka mwenyewe
Yeye mbona alinyamazishwa milele na Allah?
 
Wakati mwingine ubabe unahitajika saana pale unapokuwa Kiongozi

maana Kuna watu baadhi hawataki kubembelezwa ni mwendo wa amri tu
Leo hi kiutaniutani mafuta ya kula dumu limefika 100,000 bado sukari mwez wa ramadhani
Hapo sasa !! Akili zitakaa sawa tu !!!
 
Tangu nikiwa mdogo nilipenda kufuatilia visa vya viongozi waliotawala kwa mkono wa chuma kama vile Stalin, Mussolini, Lenin, Hitler, Suharto Iddi Amin na wengineo.

Nikawa najiuliza hawa wababe waliwezaje kuwanyamazisha wananchi wao kirahisi wasipate watu wa kuwapinga?

Hata nikadhani labda wananchi wao ni mazezeta.

Ila alichotufanya bwana yule nilikuja kuelewa somo kwa vitendo,nilipenda sana story za hawa wababe ila ghafla nilijikuta nabadili mtazamo wangu.

Kiukweli kabisa watanzania wote tuliufyata kasoro mtu mmoja tu Tundu Lissu nadhani kwa sababu alishaonja kuzimu labda akaona kumbe hakutishi kivile, tuliobaki tukubali tuliufyata mpaka wengine kufikia kumuita Mungu, nikikumbuka nacheka mwenyewe
Wajanja ni sisi kwa kuwa tulijua "Debe tupu haliachi kupiga kelele".

Sasa mtu anaumwa magonjwa yafuatayo; Kichaa, Kisukari, UKIMWI, Herpes Zoster huku akiwa kawekewa Pacemaker (Defibrillator) kumuongezea kasi ya mapigo ya moyo, kwa nini utumie nguvu kuhangaika naye?

Tukamuachia COVID-19 tu ndiyo apite naye, na COVID hakufanya makosa.

HATUKUMUOGOPA tulijuwa ni MBOVU
 
Leo nimemkumbuka nikaishia kucheka tu mwenyewe dah jamaa alituweza
Yaani ilikuaga simu ikiita, namba ngeni, roho inaenda kasi, na hamna kupokea[emoji134][emoji134]
Ukiwa barabarani gari isimame sambamba na wewe unaanza kujiandaa kuchomoka mbio,,,
[emoji86],Ishu ya terrible teen nusta iniponze, nikafunga domo langu chap[emoji23][emoji23]
 
Ridhiwani Kikwete aliwahi kuhojiwa na Millard Ayo kuhusu mzee wake JK alipokuwa madarakani na alikuwa anatukanwa na kuchorwa vibaya yeye alikuwa anaichukuliaje??

Riz alisema ukweli ni kwamba ilikuwa inamkera sana kiasi ya kwamba alienda kumhoji mzee wake kwa nini anawaacha watu wanamkejeli na kumdhalilisha namna Ile na kwa nini hawashughulikii?

Mzee Kikwete alimwambia kwamba laiti angejua madaraka na nguvu aliyonayo Rais na akiamua kuyatumia basi hakuna atakayekuwa salama hata kidogo. Alimaanisha kwamba ana nguvu kubwa sana yeye kama Rais Ila wacha tu watu wamdhihaki sababu mtu anayeweza kumshika sharubu Simba hakika hajui Simba anaweza kumfanya kitu gani ndani ya sekunde moja tu.

Sasa Magufuli alikuwa ana ambition kubwa ya kuongoza nchi kwa kupeleka mambo haraka na the way anavyotaka, alipokuja kugundua hayo madaraka na nguvu aliyonayo akatamani kuzitumia na akaona namna watu wanavyotetemeka akipita sehemu akatamani atumie hizo nguvu kupeleka Mambo yaende.

Akazima bunge, Mahakama, waandishi au vyombo vya habari, akafumua mfumo wa utumishi wa umma, Yani akavuruga kila anachotaka hii sasa ilitokana na kujua kwamba Rais anaweza kufanya chochote.

Kwa nguvu hiyohiyo akageuka kuabudiwa sababu walitaka wale pesa yake waligundua ili waweze kula lazima wamsifie na kumhonga cheo Cha Mungu, wengine Kama sheikh Alhad wa Dar alisema Magufuli ni zaidi ya Yesu na jamaa likawa linaenjoy sana vile vyeo.

Mwishowe akalewa ule ukuu akataka atukuzwe maana walishamzoesha kumtukuza Hadi makanisani, viongozi wa dini karibu wote walimtukuza na aliyejaribu kumkosoa aliipata kisawasawa. Na pale ndipo kila aliyemkosoa alikuwa anapotezwa maana aliona yeye hawezi kukosolewa na hakutaka kukosolewa maana alishalewa ushamba wa madaraka.

Utaona kile kikosi kilichoundwa na Makonda kikiwa na jukumu la kutesa na kuua wote waliompinga na kumkosoa Magufuli kilianzishwa kwa usiri sana na kutekelezwa ushenzi mkubwa mno.

Kwa namna Ile hakuna ambaye angeweza kujitetea mbele yake ndio maana hakuwa anasikiliza hoja ya mtu yeyote akija anataka yeye aongee na mtekeleze whether you like it or not.

Hii ndio ilipelekea Hadi akataka aongoze milele lakini Mungu wa Watanzania ni Mungu wa Kweli, mnamo tarehe 17/3/2021 historia ikaanza kuandikwa upya baada ya kumpatia kifo yule fedhuli.

Sasa ukiangalia history ya madikteta wote Kama Hitler, Stalin, Pinnochet akina Mobutu, Idd Amin, Bokasa nk walikuwa na style ya kutengeneza watu wanaowapraise na wale waliowapraise waliishi vizuri sana .

Hiyo ilikuwa lazima wawepo ili waweze kusurvive kiunafiki sababu Hawa madikteta walijua kabisa hawakubaliki na hawapendwi nje na ndani ya nchi zao. Na ndio maana wanafanana kila kitu mfano, hawakusafiri nje ya nchi zao hovyo, hawakuruhusu mtu aripoti mambo ya nchini kwao na waliruhusu ripoti zinazowasifia na kuonyesha mambo ni shwari sana, nk.

Magufuli was one hell of the dictator ukifuatilia tabia za madikteta.
Kuna kundi la wasukuma liliundwa kutoka vyombo vya ulinzi akawapa nguvu sana walikuwa informers.

Mm ni muathirika wa magufuli.

Nilishukuru Mungu kumuua haraka bila kuharibu pesa ya matibabu kujitibu.

Tushukuru mungu.
 
Ahaaaaaa
 
Back
Top Bottom