Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji120]Ukweli ni kwamba, JPM alikuwa CHUMA.
Kwa hivi karibuni sidhani kama kutakuwa na wa kulingana naye.
Yawezekana wakatokea watu wenye chuki binafsi na JPM, lakini ukweli utabaki pale pale kwamba, JPM alikuwa ni KIBOKO kweli kweli.
Mjomba Magu,tumuache apambane na hali yake huko ahera.Habari za wakati huu, ni matumaini yangu wote ni wazima wa Afya na mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa letu pendwa Tanzania.
Tukirejea kwenye mada, aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Magufuli alikuwa ni kiongozi wa namna yake na kwa wakati muafaka ambao amekaa madarakani amefanya vitu vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vimeleta mageuzi na mabadiliko makubwa kiuwajibikaji, kiuchumi na kijamii na kuwa chachu kubwa kwa ustawi wa kimaendeleo wa Taifa la Tanzania.
Hakika hakuna asie na makosa, nami nakiri kuna mahali ambako aliyumba lakini bado haiondoi uhalisia na ukweli kuwa alifanya hivyo kwa dhamira kuu ya kutetea na kupigania maslahi mapana ya Taifa letu sema kuna sehemu matokeo hayakuwa chanya japo lengo lake lilikuwa jema.
Tukijaribu kuweka katika mizani yale Mazuri na mabaya, kwa hakika mazuri ni mengi sana na mfumo wa utawala wake umejenga msingi imara kwa viongozi wengi waliopo sasa na watakaokuja baadae.
Inawezekana sio wote, ila wengi wetu ni mashahidi na tumeshuhudia mageuzi makubwa kwenye kuleta mabadiliko ya uwajibikaji serikalini, kuzuia rushwa na udanganyifu, Mfumo usio na upendeleo katika kutoa ajira, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yenye kuleta tija kiuchumi kama Bwawa la Nyerere na Reli ya SGR, Umeme vijijini, Uboreshaji wa huduma za Afya, Ongezeko la ukusanywaji wa kodi, uboreshaji wa mikataba ya madini na gesi na vinginevyo vingi ambayo vimefanikisha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati wa chini mapema tofauti na ilivyotarajiwa.
Kwa hakika umefika wakati wa Hayati John Magufuli kupewa Heshima ya Baba wa pili wa Taifa la Tanzania, baada ya waasisi wa Taifa na Muungano ili kuyaenzi daima yale mema yote aliyoyafanya kwa maslahi mapana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na hatotukuwa nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani hata Korea Kaskazini wana Baba wawili wa Taifa, ila yote kwa yote neno langu sio Sheria, ni mawazo yangu tu, hivyo nawasilisha.