Hayati Magufuli anapotajwa kuwa Shujaa wa Afrika, maana yake nini?

Hayati Magufuli anapotajwa kuwa Shujaa wa Afrika, maana yake nini?

Tbc kazi yao ni kusifia tu sifa za kijinga Marehemu alipewa sifa kila secunde kuliko Mola wao me mwenyewe nilistuka Maana Katika Mashujaa wa Africa hana hata chembe moja ya kupewa sifa hiyo... Tbc kuna michumia Tumbo mule... wanadhani ukiwa raisi tu unakuwa Shujaa wa Africa so na Mwinyi nae ni Shujaa wa Africa? ???? And Kikwete pia????? Mashujaa walishaisha Marehemu nchi inapata uhuru kutoka kwa Mashujaa wa Africa alikuwa na miaka miwili
Ili uwe shujaa unatakiwa uwe na sifa gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulia wewe

Nakuona umekuwa mushauri siku hizi.. endelea bali si kuandika porojo na kulalamika kila sekunde.. viongozi wenu hawajambo!!! Posho wanazikumbuka na wanalia au wanafanya biashara siku hizi?..
 
Wasalaam wajumbe.

Nimesoma na kusikia katika vyombo vya habari kwamba Magufuli Pombe katika kipindi chake alikuwa shujaa wa Afrika.

Hii inasemwa sana, mwanzo nilijua ni kupitiwa tu, bahati mbaya. Kumbe wana habari wapo serious kabisa. Nahitaji kujua machache kuhusu Magufuli kutajwa kama shujaa wa Afrika.

Mchakato uliofanyika kumpata na kumtangaza kama shujaa wa Afrika.

Afrika ipo chini ya Umoja wa Afrika AU ambapo tunaona waliowahi kutajwa kama mashujaa waliwahi kufanya kitu katika umoja huo. Mfano mzuri ni Mwl. Nyerere na Nelson Mandela. Ambao maono yao waliyasema na kuhamasisha katika mikutano ya Umoja wa Afrika.

Katika utaratibu huo, ni wapi na lini Rais Magufuli aliwahi kuhutubia mkutano wa AU na kutoa maono yake?

Moja ya kigezo cha mashujaa ni kuunganisha jamii na kuheshimu utu. Katika kampeni za uchaguzi Magufuli alikuwa akitamka wazi kuwa hakupeleka na hatapeleka maendeleo kwenye majimbo ya Chadema. Hapo vipi wandugu.

Ni hoja tu tusijenge chuki.
Ni waimba mapambio na washangiliaji ndio wamebuni neno hilo bila kutafakari maana na uzito wake, mwendazake amefika makao makuu ya AU mara moja tu, na hakuna jingine lolote aliloifanyia afrika isipokuwa kuichonganisha na mataifa ya magharibi, wote sasa tunajua waziri wetu mpya wa nje kapewa kazi ngumu ya kurejesha mahusiano yetu na nchi za.nje ikiwemo Kenya, Rwanda ni, kwa kifupi tumenuka sana huko nje, na shujaa wa Afrika hakustahili kufanya hivyo hata kidogo.
 
Back
Top Bottom