Hayati Magufuli anapotajwa kuwa Shujaa wa Afrika, maana yake nini?

Hayati Magufuli anapotajwa kuwa Shujaa wa Afrika, maana yake nini?

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Wasalaam wajumbe.

Nimesoma na kusikia katika vyombo vya habari kwamba Magufuli Pombe katika kipindi chake alikuwa shujaa wa Afrika.

Hii inasemwa sana, mwanzo nilijua ni kupitiwa tu, bahati mbaya. Kumbe wana habari wapo serious kabisa. Nahitaji kujua machache kuhusu Magufuli kutajwa kama shujaa wa Afrika.

Mchakato uliofanyika kumpata na kumtangaza kama shujaa wa Afrika.

Afrika ipo chini ya Umoja wa Afrika AU ambapo tunaona waliowahi kutajwa kama mashujaa waliwahi kufanya kitu katika umoja huo. Mfano mzuri ni Mwl. Nyerere na Nelson Mandela. Ambao maono yao waliyasema na kuhamasisha katika mikutano ya Umoja wa Afrika.

Katika utaratibu huo, ni wapi na lini Rais Magufuli aliwahi kuhutubia mkutano wa AU na kutoa maono yake?

Moja ya kigezo cha mashujaa ni kuunganisha jamii na kuheshimu utu. Katika kampeni za uchaguzi Magufuli alikuwa akitamka wazi kuwa hakupeleka na hatapeleka maendeleo kwenye majimbo ya Chadema. Hapo vipi wandugu.

Ni hoja tu tusijenge chuki.
 
Tbc kazi yao ni kusifia tu sifa za kijinga Marehemu alipewa sifa kila secunde kuliko Mola wao me mwenyewe nilistuka Maana Katika Mashujaa wa Africa hana hata chembe moja ya kupewa sifa hiyo... Tbc kuna michumia Tumbo mule... wanadhani ukiwa raisi tu unakuwa Shujaa wa Africa so na Mwinyi nae ni Shujaa wa Africa? ???? And Kikwete pia????? Mashujaa walishaisha Marehemu nchi inapata uhuru kutoka kwa Mashujaa wa Africa alikuwa na miaka miwili
 
Ujinga ni kupenda kuufata!!


Viongozi hukumbukwa zaidi kwa itikadi na mitazamo yao, na zaidi walivyoishi na wananchi wao. Si kwa vitu walivyojenga.
Ndio maana ifikapo Oktoba 14 hatuambiwi Nyerere alijenga TAZARA, UDSM, VIWANDA, wala Mabwawa ya umeme. Tunasikilizishwa tu hotuba za zake na wosia wake.
 
Za kuambiwa changanya na zako

Hao ukiwasikiliza sana utapoteza muda wako

Wanaongelea mambo ambayo hawayafahamu, Nyerere na hata Nelson Mandela hawana title hiyo kuwa ni Mashujaa wa Africa

Mashujaa wa Africa ni wananchi na wapiganaji waliomwaga damu kwa mataifa ya nchi zao na kuna vikao inabidi viwatangaze

Sasa Tanzania hiyo mamlaka sijui wametoa wapi?

Ben Mkapa alijenga taasisi imara kama Pccb, TRA, Tanroads na hakuitwa shujaa wa Tanzania au Africa

Ben Mkapa alifanya mageuzi makubwa kiuchumi
 
Kuna propaganda ya chini kwa chini inaendelea kipindi hiki ili kuonyesha kuwa alikuwa anakubalika na wengi.

From the way msiba umekuwa "promoted" and even trying to influence the masses kwa njia mbali mbali.
uko sahihi
Propaganda kubwa inatumika "kuuza" msiba huu
Na kama unavyojua raia wa chini wasio na elimu ya kutosha huwa ni wahanga wa kwanza wa propaganda, hasa zile ambazo ni State Engineered Propaganda
 
Ujinga ni kupenda kuufata!!


Viongozi hukumbukwa zaidi kwa itikadi na mitazamo yao, na zaidi walivyoishi na wananchi wao. Si kwa vitu walivyojenga.
Ndio maana ifikapo Oktoba 14 hatuambiwi Nyerere alijenga TAZARA, UDSM, VIWANDA, wala Mabwawa ya umeme. Tunasikilizishwa tu hotuba za zake na wosia wake.
umeandika point kubwa sana mzee
 
Shujaa wa Africa wa Kuchoma moto na kuteketeza Vifaranga vya kuku wa Nchi jirani za Africa na Shujaa wa Africa wa Kunyang'anya Ng'ombe za Waafrica wenzake nchi jirani waliovuka mpaka kwa wafugaji ambao kiasili hulisha mifugo yao maeneo yote yanayowazunguka hadi wazungu walipokuja kuweka mipaka...
 
Wasalaam wajumbe.

Nimesoma na kusikia katika vyombo vya habari kwamba Magufuli Pombe katika kipindi chake alikuwa shujaa wa Afrika.

Hii inasemwa sana, mwanzo nilijua ni kupitiwa tu, bahati mbaya. Kumbe wana habari wapo serious kabisa. Nahitaji kujua machache kuhusu Magufuli kutajwa kama shujaa wa Afrika.

Mchakato uliofanyika kumpata na kumtangaza kama shujaa wa Afrika.

Afrika ipo chini ya Umoja wa Afrika AU ambapo tunaona waliowahi kutajwa kama mashujaa waliwahi kufanya kitu katika umoja huo. Mfano mzuri ni Mwl. Nyerere na Nelson Mandela. Ambao maono yao waliyasema na kuhamasisha katika mikutano ya Umoja wa Afrika.

Katika utaratibu huo, ni wapi na lini Rais Magufuli aliwahi kuhutubia mkutano wa AU na kutoa maono yake?

Ni hoja tu tusijenge chuki.
Mkuu, na hii pia inakuuma?
 
Back
Top Bottom