Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

Hayati Magufuli anashambuliwa kila kona. Siyo kesi, ila mambo yaende; yasipoenda wananchi watawazomea kila kona

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Spidi aliyokuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ni challenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani kuifikia baada ya kifo chake

Matarajio ya wananchi ni kuwa spidi itakuwa kubwa kuliko ile au itabaki ile ile.

Sasa hivi Marehemu anapondwa sana kuwa ohh alikuwa dikteta mara ohh alikuwa fisadi mara ohh staili yake haifai

Hakuna shida; cha msingi wananchi wanataka mambo yaende. Tukaneni matusi yote ila mwisho wa siku wananchi watalinganisha output yenu watukanaji na ya Magufuli kwenye kugusa maisha ya wananchi wanyonge

Marehemu Magufuli kila kona anakuwa attacked siyo kesi ila mambo yaende yasipoenda wananchi watawazomea kila kona Kila mtakakopita wadhalilisha Magufuli. Mtazomewa na kuambiwa Magufuli angekuwa hai hili lingefanyika na watawazomea.
 
Tulikuwa tukisema Magufuli anasifiwa na wananchi wasiojua lolote, ama wale waliokuwa wanafaidika na madaraka yake. Kwa wananchi wenye uelewa wa mambo tunajua ni kwa kiwango gani Magufuli ameiweka nchi hii kwenye wakati mgumu, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Namfananisha Magufuli na mwizi aliyejenga nyumba nyingi kwa fedha za wizi, ila baada ya kufariki madhambi yake yote kuwa hadharani na mali hizo kupotea.
 
He is not being attacked,mfalme amevuliwa nguo,wananchi wamefunguliwa masikio na macho yao waweze kuona na kusikia yaliyokuwa nyuma ya pazia.

Mzee Magufuli alibana uhuru wa media kuripoti habari za uchunguzi,uhuru wa watu kujadilia mada hasi za utendaji wa wake na serikali yake. Mzee amekufa na suddenly tumepata uhuru wa kusikia kuona na kujadili taka ambazo zilifunikwa na sheria kandamizi za habari.
 
Ametuachia deni la Trillioni 18 katika kipindi chake cha miaka 5 tu. Hili pia linapaswa lilipwe.
Hajaacha deni tu acha uongo.kaacha vitu vilivyotumia hiyo pesa pia.Eti kaacha deni utafikiri hizo pesa alikopa akaenda kuweka pesa kwenye akaunti yake uswisi.

Lugha ya ki layman utafikiri mtu hata shule hukwenda. Hiyo miradi kila mkoa na wilaya huioni au ? Elimu bure huioni au ? umeme kila kijiji huuoni au? barabara kila kona huoni au? vituo vya afya kote nchini huoni au nk

Kipindi chake nchi ilikuwa inakopesheka na madeni yalikuwa yanalipika bila shida.Wakopeshaji walituamini

Twende sasa ni challenge kwa serikali iliyopo itamudu kukopesheka na kulipa madeni na kuendesha miradi nchi nzima kama Magufuli alivyomudu? muda ni mwalimu mzui.let us wait and see tuone matusi kwa Magufuli kama yana mantiki
 
Utawala mpya unapaswa kupambana kuliondoa tabaka aliloliacha linakuwa kwa kasi la wanyonge kulitoa katika unyonge na kulipa maisha bora, hilo ndilo tabaka lake lililompenda sana
Hakuna utawala mpya wala wa zamani wote wapiga madili tu. Tena utawala huu wa awamu ya sita, ndio utakuwa kama ule wa mzee ruksa shamba la bibi.
 
Mama ana roho ya ubinadamu,mambo mengi maovu yaliyofanyika chini ya mwendazake yanafichuka,kutokana na ripoti ya CAG.
Mwendazake alikuwa anapambana kuwamaliza wapinzani,wawekezaji huku kukiwa na mianya lukuki ya upotevu wa fedha za umma
 
Yuko mtu anadanganywa na kadanganyika. Anafikiri hii nchi ikikwama watakao jibu ni wanao mdanganya. Kumbe watakuwa pembeni wakicheka na kutabasamu.

Hajui kwamba kajichafua na kuchafua anaofanya nao kazi. Sijui kazi atafanya na nani sasa? Unachafua mpaka Jeshi na vyombo vya Usalama kuwa havi kufanya kazi yake kikamilifu wakati ndio mbereko inayo kubeba kila uchao.
 
He is not being attacked,mfalme amevuliwa nguo,wananchi wamefunguliwa masikio na macho yao waweze kuona na kusikia yaliyokuwa nyuma ya pazia. Mzee Magufuli alibana uhuru wa media kuripoti habari za uchunguzi,uhuru wa watu kujadilia mada hasi za utendaji wa wake na serikali yake. Mzee amekufa na suddenly tumepata uhuru wa kusikia kuona na kujadili taka ambazo zilifunikwa na sheria kandamizi za habari.
Kwanini msubiri mpaka amekufa?. Anzeni kuwavua nguo awamu zote basi. Upuuzi mtupu.
 
Mbona yeye aliwa attack wastaafu alipoukwaa urais?

Kwanini yeye asishambuliwe kwa maovu aliyoyafanya?

Tena mtu kama magu watu watamu attack sana kwa sababu enzi za uhai wake alitumia mkono wa chuma kunyamazisha watu wasihoji wala kupinga chochote akifanyacho.

Ukijaribu risasi zinakuhusu!

Now hayupo acheni watu wajimwaemwae.
 
Unamlalamika CAG? Kama unamlalamikia yeye fahamu aliteuliwa na Mwendazake huenda angemuacha Assad tusengayasikia haya!
Yuko mtu anadanganywa na kadanganyika. Anafikiri hii nchi ikikwama watakao jibu ni wanao mdanganya. Kumbe watakuwa pembeni wakicheka na kutabasamu.

Hajui kwamba kajichafua nackuchafua anaofanya nao kazi. Sijui kazi atafanya na nani sasa? Unachafuacmpaka Jeshi na vyombo vya Usalama kuwa havi kufanyakazi yake kikamilifu wskati ndio mbereko inayo kubeba kila uchao.
 
Hajaacha deni tu acha uongo.kaacha vitu vilivyotumia hiyo pesa pia.Eti kaacha deni utafikiri hizo pesa alikopa akenda kuweka pesa kwenye akaunti yake uswisi.Hiyo miradi kila mkoa na wilaya huioni au ? Elimu bure huioni au ? umeme kila kijiji huuoni au? barabara kila kona huoni au? vituo vya afya kote nchini huoni au nk..
Sawa, lakini alituaminisha kabana mianya ya rushwa kweri kweri kumbe porojo
 
Spidi aliulypkuwa nayo Marehemu Magufuli ya kufanya mambo yaende na kufanyika kwa kasi inayoonekana wazi kwa kila mtu, ichallenge kwa waliopo iwe serikalini au bungeni au Mahakamani...
Sure...But history will speak by itself...Time is a good healer...Mungu amemwokoa Hayati na haya maana angesumbuliwa sana kama angetoka madarakani akaishi kama raia...God is so just, rest in peace baba...Some of us will continue with the course if not today tomorrow, if not me my descendants!
 
Tulikuwa tukisema Magufuli anasifiwa na wananchi wasiojua lolote,
Na hao ndio population kubwa ya Tanzania zaidi ya asilimia 80 na ndio wanyonge wenyewe waliompigia kura na ndio alijitahidi kuwapelekea miradi mingi na elimu bure nk

Ndio aliosimama nao.Lisu alisimama na wanaoielewa akaambulia kura milioni moja

Magufuli akasimama na wasiojielewa wenye elimu duni na uelewa duni na machinga na ma ntilie nk.

Nakubaliana na wewe alisimama na wengi wa chini hakusimama na wachaje wa juu au middle class
 
Unamlalamika CAG? Kama unamlalamikia yeye fahamu aliteuliwa na Mwendazake huenda angemuacha Assad tusengayasikia haya!

Huyu alifurushwa kutoka TRA anaweza akatumiwa vilevile. Sisi tuliona siku ya tatu baada ya maziko hii ripoti kupokelewa na ilikuwa Jumapili.

Wapambe nuksi wakaanza kumchafua mwenda zake kwamba ingekuwa ni yeye angekuwa kanisani akihutubia kutoka madhabahuni. Mungu akawa amewasahaulisha na wakasahau mwendazake ilikuwa ni zake pia kuapisha jumapili.

Mareheme siku ya tatu kaburini watu walianza kumpakaza hii oil chafu kama mafuta.
 
Back
Top Bottom