Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Pamoja na kupungukiwa subira hakika JPM alikuwa na tamaa ya dhati kabisa kuisaidia Nchi yetu iweze kufikia maendeleo ya kweli.
JPM hakuwa na subira ya hata chembe kitu ambacho kiliwaumiza na wasio husika.
Mfano mzuri ni suala la vyeti fake JPM alitakiwa angalau wale ambao walikuwa na uzoefu wa fani husika na walitumika/hudumu aghalabu zaidi ya muongo mmoja angewasamehe na wangetakiwa wapewe japo muda wa mpito ili waweze kujiendeleza kielimu kwa kuzingatia tasnia waliyokuwapo.
Pia suala la kuvunja nyumba za watu pale Kimara Hayati Magufuli alipaswa kutoa japo fidia kiasi bila kujali mambo ya sheria. Ni wazi JPM hakuwapenda wana kata ya Kimara kwa sababu ya itikadi zao za kisiasa lakini hakupaswa kuwahukumu kwa namna ile aliyoifanya.
Katika yote, JPM alikuwa Rais mzalendo wa kweli ndani ya Nchi yake!
Tuendelee kumsamehe Rais Magufuli na pia tuendelee kumuombea pumziko la milele.
RiP JPM!