Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Kwa ambao hatukubahatika kuuona uongozi wa Mwalimu Nyerere tukiwa na uelewa na ufahamu timamu tunajivunia kupata fursa ya kuuona, kuushuhudia na kuuelewa utawala wa Hayati Magufuli ambao kulingana na simulizi mbalimbali toka kwa wazee waliobahatika kufanya kazi na Mwalimu wanasema unafanana kwa mengi.
Kutoka kwa Hayati Magufuli tumeona ni kwa namna gani Mwalimu alipingwa katika sera zake za mabadiliko lakini tunachojivunia kwa wawili ni kwamba wana misimamo isiyoyumba na uzalendo usio tia shaka.
Wote wanaomsema Hayati Magufuli huku wakijua haoni wala hasikii wanajidhalilisha na kujiabisha wenyewe. Hayati Magufuli ni alama ya ukombozi halisi wa mwafrika kiuchumi katika karne hii ya 21.
Historia ya mabadiliko chini yake imeandikwa na ni historia isiyoweza kuja kufutika kirahisi na wote wanaobeza juhudi zake wanajaribu kufuta historia muhimu kwa vizazi vijavyo na hawatafanikiwa. Hayati Magufuli alikuja kwa kusudi maalumu , kutufumbua macho watanzania athari za kutokua huru kiuchumi ni sawa kabisa na kukosa Uhuru wa fikra na mawazo.