Hayati Magufuli bado anawanyima usingizi wapinzani wa Tanzania

Yes ni kweli ndani ya uongozi wa huyu jamaa wapinzani bado hawaamini kwa katiba gani na sheria ipi ilimpa mamlaka kuzuia shughuli za kisiasa zote, mikutano ya hadhara na hata wabunge kutokwenda kwenye majibo mengine kufanya kazi ya siasa. Mbali zaidi bado hawaamini namna jamaa alivyoharibu uchaguzi mkuu wa 2020, yaani kifupi pamoja na kutangulia mbele ya haki ila kaacha machungu na mambo ya ajabu makubwa mno nyuma yake. Yaani ni mengi jamaa aliasisi - manunuzi (Bulk procurement) ya viongozi wa upinzani, viongozi wa upinzani kujeruhiwa / kupotea nk yote haya yanabakia kwenye record yake.
 
Làbda anawanyima usingizi hao waliokuzaa, nobody else
 
JPM ni talk of the town....kila kona kuna kilio cha kumkumbuka JPM...hata ukimchukia vipi kuna namna lazima ukubali aliweza kuconnect na watu wa chini.. ndio maana bado wapinzani wanamuona ni kikwazo kwao
 
Karibu Tanzania upite kwenye mitaa usikie wananchi wanayoongea kila leo kuhusu JPM.... mtaani ni hero upende ama usipende.

Usifikiri wapinzani wanamuogopa mpaka leo for no reason, wanaipata feedback ya ukweli.

Anyways, pole najua kurudi bongo ni kitu ulishasahau...hauna maisha tena, hauna identity....upo kama kasha 🤔🙈🙈😂
 
JPM ni talk of the town....kila kona kuna kilio cha kumkumbuka JPM...hata ukimchukia vipi kuna namna lazima ukubali aliweza kuconnect na watu wa chini.. ndio maana bado wapinzani wanamuona ni kikwazo kwao
Ni jambo la kawaida kwa kila kiongozi unapokua madarakani lazm utakubalika mahala nakuna mahala hutokubalika... Hata wakati wa JPM Kuna watu weng tu waliona ni heri wakati wa JK, kumbuka nchi ya Tanzania haina watu wa hali ya Chini peke ake... Uwe Chini au juu maadam ww ni mtanzania unahaki ya kuneemeka na uongozi uliopo madarakani... Ni sahihi Kuna maeneo wanamkumbuka lakn kaa ukijua sio watu wote na pia vilevile Kuna wa Tz kibao wanaona afadhali wanaona samia ni bora kuliko JPM... Na ndo Maan ikaitwa nchi inawatu wengi so huwezi ukawa please wote JPM hakuwa Mungu... Kama nyerere baba wa Taifa alisemwa na kusimangwa who is magufuli
 
RIP THE BEST EVER PRESIDENT OF JMT, MUNGU ALIMTUMA KUFANYA KAZI MAALUM YA KUWEKA MIFANO KISHA AKAMUITA AKAMPE KAZI NYINGINE YA UTUKUFU MBINGUNI....
I miss my President soo much...
Kamfuate umbusu. Wewe itakuwa muuaji uliyetekeleza mauaji yote kwa amri yake
 
Stop nonsense, Hilo jitu limeua watu! Mengine ya kuona Mali naweza samehe, lkn siyo roho za watu.
 
Wakati mwingine msiwe mnaweka upumbavu wenu in public, Magufuli alikuwa muuaji katili asiye na huruma ndo maana Mungu alimchukua haraka ili kuinusuru Tanzania, nyie mnaomwambudu hamieni Chato kwenye kaburi lake labda atafufuka aje kuwaongoza
 
Historia imeandikwa kwa jitu katili , muuaji kuwahi kutawala Tanzania.
Azory Gwanda, Ben Saanane, maiti za kwenye sandarusi Coco Beach, MKIRU
Habari.

Kuna watu waliimba na kuhubiri,
Kusujudu na kurukaruka.
Kunywa bia na kuponda bata la kufa mtu kwamba kwa maisha yao yatakuwa bora mno baada ya Magufuli.

Leo ni miezi 8 bila Magufuli lakini kila wakigeuka huku hakuna umeme, wakigeuka hakuna maji ,wakigeuka huku mbolea lakini moja, wakigeuka huku wanafukuzwa kwenye migodi ,wakigeuka huku wanafukuzwa kwenye mitaa, wakigeuka huku Mungu wao yuko jela kwa ugaidi.

Leo ndiyo wamejua Magufuli alikuwa anafanya kwa ajili yao?
Jinga kabisa na bado mtaendelea kuwa watumwa hivyo hivyo.
Waliowadanganya wamtukane Magufuli wote wamepata mabwana Ulaya wanalishwa bure.

Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Stop nonsense, Hilo jitu limeua watu! Mengine ya kuona Mali naweza samehe, lkn siyo roho za watu.
Wewe ndo unapaswa kuacha upuuzi, Jamaa ni marehemu lakini bado unahangaika nae.
 
Huwa wanatokea wengi sana ila sio wote huwa wanafanikiwa kuyakwaa madaraka makubwa.
Tunahitaji katiba mpya.
Yaani duniani Mtu kama Magufuli hutokea mtu mmoja kwa karne moja!
 
Upinzani unapata shida sana mpaka sasa kupambana na legacy yake. Jpm ndio aliwapoteza upinzani kwa wananchi kwa kupiga kazi. Sasa hivi wako bize kumchafua ila wapi...
Kumbe kuwapoteza wapinzani kwa ukatili wa kuua na kubambika kesi nayo ni sifa?
 
Best president wa kuua na kubambika kesi?
 
Huwa wanatokea wengi sana ila sio wote huwa wanafanikiwa kuyakwaa madaraka makubwa.
Tunahitaji katiba mpya.
Naunga mkono hoja ile ya zamani imenyofolewa kipengele cha ukomo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…