Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mwaka 1996 wakati ajali kubwa ikitokea Ziwa Victoria mimi nilikuwa Ukraine nikiwa nimemaliza mwaka wa kwanza wa lugha nikijitayarisha kuingia mwaka wa masomo. Nakumbuka namna sisi watanzania tulivyoanzisha mjadala juu ya ajali hiyo iliyoua ndugu na jamaa zetu wengi.
Mwaka huu itatimia miaka 27 tangu msiba ule utokee. Huwa tunalo tatizo la kutoa takwimu halisi za vifo haswa kwa malengo ya kisiasa yenye nia ya kujaribu kupunguza hasira za walengwa wa moja kwa moja wa ajali (victims). Ni hulka iliyoendelea kuwepo kwa muda mrefu. Ukisika wamekufa watu 10,000 basi tambua ni zaidi ya 30,000 wamepoteza maisha.
Sina uhakika kama hayati JPM alipoteza ndugu zake wa karibu katika msiba ule mzito. Lakini kwa maamuzi ya kutoangalia watasema nini wale wakosoaji wa kila jambo akaamua kwa ushujaa kuanza kujenga meli kubwa ili itumike katika Ziwa Victoria. Ni maamuzi ya kijasiri sana na ya kizalendo.
Kuwa tayari huku mtaani watu walalamike vyuma vimekaza lakini serikali yake ikiwa inafanya kazi yenye kuacha kitu chenye kuonekana maishani mwetu (tangible).
Serikali ya JPM licha ya lawama na upungufu wa hapa na pale lakini iliweza kwa kiasi kikubwa kupambana kuacha vitu vyenye kuonekana na vyenye kuweza kupigiwa hesabu vimenunuliwa kwa pesa kiasi gani.
Manunuzi ya ndege mpya na ukarabati wa viwanja kadhaa, ujenzi wa daraja la Busisi na haya ya hapa Dar, na mambo mengi yenye kuonekana na hivyo kuchangia katika mzunguko wa pesa kiuchumi na kuinua kiwango cha maisha cha watu hao hao.
Vilio vya wote waliofiwa na ndugu zao pale ziwani tarehe 21 May 1996 angalau vimefutwa machozi na uwepo wa Meli yenye kuweza kubeba watu 2700 na tani 400 za bidhaa mbalimbali.
Wale watoto waliokuwa yatima kwa sababu ya ajali ile katili, angalau wanacho chombo cha kusafiria wakiwa na amani moyoni.
Wale wajane walioishi miaka 27 wakiwaombea misa maalum wenza wao kila siku makanisani wanacho chombo cha kusafiria chenye kulingana na uzito wa kodi wanayolipa kila wanaponunua chochote mahali popote.
JPM kwa hii meli ya Ziwa Victoria mimi kama mtu mwenye asili ya kanda ya ziwa nitakuenzi daima. Ulale mahali pema peponi.