Hayati Magufuli kama alikuwa anapambana na ufisadi, kwa nini asingefanya kama huyu shujaa?

Kuna njia nyingi za kumuua paka , sasa katika kuwa shughulikia fisadi au mafisadi kuna njia nyingi, mfano alivyo banwa Habinder Singh aliyetumika , wafaidikaji walifaidika na huo mradi, au unapenda kulopoka lopoka Tu, bila kujua njia za kuwa baini na kuwachukulia hatua, kulikuwa na issue ya Sio, Kitilya, na Nancy, walivyo banwa , je wanufaika waliokuwa serikali au Wana siasa walifaidika na hivyo vitu, , kuhusu Escrow, Ile ilichukuliwa lini, na fedha zake mgawanyo wake ulikuwaje, na unajua Magufuli amekaa miaka mingapi madarakani na aliondokaje, au ulitaka ajikite Tu Kwa mafisadi asishughulike na vitu vingine ambavyo Kwa muda mfupi tunaviona na sio kuhadithiwa. Na je unajua hizo za Escrow zilizotoka Stanbic zilitokaje na Nani wahusika na mrolongo wa kuzipata hizo pesa, na wakati huo huo kuna watu Wana kinga za kisheria.
Ume mzungumzia Rizwani, je yeye anakampuni ya kuweza kufisadi nchi ?? Au unazungumza tu, Kwa kuwa una Haki ya kuandika hapa. Au kuna mahali alipata tenda ya kujenga au kuleta bidhaa au kutoa huduma. Cha kuambia ongeza na akili zako.
 
Wafuasi wa Magufuli ndio mnataja serikali ya Kikwete na CCM imejaa mafisadi, sasa mbona Magufuli hakuweza kumfunga fisadi hata mmoja wa serikali ya Kikwete? Au kutoka hata CCM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…