Hayati Magufuli kama kuna mabaya yake tumwachie, mazuri yake twende nayo

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Posts
866
Reaction score
625
NIiwakumbushe tu kitu kimoja, ukiyabeza ya mwenzio ya kwako yatafanywa hivyo hiyo.

Nizungumzie kitu kidogo tu cha usafi wa mazingira yetu ambalo lilikuwa ni maono ya kwanza ya JPM alipoingia madarakani, na ikapitishwa siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi watu wote tufanye usafi wa maeneo yetu.

Suala hili limezikwa pamoja naye kwani lilikuwa na ubaya gani, mifuko ya plastiki iliyokuwa imeharamishwa sasa inaonekana kwa kasi, hivi tuna tatizo gani? je?

Tuamini kwamba Dr Rais Samia akimaliza kipindi chake tutaacha kupanda miti?

Tutarudi kwenye kutumia kuni?

Tujisahihishe hii tabia haina Afya kwa Nchi yetu.
 
Mtanikumbuka .......ni heri siku moja nikawe kiongozi wa malaika...
Muuaji na katili hawezi ongoza malaika!! Mfano kumfukuza CAG kisa kutaka kuchunguza manunuzi ya ndege ni haki? Kupora fedha za Bureau de Change ni haki?

JPM angeweza kuwa Rais bora wa dunia kama angeendelea na kazi zake bila kuingiza chuki zisizo na lazima. Mfano kwenda Bunda na kutishia wasipelekewe mradi wa maji kisa walichagua upinzani?! Ilikua na ulazima gani?
 
Nasubiri umalize nami niandike!
 
Sio yeye tu, hata kwenye ngazi ya familia mazuri ya mtu yaenziwe ila mabaya yake yasikumbukwe kabisa.
 
Uzuri gani mtu muuaji anaweza kufanya ili hatia yake ya uuaji imtoke?
NIiwakumbushe tu kitu kimoja, ukiyabeza ya mwenzio ya kwako yatafanywa hivyo hiyo.

Nizungumzie kitu kidogo tu cha usafi wa mazingira yetu ambalo lilikuwa ni maono ya kwanza ya JPM alipoingia madarakani, na ikapitishwa siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi watu wote tufanye usafi wa maeneo yetu.

Suala hili limezikwa pamoja naye kwani lilikuwa na ubaya gani, mifuko ya plastiki iliyokuwa imeharamishwa sasa inaonekana kwa kasi, hivi tuna tatizo gani? je?

Tuamini kwamba Dr Rais Samia akimaliza kipindi chake tutaacha kupanda miti?

Tutarudi kwenye kutumia kuni?

Tujisahihishe hii tabia haina Afya kwa Nchi yetu.
 
Muuaji na katili hawezi ongoza malaika!! Mfano kumfukuza CAG kisa kutaka kuchunguza manunuzi ya ndege ni haki? Kupora fedha za Bureau de Change ni haki?

JPM angeweza kuwa Rais bora wa dunia kama angeendelea na kazi zake bila kuingiza chuki zisizo na lazima. Mfano kwenda Bunda na kutishia wasipelekewe mradi wa maji kisa walichagua upinzani?! Ilikua na ulazima gani?
Alimuua mama yako?
 
Hata wewe unaweza ukamuelezea mazuri yake wakati mwengine bila kuongozwa na chuki kwake inayokufanya umuelezee kwa mabaya tu wakati wote kila anapotajwa Magufuli.
 
Alimuua mama yako?
Hao jamaa hutoweza kuwaelewa maana watakwambia kipindi cha Magufuli watu wengi walimuogopa hivyo hawakuwa wakimkosoa wala kumpinga ila hapo hapo watakwambia watu wengi waliuliwa kimya kimya kwa kumkosoa na kumpinga Magufuli.
 
Mawazo hakuuwawa? Saanane? Lissu hakupigwa risasi? Azory gwanda? Na JPM mwenyewe alimpa maagizo Ndugai kuwa awatimue bungeni ili wakitoka nje awashughulikie!! Alafu mnataka kumtetea huyi mkatili?

Mimi binafsi kata nayoishi kuna wafanyabiashara wakubwa wawili walikua ndio wanadhamini CHADEMA. Moja ana hardware kubwa sana mwingine ni mwanajeshi mstaafu, eeh bwana JPM alipoingia alihakikisha anawaharass biashara zao na kutishia kuzifunga. So mpaka inafika 2020 hata pesa ya kulipia kodi ya ofisi ilikua kipengele. Imagine hiyo ni kata moja? Je kwingine ilikuaje hali? Acheni kutetea ujinga.
 
NIiwakumbushe tu kitu kimoja, ukiyabeza ya mwenzio ya kwako yatafanywa hivyo hiyo.

Nizungumzie kitu kidogo tu cha usafi wa mazingira yetu ambalo lilikuwa ni maono ya kwanza ya JPM alipoingia madarakani, na ikapitishwa siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi watu wote tufanye usafi wa maeneo yetu.

Suala hili limezikwa pamoja naye kwani lilikuwa na ubaya gani, mifuko ya plastiki iliyokuwa imeharamishwa sasa inaonekana kwa kasi, hivi tuna tatizo gani? je?

Tuamini kwamba Dr Rais Samia akimaliza kipindi chake tutaacha kupanda miti?

Tutarudi kwenye kutumia kuni?

Tujisahihishe hii tabia haina Afya kwa Nchi yetu.
Hajawahi kuwa na mazuri
 
Muuaji na katili hawezi ongoza malaika!! Mfano kumfukuza CAG kisa kutaka kuchunguza manunuzi ya ndege ni haki? Kupora fedha za Bureau de Change ni haki?

JPM angeweza kuwa Rais bora wa dunia kama angeendelea na kazi zake bila kuingiza chuki zisizo na lazima. Mfano kwenda Bunda na kutishia wasipelekewe mradi wa maji kisa walichagua upinzani?! Ilikua na ulazima gani?
Hawezi kuwa mtu wa kukumbukwa kabisa
 
Back
Top Bottom