Hayati Magufuli kama kuna mabaya yake tumwachie, mazuri yake twende nayo

Hayati Magufuli kama kuna mabaya yake tumwachie, mazuri yake twende nayo

Hao jamaa hutoweza kuwaelewa maana watakwambia kipindi cha Magufuli watu wengi walimuogopa hivyo hawakuwa wakimkosoa wala kumpinga ila hapo hapo watakwambia watu wengi waliuliwa kimya kimya kwa kumkosoa na kumpinga Magufuli.
Hakubaliki na hatokubalika
 
Mawazo hakuuwawa? Saanane? Lissu hakupigwa risasi? Azory gwanda? Na JPM mwenyewe alimpa maagizo Ndugai kuwa awatimue bungeni ili wakitoka nje awashughulikie!! Alafu mnataka kumtetea huyi mkatili?

Mimi binafsi kata nayoishi kuna wafanyabiashara wakubwa wawili walikua ndio wanadhamini CHADEMA. Moja ana hardware kubwa sana mwingine ni mwanajeshi mstaafu, eeh bwana JPM alipoingia alihakikisha anawaharass biashara zao na kutishia kuzifunga. So mpaka inafika 2020 hata pesa ya kulipia kodi ya ofisi ilikua kipengele. Imagine hiyo ni kata moja? Je kwingine ilikuaje hali? Acheni kutetea ujinga.
Ubaya wa hali ya juu sana
 
Attachments

  • 20240523_124711.jpg
    20240523_124711.jpg
    260.9 KB · Views: 1
Kwa sisi tuliopo nje ya nchi hatukuona kiongozi bora kama magufuli...sifa zake na mambo yake makubwa tulikuwa tukiyaona ata uku marekani ....tukasema basi nchi yetu itafika pale inapotakiwa kufika lakini punde si punde mauti hayoooo..

Yote kwa yote magufuli alikuwa kiongozi bora
 
NIiwakumbushe tu kitu kimoja, ukiyabeza ya mwenzio ya kwako yatafanywa hivyo hiyo.

Nizungumzie kitu kidogo tu cha usafi wa mazingira yetu ambalo lilikuwa ni maono ya kwanza ya JPM alipoingia madarakani, na ikapitishwa siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi watu wote tufanye usafi wa maeneo yetu.

Suala hili limezikwa pamoja naye kwani lilikuwa na ubaya gani, mifuko ya plastiki iliyokuwa imeharamishwa sasa inaonekana kwa kasi, hivi tuna tatizo gani? je?

Tuamini kwamba Dr Rais Samia akimaliza kipindi chake tutaacha kupanda miti?

Tutarudi kwenye kutumia kuni?

Tujisahihishe hii tabia haina Afya kwa Nchi yetu.
"Na Mimi nataka niseme Watanzania mtanikumbuka na mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya kwasababu nimesacrifice maisha yangu kwa wananchi masikini"
 
Naunga mkono HOJA 🙏

Mazuri ya Nabii Magu yalikuwa mengi kuliko mabaya.

Tuchukue mazuri tuyaendeleze, mabaya tuachane nayo.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
 
Mawazo hakuuwawa? Saanane? Lissu hakupigwa risasi? Azory gwanda? Na JPM mwenyewe alimpa maagizo Ndugai kuwa awatimue bungeni ili wakitoka nje awashughulikie!! Alafu mnataka kumtetea huyi mkatili?

Mimi binafsi kata nayoishi kuna wafanyabiashara wakubwa wawili walikua ndio wanadhamini CHADEMA. Moja ana hardware kubwa sana mwingine ni mwanajeshi mstaafu, eeh bwana JPM alipoingia alihakikisha anawaharass biashara zao na kutishia kuzifunga. So mpaka inafika 2020 hata pesa ya kulipia kodi ya ofisi ilikua kipengele. Imagine hiyo ni kata moja? Je kwingine ilikuaje hali? Acheni kutetea ujinga.
Hoja yangu ni kwamba huwa mnajicontradict kwenye maelezo yenu linapokuja suala la Magufuli, tumesikia mengi sana kutoka kwenu.

Utasikia kipindi cha Magufuli watu hawakuwa wakikosoa sababu walikuwa wanamuogopa Magufuli ila hapo hapo unaambiwa watu wengi walikuwa wanauliwa kwa kukosoa, wakati ule wa corona tulisikia Magufuli yeye kachanja chanjo ya corona kisiri na kwamba anajificha kwao kijijini anaogopa Dar kuna corona halafu kakataza chanjo ili wenzie wafe mara alivyofariki mnatuambia kafa kwa corona kwa sababu aliidharau corona.

Lengo ni kuonyesha Magufuli ni mtu mbaya bila kujali kinachoelezwa ndio ukweli au kina make sense watu hawakujali hilo, yani mtu anaweza kueleza chochote kibaya kuhusu Magufuli na watu wasitake ushahidi kwa kuwa anayezungumziwa ni Magufuli.

Simtetei Magufuli ila naonyesha tu kwamba watu huongozwa na hisia zaidi linapokuja suala la kumzungumzia Magufuli.
 
NIiwakumbushe tu kitu kimoja, ukiyabeza ya mwenzio ya kwako yatafanywa hivyo hiyo.

Nizungumzie kitu kidogo tu cha usafi wa mazingira yetu ambalo lilikuwa ni maono ya kwanza ya JPM alipoingia madarakani, na ikapitishwa siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi watu wote tufanye usafi wa maeneo yetu.

Suala hili limezikwa pamoja naye kwani lilikuwa na ubaya gani, mifuko ya plastiki iliyokuwa imeharamishwa sasa inaonekana kwa kasi, hivi tuna tatizo gani? je?

Tuamini kwamba Dr Rais Samia akimaliza kipindi chake tutaacha kupanda miti?

Tutarudi kwenye kutumia kuni?

Tujisahihishe hii tabia haina Afya kwa Nchi yetu.
Mambo yameshaharibika sana - jk
 
Back
Top Bottom