Hayati Magufuli kama kuna mabaya yake tumwachie, mazuri yake twende nayo

Hao jamaa hutoweza kuwaelewa maana watakwambia kipindi cha Magufuli watu wengi walimuogopa hivyo hawakuwa wakimkosoa wala kumpinga ila hapo hapo watakwambia watu wengi waliuliwa kimya kimya kwa kumkosoa na kumpinga Magufuli.
Hakubaliki na hatokubalika
 
Ubaya wa hali ya juu sana
 
Kwa sisi tuliopo nje ya nchi hatukuona kiongozi bora kama magufuli...sifa zake na mambo yake makubwa tulikuwa tukiyaona ata uku marekani ....tukasema basi nchi yetu itafika pale inapotakiwa kufika lakini punde si punde mauti hayoooo..


Yote kwa yote magufuli alikuwa kiongozi bora
 
"Na Mimi nataka niseme Watanzania mtanikumbuka na mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya kwasababu nimesacrifice maisha yangu kwa wananchi masikini"
 
Naunga mkono HOJA 🙏

Mazuri ya Nabii Magu yalikuwa mengi kuliko mabaya.

Tuchukue mazuri tuyaendeleze, mabaya tuachane nayo.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
 
Hoja yangu ni kwamba huwa mnajicontradict kwenye maelezo yenu linapokuja suala la Magufuli, tumesikia mengi sana kutoka kwenu.

Utasikia kipindi cha Magufuli watu hawakuwa wakikosoa sababu walikuwa wanamuogopa Magufuli ila hapo hapo unaambiwa watu wengi walikuwa wanauliwa kwa kukosoa, wakati ule wa corona tulisikia Magufuli yeye kachanja chanjo ya corona kisiri na kwamba anajificha kwao kijijini anaogopa Dar kuna corona halafu kakataza chanjo ili wenzie wafe mara alivyofariki mnatuambia kafa kwa corona kwa sababu aliidharau corona.

Lengo ni kuonyesha Magufuli ni mtu mbaya bila kujali kinachoelezwa ndio ukweli au kina make sense watu hawakujali hilo, yani mtu anaweza kueleza chochote kibaya kuhusu Magufuli na watu wasitake ushahidi kwa kuwa anayezungumziwa ni Magufuli.

Simtetei Magufuli ila naonyesha tu kwamba watu huongozwa na hisia zaidi linapokuja suala la kumzungumzia Magufuli.
 
Mambo yameshaharibika sana - jk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…