Hayati Magufuli kuagwa bungeni Dodoma kesho, wabunge wengi wamlilia

Hayati Magufuli kuagwa bungeni Dodoma kesho, wabunge wengi wamlilia

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Kesho bunge la JMT litapata fursa ya kumuaga hayati Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania ambaye pia ni sehemu ya bunge.
Shughuli za kuaga zitafanyikia kwenye viwanja vya bunge.

Wabunge wengi wameonyesha hudhuni kubwa akiwemo mbunge wa Morogoro kusini babu Tale ambaye aliahidiwa kujengewa barabara za jimboni kwake na mwendazake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mungu ampe pumziko la milele...

Kuna waswahili baadhi wanadai watu wamekodishwa Uhuru + kulia


Hili limekaaje?
 
Apumzike Kwa Amani
Amelala Mauti
Tutamkumbuka Sana
 
Mungu ampe pumziko la milele...

Kuna waswahili baadhi wanadai watu wamekodishwa Uhuru + kulia


Hili limekaaje?
Akina mnyika nao walikodishwa jana.hao kila kitu kupinga mpk kwenye msiba wao ni kupinga tu
 
Lazima wamlilie hao maana bila yeye kutumia nguvu wasingefika hapo mjengoni.watalia sana esta bulaya,halima mdee na wenzao.
 
Kesho bunge la JMT litapata fursa ya kumuaga hayati Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania ambaye pia ni sehemu ya bunge.
Shughuli za kuaga zitafanyikia kwenye viwanja vya bunge.

Wabunge wengi wameonyesha hudhuni kubwa akiwemo mbunge wa Morogoro kusini babu Tale ambaye aliahidiwa kujengewa barabara za jimboni kwake na mwendazake.

Maendeleo hayana vyama!
COVID 19 watakuwepo????
 
This is too much.
Ni mwendo wa kuchomekea ratiba juu ya ratiba. It is time consuming, Costful and complicated protocol.

Maiti anazungushwa kama dagaa, hii sio sawa sana. Kama mheshimiwa marehemu ilipangwa kesho kuagwa Dodoma kitaifa, basi viongozi wote (ikiwemo wabunge) na wananchi wajumuike kumuaga uwanja wa Jamhuri. Sio kila kikundi katika maeneo yao ya kazi waletewe marehemu kumuaga.

Usishangae ukisikia, CCM nao watamuaga kwenye ukumbi wao, mara wanachuo wa UDOM watamuaka chuoni kwao, mara atapelekwa Ikulu ya Chamwino ili watumishi wake wamuage nk.
 
Tangu tarehe 17 mwezi march Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha rais Magufuli.
Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!
Kitendo cha hayati rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.
Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.
Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.
Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu,
Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.
 
Back
Top Bottom