game over
JF-Expert Member
- Jan 1, 2016
- 10,727
- 24,840
Moja kwa moja kwenye mada.
Haya ni baadhi ya mafanikio hayati JPM aliyapata akiwa kama Rais wa JMT kwa awamu moja.
1. Ujenzi wa Miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, vituo vya afya nk.
Ujenzi wa bwawa la umeme la Mwl. Nyerere ulihitaji uthubutu wa hali ya juu hasa ukizingatia vita iliyokuwepo dhidi ya mradi huu toka kwa jamii za wanaharakati wa kimataifa na baadhi ya wanasiasa uchwara (waafrica).
JPM alifanikiwa sana kwenye hili eneo tangu akiwa Waziri na hata alipokuwa Rais, Mh Jakaya Kikwete alifanikiwa sana kwenye ujenzi wa Barabara na madaraja kwa sababu ya uwepo wa Jembe JPM kama Waziri wake wa Wizara husika. Kuna wakati walitokea wanasiasa wapumbavu wakasema hawataki maendeleo ya vitu, Huu ni upumbvavu wa hali ya juu uliotokana na kokosa agenda. Hakuna nchi duniani inayoendelea bila kuwa na maendeleo ya Vitu.
Ni lazima kuwe na maendeleo ya vitu ili yalete maendeleo ya watu. Hiyo hatua haiepukiki.
2. Kufufua Shirika la ndege la Air Tanzania. Tunajua umuhimu wa shirika la ndege hasa kwenye utalii, ukizingatia potential tuliyonayo kwenye sekta ya utalii. Ilikuwa ni aibu sana kwa nchi inayongiza dola karibu bilioni 2 kila mwaka kwa utalii halafu kusiwe na shirika la ndege.
3. Kulinda na kusimamia vema rasilimali za nchi, ikumbukwe awamu ya nne tembo waliwindwa kwa kasi kiasi kwamba waliwekwa kwenye kundi la endangered species na twiga wakapanda ndege. Hapa pia reforms zilizofanyika kwenye Mining industry zimekuwa na manufaa kwa serikali na wachimbaji hasa wadogo ambao ni wengi sana. (walioko kwenye hii industry wanaelewa), among many.
4. Kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma, ikiwemo kuwaondoa wale wenye vyeti feki. Ilifika mahala watu wakaona nini haja ya kupoteza muda darasani, watu walipeana kazi kwa connections na upendeleo.
5. Alituheshimisha watu weusi, ambapo hadi sasa anazungumzwa kama Shujaa, aliyekuwa na uthubutu, nia njema kwa watu wake, na a true Pan Africanist. Haya ni Maoni ya walio wengi Tanzania, Africa na kwingineko duniani. Hii ilituheshimisha sana kama nchi.
6. Alitukumbusha watanzania kuwajibika na kuacha kuishi kwa mazoea, kama tunavyofahamu watanzania wengi ni wavivu na wazembe, na hawako tayari kuwajibika, hata walioko kwenye huduma za umma. Wao huwa ni kuangalia mianya ya upigaji tu, kazi kwao wala sio muhimu. Ndio maana kifo chake bado kinafurahiwa na baadhi ya wapumbavu wachache, wengine wapo humu JF.
7. Uchumi wan nchi uliimarika kutoka Lower Income hadi Lower Middle income Economy
8. Alisimama imara akaivusha nchi wakati wa janga la Korona, Uganda wamefungua mashule mwaka huu.
9. Upigaji serikalini ulipungua sana
10. Na mengineyo mengi.
Mwisho. Kuna namna tumepiga hatua kama nchi, ila bado Nchi yetu ni masikini (Very Poor). Siasa zetu pia ni za kipuuzi mno. Tuambizane tu ukweli. Tutachukua muda sana kusogea mbele. Pamoja na mambo mengine mengi ikiwemo wananchi kujituma kwa nafasi zao,, tunahitaji viongozi wazalendo, wenye maono, bidii na uthubutu kama JPM. Apumzike kwa Amani.
Muwe na siku njema.