KWELI Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa mwenyekiti wa chama chake tangu 1954 mapaka 1977

KWELI Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa mwenyekiti wa chama chake tangu 1954 mapaka 1977

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Kumekuwa na post ya Jenerali Ulimwengu aliyoichapisha kwenye mtandao wa X kwamba Mwalimu Julius Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa chama chake kuanzia mwaka 1954 mpaka 1977, ukweli wa kauli hii upoje?

Screenshot 2024-09-08 234221.png

 
Tunachokijua
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania na kilianzishwa mwaka 1992 na kupata usajili wa kudumu mwaka 1993 mara baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Kwa mujibu wa tovuti ya Chama Cha Mapinduzi, Chama kilianza rasmi Februari 5, 1977 kutokana na kuunganishwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa chama tawala Tanzania Bara, kikiongozwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala Zanzibar kikiongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Amani Abeid Karume.

Mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu kupitia Akaunti yake kwenye mtandao wa X aliandika kuhusu muda aliokaa madarakani Hayati Mwalimu Julius Nyerere kama mwenyekiti wa chama chake tangu mwaka 1954 mpaka 1990 akihusianisha na namna ambavyo watu wakihoji juu ya muda mrefu ambao Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekuwepo madarakani.

Je ukweli ni upi?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia utafutaji wa kimtandao umebaini Freeman Mbowe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti (tazama ukurasa wa 18) wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuanzia mwaka 2004 hadi hivi sasa 2024, akipokea kijiti hicho kutoka kwa Bob Makani ikiwa ni jumla ya miaka ishirini (20)mpaka sasa, lakini pia Freeman Mbowe amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Hai.
CHADEMA-National-Chairman-Freeman-Mbowe.jpg
Aidha tumebaini Hayati Mwalimu Julius Nyerere amewahi kuwa waziri mkuu wa Tanganyika na baadaye kuwa Rais wa Tanganyika mwaka 1961 na baadaye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya Tanganyika kuungana na Zanzibar mwaka 1964.

Mwalimu Nyerere alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha TANU (Tanganyika African National Union) kati ya mwaka 1954 hadi 1977 na baadaye akaendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kati ya mwaka 1977 hadi 1990 kabla ya mrithi wake Hayati Ali Hassan Mwinyi Rais wa wa pili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupokea kijiti cha uenyekiti mwaka 1990.

Hivyo Mwalimu Nyerere aliiongoza TANU kwa miaka 23 Na baadaye CCM kwa miaka 13.

julius-nyerere.jpg
Back
Top Bottom