Hayati Ndugai anazikwa kwa Ibada ya Kanisa ama na Bunge?

Kitimoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2012
Posts
8,198
Reaction score
9,911
-1578539565.jpg

Nimeona kwenye msalaba wa marehemu limeanza na neno "Mhe." (ambalo nadhani linamaanisha Mheshimiwa). Kama mazishi haya yanafanywa na Bunge, basi hiyo ni sawa na stahiki ya heshima kwa nafasi yake ya kitaifa ila kwanini watumie msalaba.

Lakini kama ni ibada ya Kanisa, ningetarajia msalaba huo uandikwe kwa namna ya kiimani kwa mfano, majina matatu aliyobatizwa nayo, kama ilivyo kawaida katika ibada za Kikristo.

Je, huu ni mchanganyiko wa heshima za kidunia na za kiroho?
Wapi mpaka unawekwa? Maana ibada ya Kanisa ina utaratibu wake.

Nawasilisha kama swali na pia tafakari kwa jamii.
 
Dah! Mpaka mtu anafikia hatua ya kuwa marehemu, bado anaitwa Mheshimiwa!! Wahusika wanatakiwa kutambua huo tayari ni udongo, na pia chakula cha viumbe hai wa ardhini..

Wanadamu tutambue thamani yetu ni pale tu tunapokuwa hai. Tukishakufa, na thamani yako nayo inafikia tamati.
 
Masharti ya kanisa ni kwako wewe mdanganyika kapuku. Wakifa viongozi taratibu zinapindiswa tu.

Kingunge tuliambiwa alirudi kundini masaa machache kabla ya kufa na akazikwa na kanisa kama kawaida.
 
View attachment 3438271

Hakuna kinachoenda mbinguni, na si dhambi siku ya mwiso utambulisho wa marehemu kuwekwa kwenye msalaba au kaburi, kama ilivyo Dr, Rev, Prof, Gen, Inspector n.k
Ni utambuisho wa marehemu huku duniani, hata majina tuliyobatizwa duniani yanabakia duniani pia, hayatumiki huko paradiso au akhera
So kwa kaburi unaweza andika chochote kilichomhusu marehemu kabla ya mauti
 
Nafikiri jamaa ametoa angalizo muhimu. Mhe Kuna wakati unaisha na ukishakufa ndio basi tena. Ndugai atakuwa amevunja rekodi ya kuwa mhe hata akiwa kwenye jeneza. RIP Ndugai
Kuna shida gani kwenye msalaba kuandika titles za marehemu? i.e Rev, Dr, Bishop, Gen, Inspector, Prof n.k kama umekufa ukiwa unazitumikia???
 
Ni upuuzi tu. Huko kwenye imani za kikanisa hakuna huo upuuzi. Jina lako rasmi ndilo unalotambulika nalo. Kwa Mungu wewe ni binadamu kama binadamu wengine, haijalishi mamlaka yako.
 
Dah! Mpaka mtu anafikia hatua ya kuwa marehemu, bado anaitwa Mheshimiwa!! Wahusika wanatakiwa kutambua huo tayari ni udongo, na pia chakula cha viumbe hai wa ardhini..

Wanadamu tutambue thamani yetu ni pale tu tunapokuwa hai. Tukishakufa, na thamani yako nayo inafikia tamati.
Mkuu wewe kwenye maswala yote Uko Sawa na una akili vizuri tu.
Ila likiwa swala la Yanga ni balaa
 
Mkuu
Acha Mambo Yaende Kumbuka Haya Maisha Job Ameyamaliza
 
Ni upuuzi tu. Huko kwenye imani za kikanisa hakuna huo upuuzi. Jina lako rasmi ndilo unalotambulika nalo. Kwa Mungu wewe ni binadamu kama binadamu wengine, haijalishi mamlaka yako.
upuuzi gani? kwani amezikwa kenye property yako? kwa culture nyingi hiyo ni acceptable, hata kama unamchukia ndyo ulichukie hata kaburi lake?
  • When someone you didn't get along with dies, many complex and challenging grief emotions can follow.
  • It is understandable and normal to feel a sense of relief, or even happiness, when someone you intensely dislike or hate dies
 
Masharti ya kanisa ni kwako wewe mdanganyika kapuku. Wakifa viongozi taratibu zinapindiswa tu.

Kingunge tuliambiwa alirudi kundini masaa machache kabla ya kufa na akazikwa na kanisa kama kawaida.
Maskini hawana nafasi katika makanisa ya wakristo hasa protestant and catholic
 
Malkia Elizabeth alivuliwa vyeo vyote na akazikwa kama Elizabeth, huku kwetu wanatafuta sifa
hiyo ni monarch system, ni mfumo tofauti sana
In monarchies, the death of a king or queen (demise of the crown) automatically transfers power to the designated heir, often the eldest child, without a formal dethroning process.
 
Back
Top Bottom